Sheikh Mussa Kundecha - Nilipewa Kesi Ya Mauaji

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,318
24,218
Sheikh Mussa Kundecha asimulia kashikashi nyingi alizopitia akiwa mwanaharakati Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=rDaa_3GLI2Y&

Kiongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu asimulia jinsi alivyopewa kesi ya mauaji baada ya kutoafikiana na Polisi waliolazimisha aongee mbele ya vyombo vya habari kituo cha Polisi awaombe Waislamu waliokuwa na mpango wa kuandamana wasifanye hivyo. ...

Wakati huo Polisi Dar es Salaam mkuu wa upelelezi mkoa ni RCO Abdallah Zombe anaongoza .... nikatupwa selo asubuhi mahakamani nikasomewa kesi ya mauaji ya watu wawili kwa risasi mmoja askari polisi na mwingine raia, kutoka hapo nikapelekwa rumande Segerea miezi 6 ....

Kuhusu siasa Sheikh Mussa Kundecha anasema huwezi tenganisha siasa na dini.

Upande wa elimu anaelezea umuhimu wa suala hilo ... nilisoma Tabora kisha kwenda nje Burundi, Kenya, Saudi Arabia kuongeza elimu nikarudi Tanzania nikafundisha Tabora, Arusha na Dar es Salaam mitaa wa Kiungi Magomeni pia Kinondoni Mkwajuni na msikiti wa Kichangani Magomeni.

Mihadhara ya MwembeChai iliyoshamiri kuanzia mwaka 1994 hadi 1997 jijini Dar es Salaam iliniletea matatizo miaka hiyo ikiongozwa na kina sheikh Mazinge na wengine ...

Pia nilifanya kazi ya kuunganisha waislamu ambao ni wasomi (professionals) wa elimu pana ya kisecular na masheikh wa wanaotoa elimu ya dini, kwani makundi haya mawili yaani professionals wa kiislamu waliona masheikh wao hawana ufahamu wa masomo ya elimu ya secular huku pia masheikh wakiona waislamu wasomi kuwa hawana ufahamu wa dini yao.

Harakati hizi zimeleta mafanikio kuna misikiti zaidi ya 3,000 na huku kuna shule zaidi ya 300 za waislamu kutokana na kuunganisha nguvu za waislamu ....

Mussa Kundecha anaulizwa sheikh ni nani hasa ... pamoja ya kuwa sheikh ni kama inatumika kuonesha kuwa ni mtu mzima isipokuwa katika utaratibu ....

Sheikh Mussa Kundecha akiangalia mbele kuhusu kupata elimu ya dini, anashukuru kuwa mazingira yanazidi kuwa mazuri vitabu vipo vingi tofauti na zamani hapa Tanzania kilikuwapo kitabu kimoja cha Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy .. sasa kuna vingi zaidi ...

Kuhusu BAKWATA - Baraza Kuu La Waislamu Tanzania kutokubaliwa na baadhi ya waislamu, Sheikh Mussa Kundecha anasema kila mmoja ana nafasi yake hivyo ...

Wateja wengi wa Islamic Banking Tanzania ni wale wasio waislamu na wamewapita kwa idadi kubwa huku waislamu wakiwa wachache hivyo ni jambo jema la kijamii kwa wasio waislamu kuwa wengi sana kwa idadi ktk Benki za Kiislamu ...anabainisha Sheikh Kundecha..
 
Dah. Huwa namkumbuka Mwajuma Kundecha, binti mmoja mrembo sana alisomaga IFM miaka hiyo, sijui ni mtoto wa shekh?
 
Hakika wanaharakati kama sheikh Mussa Kundecha waendelee kufunguka jinsi mfumo wa haki jinai (criminal justice system) unavyoweza kutumika ndivyo sivyo.
 
Sheikh Msellem mwanaharakati wa uamsho toka Dogwe Zanzibar alivyoishia gerezani kutokana na masuala ya sensa na pia katiba


View: https://m.youtube.com/watch?v=68L5Fxb33J4

Suala la dodoso letu la kipengele cha dini katika sensa tulipata maadui toka pande zote ikuwemo CUF na pia CCM chama tawala wakatuchukia anabainisha Sheikh Mselem ..

Uamsho tuliunga azimio la katiba mpya ya serikali tatu, moja ndogo ya sovereignty ya Muungano, pia ya Tanganyika na ile ya Zanzibar tunashukuru jaji Warioba alitusikiliza ikawekwa kwenye rasimu .... lakini sijui nini kilitokea ...

Jela sisi wenyewe kwa wenyewe tulihitafiliana, tukawana tunachongeana


View: https://m.youtube.com/watch?v=JtmZmYhlNlo

Anaongeza sheikh Mselem kuwa hilo jambo si Tanzania bali kote ulimwengu uislamu tunavurugana wenyewe kwa wenyewe ....
 
Back
Top Bottom