Nimekuwa nikifatilia hali ya kiasa inavyokwenda pamoja na mbio za urais zilivo hapa Tanzania ila nashangaa sana kuona Wanzania ambao wamekuwa wahanga wa matokeo ya uongozi mbovu wamekuwa wafuasi wazuri wa uongozi huohuo.
Tanzania sasa ina deni linalofikia trilion tzs 22, maisha yanazidi kuwa magumu sana, afya ianzidi kurudi nyuma, elimu ndo usiseme, nishati tunaona kinachofanywa na viongozi wetu tuliowaamini, juzi mmeona na kusoma siri kubwa iliyo nyuma ya gesi from Mtwara to Dar es salaam, hizi zote ni hila na njama mbovu za watawala walioapa kuifilisi nchi kwa kiwango cha juu.
Nimeona mheshimiwa Shelukindo akimendorse Edward Lowasa for president 2015, huu ni upumbavu na njaa ya watanzania wenye mawazo kama haya, ni ujinga na ewendawazimu uliokithiri kipimo, ni uayawani usio na kipimo, ni ulevi wa madaraka na upungufu wa maono, ni ufedhuli na uasi kwa Watanzania, ni ukosefu wa huruma na ulafi wa kiwango cha oscar award, haya hayavumiliki hata kidogo.
Naongea kwa masikitiko makubwa sana kuona watanzania walioshiriki kwa kiasi kikubwa kudhorotesha maendeleo ya watnzania walio wengi ndo wanaopigiwa chapuo ya urasi, mfumo mbovu na utindio wa ubongo wa watanzania walio na uwezo kimamlaka, wametumia loophole ya ubumbuazi wa watanzania kujineemesha huku na wale walioudhuria shule bila kuelimika wakifuata nyuma bila kujua siri iliyo ndani ya mtungi.
Tunamjua Lowasa, si mchapakazi hata siku moja kwani sifa za wachapakazi zinajulikana, yeye ni mjasiri wa kutumia mabavu hata kma jambo sio yeye anaweza kufosi kulipitisha kama alivolazimisha njia tatu kipindi cha kupunguza foleni ingawa alishauliwa sana na wataalam akagoma na tulishuhudia vifo vingi sana vya watanzania walioathirika na maamuzi Magumu, Kweny msafara wake huyu mheshimiwa, tunamuona Chenge, Tunamuona Kalamagi, Tunamuona Rostam, Tunamuona Selukamba, na wengine wengi sana, lazima tujiulize,unapoona haya majina, kwa kutumia akili ya kawaida unahisi nini? Je hii nguvu na pesa inayotumika kuutafuta uraisi inarudi vipi!
Tuwe makini na hawa watu kama kweli tunataka kuiona Tanzania katika sura nyingine.