Sheikh Ponda yuko sahihi

Nafikiri imefika wakati kila mtu mwenye akili timamu kukemea hii non sense na hawa akina ponda. Mimi nishangaa serikali kwa nini inamfumbia macho mrundi huyu. Mna agenda gani na mrundi huyu? Hivi waislamu mnataka tuamini maneno anayosema ponda mnakubaliana nayo???????? Unajua kuna mambo mtu mzima anaongea unajiuliza alimaliza kunyonya lini maana kama ameanza angalau kutembea hawezi kuwa na akili hizi. Hivi kujua waislamu wako wangapi kwenye sensa inatusaidia nini? Wanaotetea wazo hili watuambie na sisi tujue!!!!!! Ponda anajua maana ya sensa? Moja ya kazi ya data za sensa ni kujua namna ya kugawa raslimali za nchi kwa usawa. Je idadi ya waislamu inatusaidiaje hapa? au kwenye elimu, afya, miundo mbinu n.k. Kuna huduma za waislamu peke yao na wakristo peke yao? Au kuna agenda ya siri kuhusiana na suala la Ponda? Kwani Zanzibar walitumia kigezo cha katiba wakachoma makanisa, kwa mtindo huo anataka kutumia kigezo cha sensa achome makanisa huku bara. This time we are fed up, kama akileta huo ujanja wake hatutavumilia. Wakristo tumevumilia sana vitendo hivi vya kijinga. Tumechoka, enough is enough.
Suala la ajira, aliyekuwa katika Wizara hiyo kwa muda mrefu (Hawa Ghasia) alikuwa mkristo? Rais wa nchi hii ambaye ndiye mwajiri mkuu ni mkristo? Makamu wa Rais ni Mkristo? Acheni majungu na kuunga mkono mawazo ya watu wajinga. Natamani kujua elimu ya Ponda maana sitaki hata kumwita sheikh kwani naamini sheikh ni mtu mwadilifu, mcha Mungu si mtu mhuni anayetamani kuona watu wakimwaga damu kwa mambo ambayo hayana tija kwa nchi yetu. Mgawanyo wa ajira unafanywa kwa kutumia dini? Haya mambo gani ya ajabu haya? Kwa hiyo kama umesoma sana dini ya kiislamu hata kama huna qualification upewe ajira? Hivi ambao wasimamia ajira wote ni wakristo?
Nafikiri ifike mahali waislamu wakatae watu kama Ponda kwani wanafika mahali wanawadhalilisha waislamu ambao mimi ninaamini ni watu wenye akili safi na wanaofahamu ukweli wa kila jambo.
grndossy,
Mbona lengo la Ponda ni wazi kabisa? Yeye kishatamka kuwa Waislamu ni 64% ya population ya Tanzania. Kitakachofuata ni kutangaza Tanzania kuwa ni nchi ya Kiislamu. Lengo lake liko wazi kabisa.
 
Hayo yote walisha analyse wakubwa wakaona alot of confusions exists unapoingiza swala la udini kwenye mipango ya nchi.kulingana na Sheikh Ponda anadai waislamu wamebaguliwa kwenye mgawanyo wa national cake,ina maana kuwa kwenye ajira za nchi hii waislamu wanawekwa pembeni.Hii siyo sahihi hata kidogo kwani unapoongelea swala la ajira ni kwamba ajira zinatolewa kwa ushindani.mwajiri anataka yule best candidate ndio atapewa kazi.kama ukija kupitia takwimu na kukuta waislamu ni wachache kwenye ajira ya serikali ina maana gani ni kwamba si wazuri katika soko la ajira,yaani hawana ushindani.Kwa vile mwajiri lengo lake ni kupata mtu aliye mzuri ili aje asaidie kutimiza malengo yake, ni lazima atachukua the best candidate bila ya kuangalia other criteria.Huwezi ukaacha watu wazuri kwenye soko ukachukua wabovu eti tu kwa vile ni waislamu.Chukulia wewe una biashara yako ya usafirishaji,unataka kuajiri dereva,wewe ni muislamu wamekuja watu wawili ambao mmoja ni muislamu na mwingine ni mkristo.Katika uchunguzi wako pamoja na interview ulizo wafanyia hawa watu wawili you are certain kuwa yule mkristo ni dereva mzuri kuliko yule muislamu.Na kuna all indications kwamba ukimuajiri huyo muislamu hata kaa muda mrefu kabla hajaibinua hiyo gari.Yule mkristo anautulivu wa hali ya juu na ni mjuzi kwelikweli wa kuendesha magari.Je uta opt kuajiri muislamu mwenzako katika biashara yako kwa sababu tu ni muislamu,bila kujali hasara utakazopata kwenye biashara hiyo ambayo mtaji wake umekopa bank na umeweka nyumba yako kama colateral.

mkuu wangu naona kama bado hujanielewa vizuri... sijasema wala sitasema kama waislam wanabanwa na mfumo wa ajira uliopo..... kwa sababu sina ushahidi na hilo...hoja yangu ulikuwa ni umuhimu wa kujua imani(dini) ya mtu hasa kwenye suala la sensa. hapa sikuzungumzia uislam pekee. Nilichotaka kuelezea ni umuhimu wa kujua takwimu za imani za watu hasa katika kufanya maamuzi mbalimbali ya maendeleo. Tuache kuhusu uislam .....kwani tatizo la waislam katika ajira linajulikana toka zamani.....Kwa mfano unahitaji dereva wa lori lako ulilokopa liweze kufanya kazi siku 7 kwa wiki ili uweze kulipa deni.... na unawasaili madereva wawili... mkristo (msabato) ni mzuri kuliko yule muislam... sasa hapo huoni kama ni dini ndiyo itakusaidia katika kufanya uamuzi???? Aidha ukubali kulitumia lori lako kwa siku 6 (mkristo) au siku 7(muislam). hoja yangu ndiyo ilikuwa hapo yaani kwa namna gani dini(imani) ya mtu inavyosaidia katika kufanya maamuzi.
nawasilisha mkuu
 
Wakuu heshima kwenu,

Mkuu Jasusi kagusia kidogo sensa ya mwaka 1967 ngoja niwawekee kwa faida ya mjadala.


Takwimu ya dini[hariri] Sensa ya 1967

Takwimu ya dini nchini Tanzania kwa sasa haipatikani kwa sababu maswali kuhusu dini yaliondolewa na serikali katika sensa baada ya mwaka 1967. Sensa ile ya tarehe 27 Agosti ilihesabu wafuasi wa dini za jadi kuwa 34.3%, Wakristo 33.5% na Waislamu 31.4%, mbali na wengineo 0.8%.[SUP][1][/SUP]
[hariri] Namba zenye athira ya kisiasa

Tangu mwaka ule swali la takwimu ya kidini Tanzania limejadiliwa sana inaonekana ni swali lenye uzito wa kisiasa pamoja na upande wake wa kitaalamu.
Kwa miaka mingi makadirio ya kawaida yalikuwa Watanzania ni theluthi 1 wafuasi wa dini za jadi, theluthi 1 Waislamu na theluthi 1 Wakristo.[SUP][2][/SUP]
Lakini ni wazi ya kwamba dadi ya wafuasi wa dini za jadi imeendelea kupungua. Baadhi ya viongozi na wanaelimu-jamii wanakadiria kwamba jumuia za Kikristo na Kiislamu zipo sawa tu kwa ukubwa, zote huhesabiwa kiasi cha asilimia 30 hadi 40 kwa idadi ya wakazi, na waliosalia ni waumini wa imani zingine, dini za jadi, na wale wasio na dini kabisa.
Lakini wataalamu wengine wanasema uwiano huo unashikiliwa kisiasa kwa sababu uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu ni jambo la siasa ya taifa kwa hiyo makadirio yanaelekea kutaja uwiano sawa kati ya pande hizi mbili.[SUP][3][/SUP]
[hariri] Mifano ya makadirio mbalimbali

Kwa hiyo namba zote kuhusu takwimu ya dini nchini Tanzania ni makadirio tu hakuna namba za kutegemea. Vyanzo vinavyotaja namba vinatofautiana sana mara nyingi kufuatana dini ya wahariri.

  • "World Christian Encyclopedia" (toleo la pili, Oxford 2001) imekadiria kwa mwaka 2000 Wakristo kuwa 50.4 % (Wakatoliki 24.7%, Waprotestanti mbalimbali 16.5%, Waanglikana 7.9%, wasio na madhehebu maalumu 3.5%, madhehebu huru 1.9%, madhehebu yasiyokubali imani ya msingi ya Wakristo wengine wote 0.1%, wenye kufuata madhehebu mawili kwa wakati mmoja 4.2%), Waislamu 31.8%, wafuasi wa dini za jadi 16.1% na wengineo 1.8%. Pia imetabiria kwa mwaka 2025 uwiano kuwa 56.1, 32.8, 8.9 na 2.1%, na kwamba kufikia mwaka 2050 Wakristo na Waislamu watakuwa karibu 65 na 35% kati ya wakazi wa nchi.


  • Takwimu zinazoonyeshwa na Waislamu hudai kundi kubwa la Watanzania kuwa Waislamu wakiwa na asilimia 50 - 60 za watu wa nchi [SUP][5][/SUP]

  • Kuna shirika za Kiislamu zinazotabiri Tanzania itakuwa nchi ya Waislamu wengi mnamo mwaka 2020 [SUP][6][/SUP]
Pande zote zinarejea takwimu za kuongezeka za watu katika maeneo fulani wakiongeza makadirio yao juu ya matokeo kwenye namba za kidini.

Source; wikipedia.
 
Nafikiri imefika wakati kila mtu mwenye akili timamu kukemea hii non sense na hawa akina ponda. Mimi nishangaa serikali kwa nini inamfumbia macho mrundi huyu. Mna agenda gani na mrundi huyu? Hivi waislamu mnataka tuamini maneno anayosema ponda mnakubaliana nayo???????? Unajua kuna mambo mtu mzima anaongea unajiuliza alimaliza kunyonya lini maana kama ameanza angalau kutembea hawezi kuwa na akili hizi. Hivi kujua waislamu wako wangapi kwenye sensa inatusaidia nini? Wanaotetea wazo hili watuambie na sisi tujue!!!!!! Ponda anajua maana ya sensa? Moja ya kazi ya data za sensa ni kujua namna ya kugawa raslimali za nchi kwa usawa. Je idadi ya waislamu inatusaidiaje hapa? au kwenye elimu, afya, miundo mbinu n.k. Kuna huduma za waislamu peke yao na wakristo peke yao? Au kuna agenda ya siri kuhusiana na suala la Ponda? Kwani Zanzibar walitumia kigezo cha katiba wakachoma makanisa, kwa mtindo huo anataka kutumia kigezo cha sensa achome makanisa huku bara. This time we are fed up, kama akileta huo ujanja wake hatutavumilia. Wakristo tumevumilia sana vitendo hivi vya kijinga. Tumechoka, enough is enough.
Suala la ajira, aliyekuwa katika Wizara hiyo kwa muda mrefu (Hawa Ghasia) alikuwa mkristo? Rais wa nchi hii ambaye ndiye mwajiri mkuu ni mkristo? Makamu wa Rais ni Mkristo? Acheni majungu na kuunga mkono mawazo ya watu wajinga. Natamani kujua elimu ya Ponda maana sitaki hata kumwita sheikh kwani naamini sheikh ni mtu mwadilifu, mcha Mungu si mtu mhuni anayetamani kuona watu wakimwaga damu kwa mambo ambayo hayana tija kwa nchi yetu. Mgawanyo wa ajira unafanywa kwa kutumia dini? Haya mambo gani ya ajabu haya? Kwa hiyo kama umesoma sana dini ya kiislamu hata kama huna qualification upewe ajira? Hivi ambao wasimamia ajira wote ni wakristo?
Nafikiri ifike mahali waislamu wakatae watu kama Ponda kwani wanafika mahali wanawadhalilisha waislamu ambao mimi ninaamini ni watu wenye akili safi na wanaofahamu ukweli wa kila jambo.
grndossy,
Mbona lengo la Ponda liko wazi kabisa? Ameshasema kuwa Waislamu wa Tanzania ni 64%. Sijui amepata wapi hizo takwim. Na kwa mantiki hiyo kwamba Waislamu ndiyo majority, sitashangaa akihitimisha kuwa Tanzania ni nchi ya Kiislamu.
 
Sihitaji kujua idadi ya waislam wala wakristu, wingi wa makanisa na misikiti si kujua wingi wa waumini, mkishajua halafu iweje?mbona waislam mnapenda sana uchochezi?
 
Si kweli kwamba Marekani kwenye sensa wanahesabu ufuasi wa dini. Hicho kifungu kinachotaja dini ya mtu sijawahi kukiona.
Mkuu wewe huoni mtego hapa??

Kama NECTA inalalamikiwa na Mkristo anatakiwa kuondoka kwasababu hawezi kusimamia maslahi ya waislamu wakati yeye sio mwislamu....

Je, kipengele cha dini kikiingizwa, nani atafanya kazi ya kuwahesabu waislam ambao wanalalamika waktristo wanawachakachua??

STUKA!!!

Itabidi data clerk wote wawe waislamu au kuwe na vituo vya kuhesabia makaratasi ya sensa kila mtaa.
Huu ni muendelezo wa ulalamishi.........ulalamishi hautaishia kwenye sensa tu!!!
 
Step II.

Bado naendelea kumsaidia Sheikh Ponda.

Tanzania mikoa ya kanda ya ziwa ndiyo yenye idadi kubwa ya watu Tanzania ikufuatiwa na mikoa ya kanda ya kaskazini.Ukanda wa Pwani ukiondoa [Dar es Salaam] ni mikoa yenye idadi ndogo ya watu.
 
Jaman waislam hawatakaa waishi kwa amani mpk mwisho wa dunia, nadhan walitakiwa kuwa na dunia yao ingawa sidhan sana kama ingesaidia maana tunaona huko afghanistan shia na suni!wakristo wanautaratibu wao wa kujua idadi ya waumini wao nenda makao makuu kkkt utaambiwa au R.c sasa wao kwann wanashindwa kujua hilo,?hebu mtu aseme hapa ambae amesoma shule isiyo ya dini wapi shule umewahi kukuta darasa lina wanafunz wengi waislam kuliko wakristo?sasa itakuwaje kwenye soko la ajira uwiano uwe sawa?angalia mtaa unaoishi vjana wengi ambao wapo wapo tu bila mwelekeo ni wa dini gan?MAFUNDISHO YA KIKRISTO YANATWAMBIA TUPENDE WATU WOTE BILA KUJALI DINI ZETU. TUNAWAPENDA ILA MALALAMIKO YENU YANABOA MNO JAMAN MAANA MARA NYINGI HAYàNA MANTIK
 
Inaonekana hawa mashehe hata kujumlisha hesabu hawawezi. Ni rahisi tu, piga azana saa kumi wasilamu wote klia kaya wakutane msikitini kuhesabiana, baadae matokeo ya vituo yanapelekwa kata hadi Bakwata kujumlishwa, Tena ndo mtapata wasilamu halali si kama huyu mke wangu msilamu (BI,ASHA) ambaye nimemuoa nikiwa KAMA kafir wa allaha
 
Wasukukuma tuko kama 8m ambayo ni 20% ya Watanzania. Vipi hilo Sheikh Ponda from Burundi?

..Kuna sensa yoyote mliyofanya kudhibitisha idadi hiyo ya Wasukuma?the last time ichecked Tanzania haijawahi kuweka kipengele cha kabila kwenye sensa...

...Binafsi namuunga mkono Sheikh kwa hilli, na isiishie hapo, pia ni vyema kipengele cha kabila pia kiwekwe, tusijichukie tulivyo, hiyo ndio Tanzania, yenye dini mbalimbali na makabila mbalimbali, kujua idadi hiyo na kuenezwa kwa udini au ukabila ni vitu viwili tofauti...
 
Sheikh Ponda amejipa kazi ya kuenesha shari nchi hii. Pengine ni kwa sababu ya tatizo la ajira, lakini sioni ni kwa vipi waislam watakaa chini na kumsikiliza huyu semi-illiterate!<BR><BR>Week chache zilizopita alikuwa anapiga debe kuwaunga UAMSHO, sasa makanisha yamechomwa kakimbilia kwenye sensa! UAMSHO kawaacha kwenye mataa! Ni aina ya ma-sheikh kama hawa wanaoudhalilisha uislam. Hana la maana alilofanyia hii nchi zaidi ya kugawa watu.

Pole sana hujui hata unachokiandika kuhusu Ponda. Una kitu bado kinakusumbua katika elimu yako ndio maana hata ukweli akiuongea mtu asiye kuwa wewe bado hutaki kuuona kama ni ukweli. Kwa namna hii basi hili ni tatizo
 
Hahahaaa mmesahau yule Mkurugenzi alivywajibu? Kuwa maendeleo ya nchi hayapimwi kwa kigezo cha dini wala kabila la mtu. sensa inatumika katika planning ya mambo muhimu ya kimaendeleo na sio dini, tusiwe so narrow minded, hata hivyo nawashauri mtumie utaratibu kama wa kwetu wa kuandikishana, kwa mfano mimi bahasha yangu ya usharika ni No.963, that means mimi ni mkristo wa 963 katika usharika wangu kwa hio kkupata idadi ya Wakristo wote katika CCT ambapo ndipo nasali, unachukua idadi ya waliojiandikisha mara idadi ya makanisa uliyonayo katika huo mkoa, wilaya au taifa. Na kwa taarifa yako hata tunapojiandikisha tunaandika kiasi unachotegenea kumtolea MUNGU kwa mwaka huo na hii husaidia kufahamu Kanisa litakusanya kiasi gani, litumie kiasi gani na libakishe kiasi gani, kwa mfano wakati namaliza Mlimani CCT-Chaplaincy kwa kipindi hichoo tulikua na milion mia mbili na kidogo ila sifahamu ndugu zangu pale msikitini walikua na bei gani, na sisi hatuna wafadhili pia.
 
