Sherehe za Mei Mosi Tanga, JK mgeni rasmi

Sherehe za Mei Mosi Tanga, JK mgeni rasmi

Lion's Claws

Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
30
Reaction score
14
Leo ni siku ya wafanyakazi duniani. JK atazungumza na wafanyakazi kupitia sherehe za mei mosi. Atakuwa na jipya la kuwaambia wafanyakazi maana amekuwa hatekelezi ahadi zake?

Amesahau alipowaambia wafanyakazi akili zao wachanganye na za mbayuwayu wakati wa mgomo wao na kuwaambi wagome hata miaka minane kamwe hawataongezewa mishahara?

Leo mshahara uko palepale wakati mfumko wa bei ni mkubwa na wafanyakazi wanakatwa kodi kubwa kuliko hat wafanyabiashara.
 
Wafanyakazi wana maisha magumu sana. Si ajabu kuwa hadi leo tarehe 1 wapo ambao hawajapata mishahara. Mei 1 ya tz ni hadaa kwa wafanyakazi. Uliza wafanyakazi wa udom
 
Hey,
Nimekuwa nafanya analysis
Thamani ya mfanyakazi wa umma imeahuka kwa mshahara kiduchu.
Ndio maaana ufisadi umeongezeka.... Mtu akipata kazi ni kufikiria jinsi ya kuiba....

Nilienda kijijini kwangu, afisa mtendaji anapokea rushwa kama hana akili mzuri

Wafanyabiasha menoooo njeeeeee
Wanapiga faida kama kawa, kodi hawalipi ama ni kidogo!! Biashara za magendo ni kibao, tena wanashirikiana na viongozi wa siasa!!!

Mfanyabiashara wa ana capital milioni 20 kodi kwa mwaka analipa elfu 90
Mfanyakazi mshahara laki tatu kodi kwa mwezi 15,000/=

Nchi ovyoooooo

Poleni wafanyakazi hasa walimuuuuuuuu
 
Yaan utashanga ataongea ugoro wake huo na wake (cuf) zake watashangilia!!

Mimi nashindwa kuelewa sijui Tz inatumia mfumo gani wa utawala yaani serikali ime-fail kila nyanja! Hivi Kikwete leo utasimama jukwaani kuwaeleza nini wafanyakazi wa Tanzania kwa jinsi unavowanyonga!? Mfumko wa bei, ujira mdogo, kodi kubwa na mazingira mabovu ya kazi?

Yeye utamuona akitabasamu tu as if nchi iko salama! Ajira hakuna kwa vijana bado mmeanza kutuchinja kama ng'ombe! Hivi Kikwete aliingia Ikulu kufanya lipi!!??

Kikwete nchi huiwezi STEPDOWN!!
 
Naomba kufahamu mfanyakazi anapaswa kutozwa kodi asilimia ngapi ya mshahara wake? Nimeongea hivyo kwani capitalist mmoja kaniajiri na ananikata kodi %14. Basic yangu ni 550000 so nakatwa 77500. Je ni sahihi?
 
kodi kubwa sana tunakatwa inabidi serikali ipunguze kodi ni mzigo kwa mfanya kazi wa serikali watafute vyanzo vingine vya mapato kwa mfano wanaopangisha hawatoi kodi kabisa, wafanya biashara wengi wana kwepa kodi kwa nn wasiwabane wakwepa kodi waongeze mapato kuliko kumpora mfanya kazi kamshahara kake wakati hata hakatoshi.
 
Kauli mbiu ya Mei Mosi mwaka huu "Mishahara duni, kodi kubwa na mfumko mkubwa wa bei ni pigo kwa wafanyakazi" Maadhimisho kitaifa yanafanyika jijini Tanga na mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.
 
Kila siku ni Jei Ef Day.. Enjoy mamii...
 
Pamoja na kodi kubwa lililo kubwa kuliko yote ni tofauti kubwa ya mishahara.

Tutaongea kila neno kuhusu vipato lakini kama kuna wachache wanayamudu maisha kwa unono wa vipato vyao ni kazi bure.
Pili ni faraja ya watu wachache waipatayo kwa njia mbadala isiyo rasmi iitwayo UFISADI.

Wafanyakazi wengi huridhika kupitia ka udhalimu hako.Wengi hata wanapoomba kazi hawaulizi mshahara huuliza mianya ya rushwa.

Tatu,tupiganie kuimarisha uchumi na thamani ya fedha yetu kwa kudhibiti raslimali zetu na kupromote kilimo kwa kuongeza uhuru wa soko na kuongeza viwanda.

BILA KUDHIBITI UFISADI KILA KITU NI KAZI BURE NI SAWA NA KUJAZA PIPA LENYE MATOBO KIBAO.
 
Mbele vyama dhaifu vya wafanyakazi huku vikihujumiwa na UWT (Usalama Wa Taifa)....
Kila siku kelele zitendelea kuwa hizi hizi...
Full kupotea hii nchi
 
hahaa TANMO... Me nlidhan jf day ni 2nayoweza meet wanajf wa eneo hucka tukabadilishana mawil matatu ama nakosea?
 
Mei mosi enzi za mwalimu sasa ni ufisadi hadi kwenye mei day.
 
Back
Top Bottom