Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

RIP yahahya.
Kusema kweli nilikua sikupendi, hasa katika kile kipindi chako cha chanel ten cha uchawi na majini.
 
Hakika bench la ufundi la JK limepata pigo, sasa tutegemee mieleka ya hapa na pale kwani ulinzi usioonekana umeondoka, pole sana JK. Dalili ya mvua ni mawingu, CCM kwishney.
 
Confirmed
Mnajimu na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar es Salaam.
Chanzo chetu cha habari ndani ya ofisi ya Sheikh Yahya kimesema mtabiri huyo amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitali ya Ukombozi iliyopo Morocco, jijini.
Sheikh Yahya amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na aliwahi kwenda India kwa matibabu. Habari zaidi tutawaletea katika mtandao huu na magazeti yetu.


Source: Global publishers


My take;

Pole JMK, this time ccm hawana mtetezi na muaguaji
 
Mbona mnashangaa? mlitaka aishi milele? Amekufa nyerere sembuse Sheikh Yahya!
 
binafsi alikuwa ananikera kweli kweli, bora sasa mambo ya utabiri yatapungua kama sio kwisha, Pole JK
 
Waefeso 6:10-12 unasema hivi

10Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu. 11Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana na hila zote za shetani. 12Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
 
huu ni msiba mkubwa, kwakuwa kazi za mzee huyu watu waliziamini na wengi walimuabudu yeye badala y anaestahili kuabudiwa
 
Habari


Sheikh Yahya:Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Septemba 15, 2010
rC.jpg
bul2.gif
Asema hahitaji ruksa ya CCM, serikali
LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kumkana, Mnajimu maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein, ameibuka na kusema kwamba hahitaji kibali katika kumwekea "ulinzi wa majini" mtu anayempenda - Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumzia kauli za viongozi wa CCM na Serikali kwamba hawatambui "ulinzi wa majini" aliosema atautoa kwa Kikwete, Sheikh Yahya, amesema: "Sihitaji kibali cha yeyote kumuwekea rais wangu ulinzi wa majini."
Sheikh Yahya, ambaye amekuwa akitoa kauli tata kuhusiana na Kikwete hata kabla ya kampeni kuanza, alisema, jana, jijini, kuwa anachozungumzia yeye si uchawi wala ushirikina; bali ni mambo ambayo yapo na hayakwepeki.
“Kila mtu anazaliwa na jini. Hata Slaa (Dk.Willibrod Slaa, Mgombea urais wa CHADEMA) ana jini anaitwa Subiani. Nakwambia sihitaji kumshirikisha mtu katika hili," alisema Sheikh Yahya Hussein na kumkabidhi simu mwanae aliyejitambulisha kwa jina la Hassan, ambaye naye alisema;
"Sheikh alisema binafsi hahitaji kumshirikisha mtu katika hili. Serikali iendelee na ulinzi wake na yeye atatoa ulinzi wake. Mbona hao walinzi walikuwapo lakini akaanguka? Matatizo yale si ya kiafya. Sheikh anafanya kwa kuwa anampenda na hutasikia tena anaanguka."
Awali Sheikh Yahya alinukuliwa katika taarifa yake akisema kwamba atatoa ulinzi usioonekana kwa macho kumkinga Rais Kikwete ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia ‘mchezo' wowote kama ilivyotokea Jangwani.

Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.

Kufuatia kauli hiyo, Dk. Slaa alikemea kauli hiyo na kusema: "Nchi haiwezi kuongozwa na uchawi. Haiongozwi na imani za watu, kila mtu ana imani yake, lakini tusifike mahali tukaongoza nchi kwa uchawi."

Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kumkemea Sheikh Yahya kwa kauli hiyo iliyotolewa juzi Dar es Salaam, la sivyo wananchi wataamini mnajimu huyo anatumiwa na CCM kuleta hofu katika jamii.

Dk. Slaa aliwakumbusha wananchi kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Sheikh Yahya alisema mtu yeyote atakayegombea urais na Kikwete atakufa na kuongeza: "Sisi wengine ni majabali, hatuogopi kufa kwa ushirikina."
Tayari serikali imesema haihusiki na hoja ya ‘ulinzi' usioonekana kwa Rais Kikwete, kama ilivyotangazwa na Sheikh Yahaya.
Hata hivyo, Sheikh Yahya alisema hakuwa anazungumzia uchawi wala nguvu za giza, "bali majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao".

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana, alisema Rais Kikwete ni muumini wa Dini ya Kiislamu, ambaye anaamini Mungu na hivyo hahusiki kwa vyovyote na kauli ya Sheikh Yahya.
Kauli hiyo ya Sheikh Yahya imeibua mjadala mkali; huku baadhi ya wananchi wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike kuangalia kama kuna fedha za umma zinazotumika kugharamia masuala ya ushirikina.
Baadhi ya wananachi hao, wakiwamo viongozi wa dini, wamekemea tabia ya baadhi ya viongozi kukimbilia katika imani za ushirikina baadhi wakitumia raslimali za umma katika kugharamia imani hizo.
Rais Kikwete amepata kuanguka hadharani mara tatu; mara ya mwisho ikiwa ni wakati akizindua kampeni yake ya urais, hivi karibuni, katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
Alipata pia kukiri hadharani kwamba alimsaidia Sheikh Yahya fedha za kwenda matibabuni nje ya nchi.


bora akapumzike tu! kwa hiyo hata mimi nina jini?
 
Kwa mujibu wa Radio 1 breaking news Sheikh Mkuu Issa Bin Simba ni kweli Sheikh Yahaya amefariki leo na atazikwa kesho


Iweje azikwe kesho wakat moslem dead body kwa heshima unazkwa b4 24 hours since passed away? Nyw na me ngoja nijipange kuja kwenye mazishi ya mzee wetu mpendwa.
 
so sad, alikuwa anaumwa? mwenye kujua atujuvye.

poleni familia ya marehemu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom