Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

r.i.p sheikh yahya .....inna illalah rajuun....


pole sana JK na wengine wote ...

Mwenyezi Mungu anasema ni bora kumtumainia yeye kuliko mwana adam..!!!
 
Ndugu wa Jamii,

Poleni sana kwa Msiba wa Mnajimu Mkuu wa Tanzania na Afrika Mashariki,

R.I.P sheikh Yahaya Hussein,

Watanzania tusiwe na tabia ya kufurahia mtu akifa,vitabu vitakatifu vinatufundisha kulia na kuomboleza,na wafiwa,tuachane na tabia/siasa za chuki,sisi watanzania ni wamoja na wapenda amani.
 
lol hiki kigagula kaaga?? hakutabiri?

Yahya Mtabiri????!! Mweeeh!!!

RIP Shekh Yahaya Poleni CCM

Pole sana Jakaya Kikwete na wafiwa kama habari hizi zinaukweli!

alikuwa anaweka usiku sana kwenye maendeleo ya nchi.....akavune alichokipanda kudadadeki....

sasa hivi shehe yahaya yuko na mabikira 80 anajivinjari nao....

Mkuu kupata bikira lazima ujilipue kwa bomu au kujiua huku ukiua wengine

huo ni utabiri au yameshatokea! tatizo litakuwa kubwa zaidi kwa wale wanaolindwa na yeye! namanisha wale waliopewa ulinzi na yeye!

Nina uhakika maandalizi ya kupata mlinzi mbadala yameshafanyika. He was a stateman, teheh tehe heh teheh haaaahaa ha

The info is true!

Mzee Yahya in no more, wamepeleka mwili wake Lugalo muda si mrefu.

Poleni wafiwa wote!


Hapo kwenye red, was he black amiri jeshi mkuu mpaka mwili upelekwe Lugalo hosp na si muhimbili?

angekuwa mnajimu huyo ni mwanamke angepewa watu gani? kwahiyo hata watu wakifa Uzinzi unaendelea tu!.
Imani zingine…..

Tatizoina bidi wakazi wa dar wakae vizuri maana yale majini yake hayana pa kwenda

Yatawaendea wateja wake tu, mnaopenda kwenda magogoni kazi kwenu…maana kule aliyaweka yeye kumlinda mkulu

ha ninashaka na khabari hizi!mbona sijaskia wimbo wa taifa?

Cd zimegoma, ulinzi aliouweka nao umetoweka.

pumzika kwa amani mzee Sheikh yahya, u will be remembered by many people.
For good or for worse?

Ni kweli sheh wa ukweli wa ccm kafariki R.I.P
duuuuuh

Huu ni msiba wa kitaifa ; itabidi Jakaya Kikwete arudi haraka toka Namibia asimamie mazishi ya kamanda!!!
Atangaze pia mapumziko ya kitaifa angalau siku mbili, bendera zote zipepee nusu mlingoti kwa majuma mawili
 
Kweli huyu alikuwa mnajimu, maana alitabiri kifo chake: alitabiri kuwa mwaka huu mtu maarufu atafariki- nadhani ndo utabiri umetimia.
 
kumbe hata yeye amekufa,nlidhani anatabiria wengine kufa kana kwamba yeye hataonja umauti.
Rest in pieces sheikh
 
Atakaye pingana na Jakaya Kikwete ndani ya ccm kwenye kinyan'ganyiro cha uchaguzi atafariki dunia-sheik yahaya
 
Hivi karibuni mnajimu maarufu sheikh Yahya Hussein alisema kuna baadhi ya wabunge wataburuzwa mahakamani kwa kashfa. tangu atoe kauli hiyo ni miezi sasa. hivi sasa sakata la takukuru na wabunge limeshika kasi. jee takukuru itaburuza wabunge mahakamani? Je, haya ndio matabiri ya Sheikh Yahya yakitimia?

Sasa anakuja na hii:

Sheikh Yahya: Atakayempinga 2010 Kikwete kufa!

Na Exuper Kachenje

MNAJIMU mashuhuri katika Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amemtabiria ushindi wa kishindo, Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwakani na kwamba atakayejitokeza kumpinga kiongozi huyo katika kuwania nafasi hiyo, atakufa ghafla.

"Natabiri kuwa Kikwete ndiye Rais mpya wa mwaka 2010 na atakayempinga katika chama chake atakufa ghafla. Natabiri ushindi wa Rais Kikwete mwakani utaleta serikali ya mseto Tanzania Bara na Tanzania Visiwani," alisema Shekhe Yahya.

Alisema kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Lawrence Gama, ni ishara ya ushindi mkubwa wa Rais Kikwete katika uchaguzi wa mwakani. Alisema kifo hicho ni ishara kwa Rais Kikwete kushinda kura za maoni na kupata tiketi ya CCM, ili kugombea urais katika muhula wa pili.

Alisema njia kwa Rais Kikwete kuingia tena Ikulu ni nyeupe na kwamba wale watakaoshindana naye, watasambaratika kwa sababu uongozi wa Kikwete ni urithi kutoka kwa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema wakati wa uhai wake, Mwalimu Nyerere, aliamuru Kikwete kumuachia Rais mstaafu Benjamin Mkapa, nafasi ya kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 1995 na kwamba hiyo ilikuja baada ya Kikwete kushinda katika kura za maoni.

"Kwa hiyo Kikwete alirithi urais huu kutoka kwa Nyerere. Ngoja awamu ijayo, mwachie Mkapa, kauli hiyo bado haijafutwa kwani mirathi kutoka kwa mwalimu ni ya awamu mbili," alisema Shekhe Yahya.

Mnajimu huyo pia alitabiri kutokea kwa kifo cha kiongozi mmoja wa zamani wa kitaifa katika kipindi cha ya kati ya sasa na Aprili mwakani.

Kuhusu mapambano ya ufisadi hasa kuelekea uchaguzi mkuu mwakani, mtabiri huyo alisema vita hiyo inakwamishwa na wabunge ambao alisema wanawajua mafisadi.

ebu jikumbushe
 
Mods,
Unganisheni threads za tukio hili iwepo moja, zatuchanganya na repeated threads.
 
Habari


Sheikh Yahya:Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Septemba 15, 2010
rC.jpg
bul2.gif
Asema hahitaji ruksa ya CCM, serikali
LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kumkana, Mnajimu maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein, ameibuka na kusema kwamba hahitaji kibali katika kumwekea "ulinzi wa majini" mtu anayempenda - Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumzia kauli za viongozi wa CCM na Serikali kwamba hawatambui "ulinzi wa majini" aliosema atautoa kwa Kikwete, Sheikh Yahya, amesema: "Sihitaji kibali cha yeyote kumuwekea rais wangu ulinzi wa majini."
Sheikh Yahya, ambaye amekuwa akitoa kauli tata kuhusiana na Kikwete hata kabla ya kampeni kuanza, alisema, jana, jijini, kuwa anachozungumzia yeye si uchawi wala ushirikina; bali ni mambo ambayo yapo na hayakwepeki.
"Kila mtu anazaliwa na jini. Hata Slaa (Dk.Willibrod Slaa, Mgombea urais wa CHADEMA) ana jini anaitwa Subiani. Nakwambia sihitaji kumshirikisha mtu katika hili," alisema Sheikh Yahya Hussein na kumkabidhi simu mwanae aliyejitambulisha kwa jina la Hassan, ambaye naye alisema;
"Sheikh alisema binafsi hahitaji kumshirikisha mtu katika hili. Serikali iendelee na ulinzi wake na yeye atatoa ulinzi wake. Mbona hao walinzi walikuwapo lakini akaanguka? Matatizo yale si ya kiafya. Sheikh anafanya kwa kuwa anampenda na hutasikia tena anaanguka."
Awali Sheikh Yahya alinukuliwa katika taarifa yake akisema kwamba atatoa ulinzi usioonekana kwa macho kumkinga Rais Kikwete ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia ‘mchezo' wowote kama ilivyotokea Jangwani.

Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.

Kufuatia kauli hiyo, Dk. Slaa alikemea kauli hiyo na kusema: "Nchi haiwezi kuongozwa na uchawi. Haiongozwi na imani za watu, kila mtu ana imani yake, lakini tusifike mahali tukaongoza nchi kwa uchawi."

Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kumkemea Sheikh Yahya kwa kauli hiyo iliyotolewa juzi Dar es Salaam, la sivyo wananchi wataamini mnajimu huyo anatumiwa na CCM kuleta hofu katika jamii.

Dk. Slaa aliwakumbusha wananchi kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Sheikh Yahya alisema mtu yeyote atakayegombea urais na Kikwete atakufa na kuongeza: "Sisi wengine ni majabali, hatuogopi kufa kwa ushirikina."
Tayari serikali imesema haihusiki na hoja ya ‘ulinzi' usioonekana kwa Rais Kikwete, kama ilivyotangazwa na Sheikh Yahaya.
Hata hivyo, Sheikh Yahya alisema hakuwa anazungumzia uchawi wala nguvu za giza, "bali majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao".

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana, alisema Rais Kikwete ni muumini wa Dini ya Kiislamu, ambaye anaamini Mungu na hivyo hahusiki kwa vyovyote na kauli ya Sheikh Yahya.
Kauli hiyo ya Sheikh Yahya imeibua mjadala mkali; huku baadhi ya wananchi wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike kuangalia kama kuna fedha za umma zinazotumika kugharamia masuala ya ushirikina.
Baadhi ya wananachi hao, wakiwamo viongozi wa dini, wamekemea tabia ya baadhi ya viongozi kukimbilia katika imani za ushirikina baadhi wakitumia raslimali za umma katika kugharamia imani hizo.
Rais Kikwete amepata kuanguka hadharani mara tatu; mara ya mwisho ikiwa ni wakati akizindua kampeni yake ya urais, hivi karibuni, katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
Alipata pia kukiri hadharani kwamba alimsaidia Sheikh Yahya fedha za kwenda matibabuni nje ya nchi.
 
Innallilahi waina illaihi rajiun ndio mwisho wa safari ya kila mja. Tena amefariki siku nzuri ya ijumaa. Shida ipo katika matendo yake kwakweli yalikuwa yanatusikitisha waislamu wengi inshallah mmungu amuhidi kwa yale aliyokuwa akiyafanya duniani kwani sote sie ni wanaadamu na hakuna mkamilifu duniani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom