Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

Mpita Njia

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
6,999
Reaction score
1,188
He died this morning at his Magomeni home.
Kwa mujibu wa mwanawe aitwaye Hassan, Sheikh yahya amefariki kutokana na heart failure. Aliamka asubuhi ya leo akiwa buheri wa afya, akaanza kazi yake ya kuona wenye matatizo wanaokuja kwake.

Kama kwenye saa tatu hivi, akaanza kujisikia vibaya, akapewa glasi ya juisi lakini hali haikutulia. wakaamua kumkimbiza katika hospitali moja maeneo ya Morocco na alipofikishwa hapo madaktari wakasema tayari ameshafariki dunia.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake na atazikwa kesho jijini Dar.

Ameimaliza safari yake. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH YAHYA HUSSEIN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya Hussein kufuatia kifo cha Mnajimu Mkuu huyo kilichotokea asubuhi ya leo tarehe 20 Mei, 2011, katika Hospitali ya Mount Ukombozi iliyoko Morocco Jijini Dar es Salaam.


"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kipaji chake katika masuala ya unajimu wa nyota ambao ulimpatia sifa kubwa," amesema Rais Kikwete katika rambirambi zake.


Ameongeza: "Naomba, kama familia, mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi muhimu na tegemeo kubwa la familia. Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amina."


Amesema Rais Kikwete katika salamu zake: "Naelewa fika machungu mliyonayo katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu. Najua alikuwa mzazi, alikuwa baba, alikuwa babu, alikuwa mlezi na tegemeo kubwa la familia. Najua ameacha pengo kubwa ambalo litakuwa gumu kuzibika. Najua mko katika kipindi kigumu na cha majaribio. Hivyo nawaombeni muwe na moyo wa uvumilivu na subira. Yote ni mapenzi ya Mola. Napenda kuwahakikishieni kuwa niko nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba wa mpendwa wenu."


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

20 Mei, 2011
 
Mtabiri na Mnajimu mashuhuri Afrika Mashariki amefariki dunia dakika zipato 20 zilizopita.
Rip Mnajimu

Masharobaro source ni Jamii Forums
 
ya kweli hayoooo?maana washawahi mzushia khabari ka hizi..
 
RIP

Poleni sana wafiwa, mungu awe nanyi katika kipindi hiki kigumu.
 
Huyu hadi azikwe ndio tutaamini habari hii, aliwahi kum-bipu Mungu mwaka jana baadae tukaambiwa yu hai!

R.I.P. Sheikh Yahya.
 
alikuwa anaweka usiku sana kwenye maendeleo ya nchi.....akavune alichokipanda kudadadeki....

Du!..hata sikusikia kama kaumwa karibuni..!Kama kweli apumzike anapostahili..Mganga hajigangi,lol!!
 
huo ni utabiri au yameshatokea! tatizo litakuwa kubwa zaidi kwa wale wanaolindwa na yeye! namanisha wale waliopewa ulinzi na yeye!
 
Kama ni kweli itabidi JK akatishe kikao cha SADC NAMIBIA aje kumzika uyu mnajimu wake.
 
The info is true!

Mzee Yahya in no more, wamepeleka mwili wake Lugalo muda si mrefu.

Poleni wafiwa wote!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom