Lyimo
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,826
- 2,017
juzi Sheikh Ponda Issa ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu alitanabahisha kuwa iwapo serikali haitoweka kipengele cha dini katika fomu za sensa ya mwaka, jumuiya yao itahamasisha Waislamu wasishiriki katika zoezi la sensa.Alisema kuwa nchi hii siyo ya Kikristo lakini INATAWALIWA NA MFUMO KRISTO. alisema kutokana na mazoea, Waislamu wanabaguliwa katika mgawanyo wa keki ya taifa khasa upande wa ajira. ofisi na idara za serikali zinaongozwa na Wakristo kwa asilimia kubwa kulinganishwa na waislamu. alitoa mfano wa TRA, NECTA, Wizara ya Eimu, Wizara ya Ujenzi, Afya, Mahakama nk........... kwa mujibu wa Sheikh Ponda, wastani wa ajira ni karibu Wakristo 77% na Waisalmu siyo zaidi ya asilimia 20%. Licha ya hoja inayojengwa kuwa Waislamu hawajasoma lakini akasema waliosoma wapo. akatanabahisha kuwa kwa maslahi na umoja wa kitaifa, kupuuza watu ambao ni sehemu ya jamii ktk keki ya taifa ni jambo hatari sana! kwa kuwa wtu wanadai waislamu ni chini ya 20% katika nchi hii, akapendekeza sensa ya mwaka huu kiwekwe kipengele cha dini ili idadi ya watanzania kidini ijulikane. Kwa mujibu wa Sheihk Ponda, anaamini kuwa waislamu ni takriban 64% ya rais wa Tanzania. "SIYO SAHIHI WATU WENYE IDADI HII KUPUUZWA KATIKA UWIANO WA AJIRA SERIKALINI", alisema Sheikh Ponda.Alitoa mifano wa nchi karibia zote za Ulaya, Marekani, asia pamoja na Afrika, kipengele cha dili kipo kwenye fomu za sensa zao. "Ukisoma country profile au fact file uingiapo katika nchi mbalimbali, utakuta wameandika wastani wa idada ya raia kidini" alisisitiza Ponda. "Mbona mnajifanya kama hamtembei au hamjui kinacho endelea ulimwengunu jamani!" alilalama Ponda.HOJA YANGUNdugu znaguni Watanzania, tufike sehemu tuache ukweli udhihiri. kama Waislamu wanalalamika kuwa wanabaguliwa katika ajira labda kutokana na uchache wao, kwa nini suala la dini lisiwekwe wazi? au utakua udini? au uchochezi? au uvunjifu wa amani? kama ni hivyo, mbona karibu 98% ya sensa zote duniani zina kipengele cha dini!? je huko wameuana kutoakana na kipengele hicho? TUBADILIKE!!!!!!!!naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Naona hii habari yako umechanganya habari. Unataka kutuaminisha kuwa, kuhusu keki ya Taifa huwa inagawiwa kufuata dini? Pia unataka kutuaminisha kuwa Dini ndiyo interview ya kupata kazi? Badala ya kung'ang'ania kazi za upendeleo maalumu, ningeshauri watanzania tujikite kwenye elimu kisawasawa kwanza na kipigania mazingira ya elimu.