Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Rais asiteue mtu kwa kuangalia dini,kabila,kanda au rangi yake. Akianza kuchagua kwa kuangalia huo ndio UBAGUZI WENYEWE.
 
Dau pekee ndo mwenye akili ktk waislamu wote Tanzania,maana aliweza kuiba na kujenga taswira ya lidini Nssf,big up dau
acha udini mkuu,halafu bora uwe mdini lakini una roho ya kibinadamu,wewe inaonekana unachukia sana waislamu ,
lakini ujue hatuwezi wote tukawa walokole,japo wote ni binadamu,
hivi inakuwaje watafuna kiti moto mnakuwa na roho za korosho kiasi hicho?,

wewe unaona mgawanyo wa madaraka uko sawa kweli hii awamu,au unatetea kwa kuwa ni wa imani yako,unafaidika nini labda kwa mfano?
 
Sidhani kama Rais huteua watu kwa kuhoji dini zao. Pia kuna ukweli kuwa taasisi za elimu za Kikristo zimekuwa zikijitahidi sana kuendeleza watoto kielimu tofauti na taasisi nyingi za Kiislamu ambazo zimekuwa zikihimiza zaidi elimu ya Madrassa na lugha ya Kiarabu.
ni kweli rais hateui kwa kuzingatia dini kama vile taasisi za kiislam zisivyo sisitiza elimu ya madrasa na lugha ya kiarabu bali husisitiza elimu yote kwa ujumla na masomo ya maarifa ya uislam kama lilivyo somo la bible knowledge au divinity pamoja la lugha ya kiarabu kama yalivyo masomo ya lugha za kiingereza kifaransa nk. Madrasa ni kujifunza quran na mafundisho mengine ya dini baada ya kutoka shuleni kama yalivyo mafundisho kwa wakristo.
 
Kujifanya nchi hii haina udini ni unafiki. Tulipofikia kiongozi lazima abalance ktk teuzi zake la sivyo abebe lawama za upande mmoja lkn kutetea kwamba anachagua wachapakazi tu bila kuangalia dini sio kweli. Tunaishi na watu, wengine tumesoma nao na kufanya kazi nao uwezo wao ni mdogo ingawa ni wakristo. Hivyo sio kweli kwamba waislamu ni wachache wachapakazi na wasomi.
Mnasoma elimu ya kueneza dini tu, kama kuweka posti hii ya kidini na kuitetea mwenyewe kwa ID 7 tofauti, ili uonekane una watu wanaokusapoti
Huwezi kusoma madrasa udai we msomi!
 
acha udini mkuu,halafu bora uwe mdini lakini una roho ya kibinadamu,wewe inaonekana unachukia sana waislamu ,
lakini ujue hatuwezi wote tukawa walokole,japo wote ni binadamu,
hivi inakuwaje watafuna kiti moto mnakuwa na roho za korosho kiasi hicho?,

wewe unaona mgawanyo wa madaraka uko sawa kweli hii awamu,au unatetea kwa kuwa ni wa imani yako,unafaidika nini labda kwa mfano?
Inatakiwa Masharti ya kuwa kiongozi kuanzia sasa, wakati unaapa ule kitimoto
 
Haya mambo ya UDINI naJINSI yananipa taabu sana mimi. Mfano wabunge wa viti maalumu wa kazi gani katika nchi yetu?
 
Huyu shekhe anahitaji kupewa ushauri nasaha kwa upole. Lakini, niseme tu kwamba, manung'uniko yake ni kama ya kina Hellen Kijo Bisimba kuhusu ubaguzi wa kijinsia katika teuzi za JPM. Kina Hellen wanataka nafasi za uteuzi zigawiwe pasu kwa pasu kati ya wanawake na wanaume. Sasa shekhe anataka nafasi zigawiwe kwa kuzingatia uwiano fulani kati ya makundi mbalimbali ya kidini na kikanda. Naona auanongelea Ukristo dhidi ya Uislam, Umashariki dhidi ya Umagharibi. Amesahau kuongelea ujana dhidi ya uzee, Ukulima dhidi ya Ufanyabiashara, Usomi dhidi ya Kutosoma, na migawanyiko kama hiyo.

Yeye pamoja na kina Bisimba ni watu wa kuelimishwa hivi: Vyeo havigawiwi kwa kuangalia vigezo vinavyohusiana na migawanyiko ambayo haina tija katika ofisi. Kwa mfano, mwalimu wa hesanu anaweza kuwa mwanamke au mwanamume, mkristo au muislamu, mmashariki au mmagharibu, kijana au mzee. Lakini hawezi kuwa mkulima wala mfanya biashara kama ambavyo hawezi kuwa asiye na kisomo. Vigezo vya ujuzi, ustadi, uzoefu na utayari vinahusika. Hivi hoja hii ni ngumu?

Kuna performance indicators in good governance wanatuletea hawa development partners kama vile gender equity, denominational equity, geographical equity, inter generational equity, n.k. Haya mambo tuyakatae kwa hoja kwa kuwa hayana tija. Tukikubali kila kitu tutakuwa kama madodoki.
Nashindwa nikupongezaje kwa fact ulizoshusha apa, mwenye macho na uelewa kamili ataelewa. [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Kwa hili sawa tu.asiwaingize waislam wenzetu.kwenye utawala wa dhuluma.tena ikiwezekana awafute kazi na hao waislam wore.
 
Unaweza ukawa na akili na nguvu nyingi lakini ukinyimwa HEKIMA na BUSARA, basi wewe huna maana tena, subiri kuja kuskfiwa kwenye MSIBA wako kama tunavyoona, kitu ambacho hakitakusaidia huko unakokwenda.

Watu wajifunze kuwa WAADIKIFU hasa katika wiki hii inayomalizika leo tarehe 13/11/2016, misiba iliyotokea kwa viongozi ambao kila mtanzania ameishuhudia nabkuona UNAFIKI wa hawa viongozi.

Tu-refer pesa zilizochangwa na watu mbalimbali kwa ajili ya watu/watanzania waliofikwa na tetemeko la ardhi kule KAGERA eti tunaambiwa hela zinaenda kufanya ukarabati wa miundombinu ya Serikali!? Kweli?!

Mungu na awahukumu wale wenye kufanya jeuri juu ya malmaka ili adhabu isijekutupata na tusiohusika ikaonekana hatujachangia japo kwa maandishi.
 
KUWA MUADILIFU, USIONGEE HIVYO KWAKUA KASEMWA WA DINI YAKO, WAKATI MWAKA JANA JK KILA AKITEUA ULIKUA UNALETA MAMBO HAYA HAYA ANAYOYASEMA SHAIKH KHALIFA, JE HAKUSEMWA JK KWA UDINI HUMU?, HAMKUTOA MATAMKO CHUNGU TELE HUMU?, HIVI UTAACHA LINI KUWA KIPOFU UPANDE MMOJA NA JARIBU KUWA MUADILIFU, WAISLAM WALISAKAMWA SANA HAPA KIPINDI CHA JK, SIUNGANI NA SHAIKH KATIKA HILI JAPO LIPO, BUSARA NI KUNYAMAZA TUONI KAMA UADILIFU UNA DINI, UNAWEZA UKAWA MKATOLIKI, UKAFUKUZA WARUTHELI WOTE SERIKALINI NA BADO USIFANYE CHOCHOTE SERIKALINI ZAIDI YA KULETA MAUZA UZA TU, KIKUBWA NINACHOKIAMINI NI KUMUACHA AFANYE ANAVYOTAKA, ILI TUONE UTOFAUTI WA MDINI WA KIKRISTO NA MDINI WA KIISLAM NANI ALIFANYA UADILIFU KWA WENZIWE..........COUNT !!!! 1. MISAADA YA WAHANGA,
ALLAH KAREEM, ANAONA.
 
viongozi wa waislamu wamepambazwa kwa kujengewa makao makuu ya bakwata kwa hiyo wengi wao hawaoni wala kusikia ubaguzi huu kwenye uteuzi wa watendaji. Ukweli ni kwamba waislamu wengi kwa sasa wamesoma tena wasomi waadilifu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom