Sherehe za Mei Mosi Tanga, JK mgeni rasmi

Hiyo inaitwa twanga kotekote. CCM inasalimiwa kila mahali ila haitaki kuitikia.
 
ndio JK kamaliza kutoa zawadi za wafanyakazi bora na sasa Katibu Mkuu TUCTA (Bw. Mgaya) anatoa salam za wafanyakazi
 
Acha uongo wewe. Sherehe zimenoga sana. Na hapa tulipo, Uwanja wa Mkwakwani umefurika na hadi watu wamekaa ndani ya uwanja wa mpira! naona JF siku hizi imevamiwa na wapotoshaji wakubwa.
 
Wafanyakazi hatuikubali TUCTA ya kina Mgaya na JK walokula deal naye kutunyonga
 
Ukiangalie mpangilio mzima wa hiyo sherehe na hotuba (na hata salamu) ni wazi kabisa kuwa Mgaya ameshawauza wafanyakazi. Ni propaganda tupu.

Sijaelewa ni kwanini jumuiya wa wafanyakazi inategemea wafadhili toka nje i.e balozi za nje!
 
mgaya anasema wafanyakazi wa tanzania wanaishi kwa kubangaiza na hata nyuso za wengi wao zimekata tamaa na kuna wengi tools down kama madaktari
 
anasema wengi wanapokaribia kustaafu wanaomba ku-extend ajira kwa mikataba kwa vile mstaafu wa nchi hii ni kituko
 
Kima cha chini kitafika laki 2 ifikapo 2016 mbona JK kashawaona wafanyakazi mazoba! Wajanja wanapiga deal na kuondoka na mamilioni hata viongozi wa TUCTA wameambulia kama unavyowaona hapo Tanga
 
mgaya anaiponda tume ya rais ya ajira maana anadai wafanyakazi hawajaona ilichofanya licha ya pesa nyingi.
Anaiponda serikali kwa tangazo la kushusha mishahara na posho wakati hali ya uchumi inapanda
 
anaongelea kodi kwa wafanyakazi kwamba watumishi walio kwenye payroll (kama milioni 2) ndio wanaotozwa kodi tena kubwa sana ilihali wafanyakazi nchi hii ni milioni 20 katika sekta zote. Kama serikali ingekusanya kwa wote hawa, mzigo wa kodi kwa mfanyakazi wa umma ungepungua
 
Naona uwanja leo haujajaa kama ilivyozoeleka

wewe umesema hivi, na huyu karipoti hiv

Tanga kwetu
Re: LIVE kutoka Mkwakwani Stadium kwenye Mei Mosi Kitaifa
watu ni wengi...uwanja umefurika...majukwaa yamependeza kwa sare
Nani tumwamini? Mnatuzingua sasa.
 
anashauri misamaha ya kodi ipunguzwe (anasema misamaha ya kodi mwaka jani ilikuwa ni 2% ya GDP around trilioni 3, Kenya ilikuwa 1.2% GDP)
 
Wana bodi,
Kutoka Tanga mjini, response ya wafanyakazi ni Ndogo Mno...pole pole tu tutafika, tutang'oa mzizi wa fitina,huyu Mgeni Rasmi ndo Mwanzo wa kila tatizo linaltukabili kwa Sasa....

Mwanzo wa kila tatizo linalokukabili ni wewe mwenyewe,usimsingizie JK. Wewe ni Mvivu wa kufanya kazi,mvivu wa kufikiri,unaiba muda wa mwajiri,mbadhirifu wa mali ya umma kwa kiwango chako,mkwepaji kulipa kodi,kila kitu unafanya kwa manufaa yako si ya manufaa ya nchi n.k. Jitazame kwanza wewe mwenyewe!
 
anashauri serikali ipanue wigo wa vyanzo vya kodi pia kupunguza matumizi ya serikali ikiwemo hospitality, ukubwa wa misafara ya viongozi wa serikali kwa safari za ndani na nje
 
mgaya anaiponda tume ya rais ya ajira maana anadai wafanyakazi hawajaona ilichofanya licha ya pesa nyingi.
Anaiponda serikali kwa tangazo la kushusha mishahara na posho wakati hali ya uchumi inapanda

yaani hali ya maisha imepanda then mishahara imeshuka!
Wabunge wenyewe wanadai nyongeza sasa iweje mfanyakazi??
Huyu jk hayupo serious kbs
 
kuhusu wage bill anasema ni 30% ya watumishi wa umma ndio wanakula 60% ya wage bill lakini serikali inaongopa kwa kujitetea kwamba haiwezi kuongeza mishahara kwa sababu ya ukubwa wa wage bill
 
Back
Top Bottom