@ nyarugando
kama wewe una uwezo wa kufikiri kwa nini hupangui hoja za sheikh ponda moja baada ya nyengine!?
inaelekea wewe ndiyo una uwezo mdogo wa kufikiri.
Hebu jiulize ingia benki mfano nbc yenye wafanyakazi kama 150 kwenye tawi la posta ya zamani. kisha unakuta waislamu 5 au 6. na hawo wakristo waliopo pakitokea fursa ya ajira wanavuta ndugu, rafiki na jamaa zao ambao ni wakristo! huu ni mfano tu lkn ndiyo hali halisi. muislamu akipeleka application kuomba kazi, anapewa ahadi ili asiingie katika himaya ya mfumo kristo. sheikh ponda siyo mjinga!

alieshiba hajui shida ya mwenye njaa! NECTA inafelisha watoto wa kiislamu makusudi ili wasiende vyuo vikuu. kama huji huu unaitwa MFUMO KRISTO. kama wewe hujui kinacho endelea. walio kuzidi umri wanajua. kutoa mfano kuwa kikwete na bilal pamoja na jaji mkuu ni waislamu siyo kitu! watendaji zaidi ya 75% serikalini kama ni wakristo kikwete atafanya nini. mind u kikwete hakwenda pale kuwabeba waislamu. ni rais wa watanzania wote.

ponda anacholalamikia ni kwamba wakristo wanasema hiyo ni halali yao kuwa wengi serikalini kwa sababu kiidadi ni wengi hapa tanzania. ponda anakataa. anasema kukata mzizi wa fitna kiingizwe kipengele cha dini kwenye sensa. "uwiano wa kila jamii na kundi katika ajira ni dalili ya uadilifu na utawala bora" Martin Luther
 
Hayupo sahihi kuingilia kazi ya serikali na kutisha serikali eti atawaambia Waislam wasihesabiwe, kwanza ni kosa kuizuia serikari isifanye kazi pili sensa ni ya serikali kwa malengo yake, kwanini nae asifanye sensa ya waislam akajua idadi ?Hii bure anayoipenda ndo imeangamiza kundi lake kwa kupenda kubebwa na kutofanya juhudi ktk mambo ya msingi matokeo yake amekua akifundisha na kushawishi watu kulalamika limekua kundi la malalamiko 2
 
Pole sana hujui hata unachokiandika kuhusu Ponda. Una kitu bado kinakusumbua katika elimu yako ndio maana hata ukweli akiuongea mtu asiye kuwa wewe bado hutaki kuuona kama ni ukweli. Kwa namna hii basi hili ni tatizo

Mr.Mak, you dont need to be brain surgen kuona kinachonyemelewa hapa.
 
Akutunae hakuchagulii tusi.

Upuuzi wote huu unalelewa na mheshimewa rais kikwete. Ukihofu sana kutekeleza majukum yake, is where everyone will come up with idears good and stupidy, it is the president and his ministers to act and protect the nation. You can not leave crazy people to mislead moral citizens.

Hakika nawaabien hizi zote ni chokochoko na ni kiinimacho THE OBJECTIVE BEHIND IS TO IMPLICATE AND ESTABLISHMENT OF SHARIA LAW and THE RULE OF MAHAKAMA YA KADHI.
 
Hivi mnajua wa islam wengi wanabadili dini?...mnajua dini nyingi za kilokole wamejaa wa islam..?...na pia waislamu wengi wanaolewa na wakikrsto na kudbadili...?..fanya hiyo tafiti hata mtaa utaona..?
 
Mi naona mnatafuta sababu nyingine ya kuandamana. Mtaandamana kupinga matokeo ya sensa, mtaandamana kutaka mkurugenzi wa Takwimu naye ajiuzulu. Mi nawajua, sensa ikitoa matokeo kinyume na matarajio yenu, kesho yake wote mko barabarani. Hebu jihesabuni wenyewe tu, maana mfumo wa sensa wa sasa hauwezi kutupa majibu ya contraversial issue kama hiyo ya idadi ya waislamu.

Yani ISOTOPE unanukia udini,kujua idadi ya watu kwa didni zao sio udini yani nisawa sawa na kujua idadi ya watu kwa jinsia zao yani ME na KE sasa ukitaka kujua idadi ya Me na Ke sio kutaka kuwabagua kijinsia ila uwenda ukawa unatafta usawa wa kijinsia vile vile unaweza kujua idadi ya watu kwa didni zao ili utafte usawa wa kidini katika taifa lenye dini mbalimbali. Kwa mtazamo wangu Shekh Ponda anaitaji majibu na hili swala linazungumzika labda ukiweka udini mbele huwezi kulizungumzia.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom