Maguge Maguge
JF-Expert Member
- Sep 1, 2016
- 2,734
- 1,781
Hizi ndizo post zinazotakiwa kufutwa, ila mods labda hawaoni kama zinagawa watu.
Hivi wewe mzee haunaga stori nyingine zaidi ya hizi ,kila siku waislamu na uhuru .....Waliofanya mapinduzi Zanzibar ni kina nani ? Mbona haijawahi kutokea Rais wa Zanzibar Mkristo ?Philipo,
Suala hili linataka mtu awe na ujuzi wa kutosha kuhusu historia ya Waislam
kwanza kuasisi TANU na mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Inabidi ujiulize kipi kiliwafanya Waislam waongoze mapambano yale na nini
yalikuwa mategemeo yao uhuru ukipatikana?
Ukimaliza hapo uingie kutaka kujua nini ilikuwa ahadi ya Mwalimu Nyerere
kuondoa ubaguzi kwa wale ambao ukoloni uliwaathiri sana mara tu uhuru
ukishapatikana.
Ukishajua ahadi ya Mwalimu Nyerere sasa ujiulize je, ahadi hiyo ilitimizwa?
Ukifika hapa utakuwa katika hali nzuri ya kufanya mjadala wa maana katika
mada hii.
Kumbuka Jk alipoteua tume ya kuratibu mabadiliko ya katiba,mzee Mtey mwanzilishi wa alivyolalamikia idadi ya waislamuRais akiwa mkristo akiteua bhasi ameangalia vigezo
Rais akiwa Muislam akiteua/anapendelea Waislam wenzake
WaTz Mungu anatuona, si kwa unafiki huu
Ukienda zanzibar ambako waislamu ni wengi kuliko wakristo, ukifuatilia utakosa hoja, maana utakuta zaidi ya 70 ya viongozi ni waislamuasante sana mkuu kwa hekima hii ya uchambuzi lakini swali pamoja na kuangalia vigezo hivyo yaani ndio mzani wa asilimia uegemee upande mmoja tu katika kila maeneo ya uteuzi hakuna hata sehemu umebalance au hata kuzidi upande mwingine?
sasa bila posho na marupurupu,samaki samaki unadhani atainngiaje?,sheikh kagonga penyewe kabisa! ingekuwa ni enzi za jk kwa udini huu nchi isingetawalika, maana wakristo wanavyopenda vyeo vya kidunia sijapata kuona!
Swala siyo Udini, Swala ni shule. Fanya sampling ndogo tu Angalia sasa hivi hata kwenye majina ya wahitimu wa shule za msingi na sekondari. Chunguza hayo majina mengi ni ya Dini gani? Halafu rudi kwenye takwimu, wakristo na waislam wapi ni wengi? Watu wamekaa kuchunguza udini Bila hoja za Msingi.
Waziri mkuu si muislam unachofanya ni kupotosha jamii isipokuwa anajina la kislam.[emoji814] Daah...HUWA NAJIULIZA HILI:
■ Awamu iliyopita,
[emoji666]RAIS= Muislam.
[emoji666]MAKAMU WA RAIS= Muislam
[emoji666]RAIS WA ZANZIBAR = Muislam
■ Awamu hii
[emoji666]RAIS= Mkristo
[emoji666]MAKAMU WA RAIS = Muislam
[emoji666]WAZIRI MKUU= Muislam
[emoji666] JAJI MKUU= Muislam
[emoji666] RAIS WA ZANZIBAR= Muislam
Sijui kama ingekuwa ni wakristo wameshikilia nafasi hizo ingekuaje kama sasahv lawama haziishi.
- Hata kwenye all 3 National pillars wangekuwa waislam wote bado kuna watu wangelaumu tu.
Mbona kaongea kwa facts? Nafikiri anayepinga naye alete data hapa..
kwa hiyo bara wakristo ni wengi kuliko waislam?Ukienda zanzibar ambako waislamu ni wengi kuliko wakristo, ukifuatilia utakosa hoja, maana utakuta zaidi ya 70 ya viongozi ni waislamu
Mtoa mada ukimaliza hili utaanza kuleta hoja zingine za kibaguzi kwa maslahi ya nani. Hii inchi ni yetu wote kwa nini mnaleta hoja za kipuuzi mala udini, mala ukanda, mala mtakuja na mambo mengine. Hivi tutafika kweli kwa ujinga kama huu. Hivi mtu asipewe nafasi kama anafaa kisa dini yake na kabila yake. Acheni hizo ni akili za hizo.Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.
Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.
Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.
Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.
Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.
Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.
Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.
Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?
Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.
Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.
Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.
Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.