Sherehe za Mei Mosi Tanga, JK mgeni rasmi

Arusha Mambo:

Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete, leo ndiye Mgeni rasmi kwenye Sherehe za Mei Mosi zinazofanyika kitaifa Mjini Tanga, muda huu maandamano ya wafanyakazi yameanza kuingia uwanjani na baadaye wafanyakazi hao watahutubiwa na Mh Rais wakiwa na shauku kubwa ya kutakuwa na nini katika hutuba yake kitakachosaidia kupunguza ugumu wao wa maisha,

Sikiliza tukio hili kupitia Arusha Mambo Internet Radio, visit www.arushamambo.com click "Sikiliza Arusha Mambo FM...." Page ya Tune IN ikifunguka tafadhali LIKE our Radio.

Source: Arusha Mambo.
 
siku ya wafanyakazi,bendera za CCM za nini uwanjani? Au kuna chama cha wafanyakazi wa CCM kinawakilisha? Siku ya leo kwa maoni yangu ilitakiwa isiwe na itikadi kwani kuna baadhi ya wafanyakazi ni wanachama wa vyama vingine vya siasa.

Taabu yetu kubwa kila kitu cha kitaifa kinafanywa CHA CHAMA TAWALA!
 
Ningekuwa raisi nisingedhubutu kumchukua mke wangu niende nae kwenye sikukuu ya mei day.

Sababu ni kuwa wafanyakazi wanahali mbaya kuliko kawaida, gharama za sherehe ni kubwa zaweza fikia nusu ya deni la wafanyakazi wote!
 
Subiri Spreech ya Bw. Mkubwa ndo utachoka siunajua kila akipata platform lazima atoe mipasho!Kikao cha CC ndo itabeba speech yake.
 
Duh! CUF ndani ya maandamano!! hii kali wanaleta mambo ya Zanzibar Tanganyika!
 
Hali ni mbaya hapa uwanjani,wafanyakazi wanalazimishwa kuonyesha hali ya shangwe,nderemo na vifijo wapitapo jukwaa kuu,huku mabango yao yakibeba ujumbe wa manung'uniko na kulia kwa ugumu wa maisha,mishahara duni, tofauti na shangwe wanazoimizwa wazioneshe kwa mkuu wa nchi.

My take:
MWONGOZA SHEREHE ASIWALAZIMISHE WAFANYAKAZI JINSI YA KUPITA JUKWAA KUU.WAFANYAKAZI WAACHWE WAONYESHE HISIA ZAO KWA HALI WAITAKAYO WAO.
 
hakuna jipya leo kwa jk zaid ya ahadi hewa kama kawaida yake, sherehe zinendelea!
ushabiki wa kisiasa hata mahali pasipotakiwa, watu wanaingia uwanjani wakiimba ccm!,ccm! bado hawajajitambua
 
Hata kusimama blaza anasimama kwa shida sana nadhani blaza kichwa kinauma
 
watanzania tunadanganywa kirahisi na tumejaa uoga.Nchi hii ni yetu sote na tuna haki ya kula matunda yake kwa usawa,hakuna aliye mtanzania kuliko mwingine.
 
Back
Top Bottom