Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hiyo si kweli kwamba kuna ubaguzi wa kikanda na kidini. Rais alipotangaza kuwa Mfalme wa Morroco amekubali kuwajengea waislamu Msikiti mkubwa sana Dar. Si waislamu walifurahi sana? Na wakristo walishangazwa sana na wakanyamza?
Na kama ingekuwa ni wakristo wanajengewa Kanisa KUBWA si kelele ingekuwa kibao?

Sasa basi ni lazima tujue TAKWIMU za DINI hizi mbili zilivyo nchini mwetu:
WAKRISTO ni 61.4%
WAISLAMU 35.2%
Kati ya hawa WAISLAMU 35.2% Wengi walienda Madrassa zaidi kuliko masomo ya elimu ya kawaida kabla ya serikali kuhimiza umuhimu wa elimu!

Wazazi wa watoto wa Kiislamu waliojua UMUHIMU wa ELIMU waliwapeleka watoto wao shule za dini ya Kikristo wakasomehuko nao hawakuwa wengi walikuwa ni WACHACHE.
Hivyo basi kati ya WAKRISTO 61.4% wengi waliosoma ni wale waliotoka mahali WAMISIONARY WALIKUBALIKA na kuanza kujenga shule.Hivyo wengi WAKABAHATIKA kusoma zaidi.

Na Sehemu zilizokuwa hazikufikiwa na wamisionari zilibaki nyuma kimasomo bila KUJALI DINI ama UKANDA. Hivyo wengi HAWAKUSOMA!
Hiyo ndio hali halisi iliyoleyeleza UWIANO kuwa hivyo MPAKA LEO!

SIDHANI kama rais Magufuli ANABAGUA.Ila anaangalia Qualifications na si UDINI! ama UKANDA.
Watanzania wote wanapewa haki sawa.
Kusema kanda ya ziwa inapendelewa si kweli Ukanda wa KUSINI una MAWAZIRI wengi zaidi. Hii ikiwa ni pamoja na WAZIRI wetu MKUU Kassimu Majaliwa ambaye ni MWISLAMU na mke wake Mary ambaye ni Mkristo.
Hizi kelele za Sheikh Khalifa HAZINA msingi wowote!
we ni miongoni , na nyie ndo mlokuwa mkimlalamikia jk alipokuwa anajitahidi kubalance! hoja ya kuwa waislam hawajasoma ni ya kijinga sana, pita collages na universities uone takwimu!
 
Kila kiongozi amechaguliwa kwa elimu yake na Si dini .

Mnaotaka kuanzisha ugomvi huu wa kidini hauta ka uishe.
 
Kwa hapa tanzania majina siyo kigezo cha dini yake. Wewe shehe naona huna hoja bali unafiki kwani umeambiwa tunakwenda kusalisha miskitini/makanisani???
 
Tukisema dini hamna katika Utawala au tusiweke dini basi pia tusiimbe wimbo wa Taifa. Maana tunamtanguliza Mungu kwanza.
WaTanzania ni Watu wanaabudu Mungu.
Na hii Amani tunayoizunguzia hapa Tanzania, chanzo chake ni dini.
Siasa tunaijua sana.
Hakuna mtu anamchukia Rais wetu wala ana nia mbaya nae. Tunampenda na tuko tayari kutetea hadhi yake popote pale duniani. Hatulipwi mshahara kwa hili. Ni viapo vyetu. Na sisi ndio tumepigia kura.
Suala udini, kweli kuna chembechembe hizo. Na ni vizuri sana kama Rais wetu atakuwa ni mdini. Tunataka kiongozi anayekuwa na maadili mazuri. Tusiogope hilo kabisa. Kiongozi Mcha Mungu ndio anayewajali wananchi wake. Ni dini ndio inayolainisha moyo.
Tusichoke kufundishana.
Kwa wale wale waliosomea "Uongozi" tunajua kabisa nini maana ya "Itifaki ya Uongozi".
Kiongozi huchagua watu ambao anawaamini, kwanza ni Usalama wake. Watu wanaomzunguka.
Watu watakaomtii kirahisi na watakaotekeleza kazi ili kushamirisha Utawala.
Kama Mheshimiwa Maghufuli kafanya kwa kuzingatia itifaki ya Uongozi na Utawala bora. Tunampa pongezi kubwa sana.
Kama Mheshimiwa Maghufuli amefanya kwa kutojua au kaponyoka na kanaswa kama binaadamu mwingine, kwenye "Udini Ubaguzi" basi sio vibaya kukumbushwa. Tunajua na yeye pia atapenda.
Waislam kama wanaona wamebaguliwa wana haki ya kusema. Ni mchango wao wa kutafuta haki zao kama wananchi wa Taifa hili.
La muhimu ni kuzingatia utamaduni wetu, kuambiana kwa upole, kutengeneza uhusiano na mawasiliano na Utawala wetu.
Tunatakiwa kujua katika dunia ya sasa sehemu nyingi duniani Waislam wananyanyasika, kuvamiwa na kukaliwa ardhi zao kwa nguvu, wengi wako mahabusi na hawana hatia pia. Leo hii kikichompa Ushindi Rais wa Marekani ni chuki za Kidini na kuwachukia watu weusi na wageni wahamiaji.
Ukisema "Taaluma na Uwezo wa Kungoza".. Wako akina Shabani na akina Mrisho na ni waatifu na wazalendo sana" pia wana uwezo mkubwa sana. Ikibidi balance ifanyike kuondoa shaka.
Utawala wetu usiwe na Ubishi, miaka 4 imebaki ya kupiga kura tena. Kura nyingi za CCM zimetoka kwa Waislam licha CUF kutumia udini. Diplomasia sio Taifa kwa Taifa, diplomasia pia iwe Serikali na watu wake.
Rais wetu, wengi tunakupenda kwa dhati, na tunakupenda kwa ucha Mungu wako. Na tunakukumbusha, usichoke kufuata nyao za Bwana Yesu. Yesu Mkombozi hakubagua watu.

Uhuru na Umoja wetu daima.

Jumatatu njema.

"Msema kweli ni MpenZi wa Mungu"
 
Kuteuliwa kazi serikalini sio bakwata wala tec. Hatuangalii elimu ya madrasa wala teolojia ya dini bali vigezo vingine. Wewe shehe wawapi.
 
ila jamaa amekuja na visible data.....minaona tungempinga kwa mtindo huohuo na simaneno matupu
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
mwenzio katoa data .....we unaishia kusema muongo bila ushahidi
 
Muhimu ni Rais kufanyia kazi haya malalamiko,taifa hili ni la watu wa dini zote
Mpangawangu,
Tatizo hili ni la muda mrefu sana.
Msome Mwalimu Nyerere anasema nini kuhusu tatizo hili:

''Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:

Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.[1]''

Hapo chini ni uchambuzi wangu ambao upo katika kitabu cha Abdul Sykes:

Hotuba hii ilikuwa ya ulaghai. Ukweli ni kuwa miongo mitatu baada ya uhuru Waislam hawajanufaika chochote wako katika hali ile ile aliyowaacha wakoloni au mbaya zaidi. Sivalon (1992) amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himaya yake ambayo inahodhi 75% ya viti katika Bunge la Tanzania. Kati ya viti hivyo 70% vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobaki vimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine.[1] Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingedhirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali.''
 
ilivyo nchini mwetu:
WAKRISTO ni 61.4%
WAISLAMU 35.2%
Kati ya hawa WAISLAMU 35.2% Wengi walienda Madrassa zaidi kuliko masomo ya elimu ya kawaida kabla ya serikali kuhimiza umuhimu wa elimu!
Hii sensa imefanyika lini?! "Wasomi" nyinyi utawasikia "huwa tunapitisha sensa makanisani!" Kama nawe hili ndo jibu lako; basi naomba unisaidie yafuatayo!

Nchi hii ina makundi makubwa yafuatayo:
  • Wakristo
  • Waislamu
  • Wapagani
Now let's assume baada ya kupitishwa sensa makanisani; mkapata kwamba mpo 61.4% na iliyobaki ni 38.6%. How did you know out of 38.6%; miongoni mwao 35.2% ni Waislamu?! Au Wapagani nao huwa wanafanya sensa ambayo baada ya kufanya subtraction ya %age ya Wakristo na Wapagani, hapo mkafahamu waliobaki ni Waislamu!!!

Halafu acha ujinga wa wenzako wengine... kama mmekaririshwa makanisani hizo nyimbo za madrasa zinawafanya muonekane totally dumb manake mnaoongea msichokijua! Kama una marafiki Waislamu anzia hapo hapo kuangalia among your fellow Muslims ni wangapi wanaifahamu Quran!! Ni wangapi walikuwa wanasoma madrasa wakati wapo sekondari! Na kama unaishia kwenye mji wenye Waislamu; tembelea madrasa yoyote kama hujakuta wamejazana watoto ambao nao huwa wanaacha madrasa kadri siku zinavyoenda...!! Majority ya Waislamu hata hiyo Quran yenyewe hawaijui... hata juzu moja hawajamaliza lakini utafikiri mmegeuka kasuku na hoja ya madrasa!! Hoja yenu ya madrasa ni hoja ya kijinga kama sio ya kipvmbavu manake mnaongea kitu msichokijua!
 
hata mimi sikubaliani na suala kuwa utawala wa JPM unawapendelea wakiristo sababu kuna maswala matatu mazuri rais aliwafanyia waislamu, ambaye wakiristu haja wafanyia:
1) kwanza kashiriki Baraza la IID, na kuwaahidi mali zote za waislam zilizo porwa, watarejeshewa.
2 )waislam waliahidiwa kuwa BAKWATA, wajengewe OFISI mpya.
3) rais aliwaobea kwa Mfalme wa Morocco awajegee MSIKITI MKUUUBWA..
sasa wakiristu hakuna hata jambo moja walio fanyiwa
sasa huo msikiti wataingia waislam wote
 
Angefanya ulinganisho na Awamu iliyopita ningemuelewa.

Kwamba awamu iliyopita ambayo Rais alikuwa muislam teuzi zilikuwa hivi na hivi sasa ni hivi.

Pamoja na hayo pale hawaendi kuhubiri dini wanaenda kuwatumikia watanzania wote yoyote anafiti kama anakizi vigezo.

Waanze na kukataa kujengewa mjengo na serikali kwanza.
Toka tupate uhuru haijawahi kutokea waislamu kuwazidi wakristo kwenye teuzi serekalini.
Ndi wakristo kwa zaidi ya 70% wanatumikia kanisa
 
Kuteuliwa kazi serikalini sio bakwata wala tec. Hatuangalii elimu ya madrasa wala teolojia ya dini bali vigezo vingine. Wewe shehe wawapi. i
argument kuwa waislam hawajasoma ni argument ya kipumbavu kuwahi kutokea! anyway endeleeni ni dhulma jehanam inawasubiria, thus y kuna siku ya hukumu
 
Mtoa mada ukimaliza hili utaanza kuleta hoja zingine za kibaguzi kwa maslahi ya nani. Hii inchi ni yetu wote kwa nini mnaleta hoja za kipuuzi mala udini, mala ukanda, mala mtakuja na mambo mengine. Hivi tutafika kweli kwa ujinga kama huu. Hivi mtu asipewe nafasi kama anafaa kisa dini yake na kabila yake. Acheni hizo ni akili za kipumbavu hizo.
Kwa hiyo wanaofaa ni wakristo tuu?
 
Kwani wameteuliwa ili wakafaye ibada au watumikie taifa? Msipende kuongea vitu kwa hisia Bali angalieni tija hakuna dini kwenye selikari ya Tanzania
 
Facts zipi unaongelea? Kwani kigezo cha uteuzi ni dini ya mtu? Tafuteni elimu kabla ya kuanza kupayuka ovyo ovyo.
Mngekuwa na elimu hiyo mnayodai tungeona maendeleo kwa jinsi mlivyojazana serekalini.
Inaelekea huko shule mnaenda kusomea ufisadi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom