Sheikh Ponda apandishwa kizimbani Morogoro

Sheikh Ponda apandishwa kizimbani Morogoro

Mkuu nisaidie uelewa kidogo. Kwani quran imetaja jina Yesu au Jesus ambaye alikuwa anasema yeye mwenyewe atakufa na siku ya tatu atafufuka kwenye Kurasa zake zozote?. Kama yule wa quran hajasema hivi basi nadhani Yesu wanaye muamini wa kristo atakua ni tofauti na Issa aliye kwenye quran na hivyo hakutakiwi kuwe na ugomvi wowote kati ya wakristo na waislamu!. Kila mmoja aheshimu imani ya mwenzake. Mbona wahindi wanaabudu N'gombe lakini hamuwakemei kwenye mihadhara!.Tuwe wavumilivu kwa imani ya kila mtu humu duniani.

na hakuna kanisa duniani linalohubiri Issa. Ukikemea pepo kwa jina la ustaadh Issa hawatoki, ila kwa jina la YESU weeee!
 
Serikali imejichanganya sana na mwishowe Sheikh Ponda ataachiwa huru...Mbona hakuna uchochezi wowote apo yani kusema waaislam wasikubali mambo ya BAKWATA nayo ni uchochezi? Ebu tafuteni uongo mwingine wa kumbambikia kesi ata ya madawa ya kulevya basi kuliko kesi za kitoto km hizi....Mbona waTZ wengi wanapinga mambo ambayo hawayaelewielewi nayo ni uchochezi? what if angesema Rais wa nchi ni muuzaji wa madawa ya kulevya na ana marafiki wengi ndo maana alikaa kimya ata baada ya majina kupewa????
mimi sioni kosa wala kinacho sababisha serikali kuhangaika na huyu mtu mmoja kila siku. wao wakae pembeni wafuatilie kile anachokifanya waone kama analketa madhala kuliko kumfanya awe maarufu kwa kitu kisichoonekana
 
Siku zote serikali za kidhalimu huwahofia wapigania haki.Anachofanyiwa sheikh Ponda ni uthibitisho mwingine wa namna serikali inavyowatendea viongozi wa kiislam.Ni wazi Kuwa nchi hainamujtama mwema
 

HUWEZI kuacha kutafsiri kwamba, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anawahenyesha askari wa Dar es Salaam tena kwa saa 24, Ijumaa Wikienda limegundua.


Hali hiyo imesababishwa na ulinzi mkali anaotakiwa kupewa Shehe Ponda na askari wa jela kwenye Magereza ya Segerea, Dar baada ya kupokea mzigo huo wa kumlinda kutoka kwa askari polisi na usalama wa taifa alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili.


Wiki mbili zilizopita akiwa kwenye mhadhara mjini Morogoro, Shehe Ponda alidai kupigwa risasi kwenye bega la kulia.

Wakati wa tukio hilo, Ponda alikuwa akisakwa na polisi kwa kosa la kutoa hotuba yenye uchochezi akiwa Zanzibar huku akijua yupo ndani ya kifungo cha nje cha mwaka mmoja ambacho kinataka asipatikane na shitaka.


Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, afande mmoja kutoka jeshi la polisi (aliomba hifadhi ya jina) alisema polisi wanamshukuru Mungu Ponda kupelekwa Seregea, wenzao wa magereza nao wakahenyeshwe na ulinzi.


“Unajua nini ndugu mwandishi? Kumlinda Ponda ni kufa na kupona, popote unapokuwa naye awepo, wenzake wanaweza kuvamia na kuvunja amani, wewe una bunduki wao hawana silaha, unafanyaje hapo?”
alisema afande huyo.


Uchunguzi zaidi wa Ijumaa Wikienda umebaini kuwa, baadhi ya askari polisi walikuwa wakikwepa kushika zamu ya kumlinda Ponda Muhimbili kwa kuona ugumu wa kudhibiti vurugu endapo wafuasi wake wangeamua kukinukisha.


Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ilimhukumu Ponda kifungo cha nje cha mwaka mmoja jela. Ponda na wafuasi wake 49 (waliachiwa huru) walidaiwa kakaidi agizo la jeshi polisi kwa kufanya maandamano haramu Februari 15, mwaka huu kwenda katika ofisi za DPP.


chanzo.
SHEIKH PONDA AWAHENYESHA POLISI SAA 24...!! ~ MAMBOMSETO
 
Sijui kwanini binafai siamini katika habari za udaku. Sasa wewe uliyeleta habari hii unataka tujadili nini
 
Magereza pimbi wewe, ndio hivi mnasema Dr. Ndalichako katumwa na Kanisa Katoliki.

Kama huko madrasa mnafundishwa ni MAJELA basi jiangalieni.
Sijakuelewa!
Unakataa kuwa jela wingi majela si neno la Kiswahili (limeazimwa kutoka lugha ya kiingereza kama kawaida ya Kiswahili) au unalikataa kuwa si Kiswahili sahihi katika standard ya baraza la mitihani?
 
kiswahili fasaha ni Jela,umoja ni JELA WINGI NI JELA
MFANO JELA IMEJAA
WINGI ITAKUWA JELA ZIMEJAA
Fasaha kwa standard ya nani?

Mimi ninasema Moja ni jela wingi majela (ma tunatumia sana kwa kitu kisichopendeza) hivyo majela yamejaa.
Mkoroshokigoli said:
JELA NI NOMINO AU JINA LILILO KWENYE NGELI YA I-ZI
Kule nilikotokea kanuni zetu za kimatumizi chochote kisichopendeza mara nyingi huanziwa na MA. mfano,mahabusu (asili yake habsi, hubisa), magereza, majitu (lafidhi nyingine mijitu), mahayawani...
 
Ukiandika hiki kiswahili kwenye mtihani utakoseshwa tu hata kama wewe ni Muislam haiwezekani upewe marks hapa kwa kuogopa utasema kuna Mfumo kristu, bsfuuu!!!!!

kiswahili kipo sawa we ndo upeo wako mdogo
 
pondas.jpg

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda

KWA mara ya kwanza tangu apelekwe katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amezungumzia hali ilivyo katika gereza hilo.

Akizungumza kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Sheikh Ponda ameonyesha kuridhishwa na huduma anazopata katika gereza hilo.


Profesa Lipumba alimkariri Sheikh Ponda, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kumtembelea gerezani kiongozi huyo wa Kiislamu. “Nimekwenda pale Segerea na kufuata taratibu zote za kutaka kumuona Sheikh Ponda, nashukuru walinielewa na kunikutanisha naye katika chumba maalumu na kufanya naye mazungumzo.

“Kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh Ponda, anapewa huduma zote na dawa zake zilizoachwa Hospitali ya Taifa Muhimbili zimepelekwa na anaendelea na matibabu vizuri, kidonda chake kinasafishwa vizuri na ana godoro lake la kulalia.

“Hata mimi nimeridhishwa na mazingira anayoishi gerezani, tuliweza kuelewana vizuri katika mazungumzo yetu.

“Amewasifia askari magereza kwa weledi wao wa kujali mtu tofauti na ilivyo kwa askari polisi ambao wamekuwa chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi.

“Kwa taarifa ambazo nimeelezwa, ni kwamba Sheikh Ponda hajapasuliwa mishipa ya bega alilopigwa risasi na imekuwa ni bahati nzuri kwani imeonekana risasi ilipenya kwenye nyama.

“Si kwamba Sheikh Ponda anafurahia maisha ya gerezani, bali yuko huko kwa sababu ametakiwa kuwapo, kwa hiyo, CUF na Waislamu wote, tunaomba aachiwe,” alisema Profesa Lipumba.

Katika mazungumzo yake, aliwataka Watanzania kuungana pamoja katika kupinga vitendo vya ukatili vinavyofanywa na askari polisi nchini.

Alisema kwamba, chama chake kimechoshwa na ukatili unaofanywa na askari hao na kwamba ukatili huo uweze kukomeshwa, lazima Watanzania washirikiane kuupinga.

“Leo polisi ndiyo wanaoshirikiana na majambazi kufanya uhalifu, polisi hao ndiyo wanaoshirikiana na wauza unga na polisi hao hao, ndiyo wanaosahau wajibu wao wa kulinda raia na mali zao.

“Polisi hao wamekuwa wakijihusisha na mambo yasiyo na maadili na kulifanya Jeshi la Polisi lionekane la kihuni kwa sababu wananchi wanakosa imani nalo. Kwa hiyo, tunataka tume huru ya uchunguzi wa tukio la Sheikh Ponda na tunataka askari aliyehusika afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Jambo jingine la muhimu kwa wanasiasa wenzangu ni kwamba tuungane ili kuonyesha ushirikiano pale mmoja wetu anapopata matatizo na pia isiwe kwa wanasiasa peke yao bali pia kwa Mtanzania yeyote,” alisema.

Wakati huo huo, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, zimemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuunda tume huru kuchunguza tukio la kupigwa risasi Sheikh Ponda.

Mbali na tume hiyo, pia wanawataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, wawajibike.

Katika mkutano wa dharura wa Waislamu uliofanyika jana katika Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam jana uliokuwa na lengo la kujadili hatua za kuchukua kuhusu suala la hilo, walisema wanataka tume isiyokuwa na polisi kwa kuwa wao ni watuhumiwa.

Sheikh Kondo Juma wa taasisi hiyo, alisema Kamanda Shilogile ni mtuhumiwa wa kwanza kwani ndiye aliyetoa amri ya Sheikh Ponda kupigwa risasi.

“Tunatoa muda, kama hawakuwajibishwa, basi tutaandaa maandamano ya Waislamu wote nchi nzima, kwa kuwa tunaamini Ponda si mchochezi, kama angekuwa mchochezi nchi isingetawalika.

“Dalili za Ponda kupigwa risasi zilianza tangu tukiwa hapa Dar es Salaam wakati wa Iddi mosi kwani baada ya Baraza la Iddi katika Msikiti wa Mchangani, polisi walisema tukienda Morogoro watu wote waongee kasoro Ponda, sisi tukasema tutakwenda na tutaongea.

“Tukiwa Morogoro, gari yetu ilivamiwa na polisi ambao walikusudia shari na hawakuwa na lengo la kumkamata tu, lengo lilikuwa ni kumuua, tukaachana na Ponda kama mita 100 hivi, baada ya muda ndio nikapata taarifa kuwa amepigwa risasi,” alisema Sheikh Kondo.

Naye Sheikh Ameir kutoka Zanzibar, alisema kuna taarifa serikalini zinasema kuwa, tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wa Uingereza chanzo chake ni Ponda, ambapo alisema matukio ya kumwagiwa tindikali visiwani humo yako tangu miaka saba iliyopita.

“Alimwagiwa tindikali Sheikh Soraga, si mzungu yule, lakini pia gazeti la Telegraph la Uingereza limesema, matukio ya kumwagiwa tidikali nchini humo, yamekithiri, sasa tutaamini vipi kama si wazungu wamefanya tukio lile?.

“Kwa muda ambao wasichana wale wanadaiwa kumwagiwa tidikali, asilimia 99 ya Wanzanzibar walikuwa wanafuturu, hivyo watu wasithubutu kuunganisha tukio hili na Uislam.

“Hata hivyo, tunasikitika kwamba, Sheikh Ponda hakutendewa haki kuchukuliwa akiwa hospitali anaumwa, lakini siku zote haki haiombwi kwa hiari, ikishindikana tutajiandaa kuidai,” alisema.

Kwa upande wake, Sheikh Hussein Ismail, alisema kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda ni kama wamepigwa Waislamu wote na akawataka kuchangia fedha za kuendesha kesi hiyo, fedha ambazo zilichangwa viwanjani hapo lakini hazikuhesabiwa.

Alisema watatumia utaratibu wa kufuata sheria na majukwaa hadi haki itakapotendeka kuhusiana na suala hilo. chanzo.
Ponda asimulia ya gerezani
 
Fasaha kwa standard ya nani?

Mimi ninasema Moja ni jela wingi majela (ma tunatumia sana kwa kitu kisichopendeza) hivyo majela yamejaa.Kule nilikotokea kanuni zetu za kimatumizi chochote kisichopendeza mara nyingi huanziwa na MA. mfano,mahabusu (asili yake habsi, hubisa), magereza, majitu (lafidhi nyingine mijitu), mahayawani...

Yani wewe watu wanajitahidi kukuelimisha bado unakua mbishi halafu ukifeli mitihani unaanza kumlaumu mama Ndalichako.
 
Hakuna kiswahili cha 'majela' .kama ulipita darasani basi rudi kasome tena.
Yap!
Ungesema basi kwa Kiswahili nilichofundishwa mimi darasani badala ya kukiita fasaha! afadhali ungetumia neno Kiswahili standard ningekuelewa.

Halafu unasema tena hakuna Kiswahili "majela" wakati waliokupangia wewe namna gani ya kupangilia Kiswahili ni wanaume kama sisi!
 
Waumini.jpg

Mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa kwenye mkutano katika viwanja vya Mwembeyanga,Temeke Jijini Dar es Salaam jana.


Sakata la kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, limepamba moto, baada ya mkutano wa Waislamu jana kuibua mapya.

Kati ya mapya yaliyoibuliwa katika mkutano huo ni pamoja na kupitisha maazimio matatu likiwamo la kuhamasishana kutokipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi utakaoitishwa wakati wowote kuanzia sasa.

Maazimio mengine yanawataka Waislamu kujiandaa kwa maandamano yatakayofanyika nchini kote kupinga dhuluma na kudai haki zao.

Pia kuitaka serikali iunde Tume huru ya uchunguzi wa tukio la kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda.

Maazimio hayo yalisomwa na Sheikh Kondo Juma Bungo, katika kongamano la waumini hao, lililoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za KiislamuTanzania, katika viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Akisoma maazimio hayo, Sheikh Kondo alisema tatizo la msingi dhidi ya Waislamu ni CCM.

Sheikh Kondo alisema juzi walishindwa kufanya maandamano kwa sababu hawakuwa wamejiandaa, hivyo anajiandaa kufanya maandamano nchini kote.

Hata hivyo, alisema Rais Jakaya Kikwete, bado ana nafasi ya kuundaTume huru kuchunguza tukio la
kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda na kwamba wakati hatua hiyo ikisubiriwa hatua nyingine zichukuliwe.

Alizitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kushtakiwa mahakamani kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, Mkuu wa Kikosi cha Polisi kilichoongoza operesheni katika tukio lililosababisha kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda na askari polisi anayetuhumiwa kumpiga risasi Sheikh huyo.

Hatua nyingine ni kujiuzulu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Awali, akiwasilisha mada kuhusu yaliyosababisha Sheikh Ponda kujeruhiwa, Sheikh Suleiman Daudi, alisema kwenye kongamano hilo kuwa ni kuzungumzia madai ya Waislamu ya muda mrefu.

Alisema baadhi ya madai hayo ni Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC) na kurejeshwa kwa Mahakamaya Kadhi.

Kwa mujibu wa Sheikh Suleiman, madai hayo yaliwahi kuwasilishwa na Waislamu kupitia halmashauri yao serikalini lakini hayakufanyiwa kazi.

Alisema wanashangazwa kuona baadhi ya makundi ya watu katika jamii, wakiwamo wanasiasa wakitoa kauli za uchochezi, kama vile nchi haitatawalika,lakini hawajawahi kufanyiwa kama alivyofanyiwa Sheikh Ponda.

Naye Sheikh Hussein Ismail, alisema Waislamu wanaviamini vyombo vya sheria nchini, hivyo akawataka Waislamu wachangie gharama za kuwezesha kusimamia kesi inayomkabili Sheikh Ponda mahakamani.

Kutokana na wito huo, Waislamu waliohudhuria kongamano hilo waliitikia na kuchangia fedha taslim katika viwanja hivyo.




CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom