Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Uvuvi wa kufikiri ni tatizo sana hivi huo udini huwa unakuja pale tu wanapowekwa wakrsto?mbona kipindi kile wamejazana wao walikuwa hawasemi? Kutoka moyoni I hate this behaviour.
Wamekaa tu hawafanyi kazi kazi majungu tu.
 
Mkuu ni sawa ila to be honest, wakristo hawakuwahi kulalamikua seriously hilo na kama walilalamika sio suala lililochukua hata mwezi mmoja.

Ila ndugu zetu waislam walishamlaumu kuwa amekuwa agent wa wakristo na hawajali waislam wenzie na kipindi hicho Lowassa ndio alikuwa very close na waislam

Leave alone hizo issues, imekuwa ni kawaida ndg zetu waislam kucomplain kwenye kiiila kitu kuwa wanaonewa.

Research yourself utagundua.
Labda kama hukuwa mfuatiliaji wa masuala haya. Baraza la maaskofu Tanzania ilikuwa haipiti wiki wa nakuja na matamko.Mkuu masheikh ni wastaarabu sana katika nchi hii toka utawala ulopita mpaka leo hutosikia baraza la waislam limeigiza serikali kufanya hivi wala vile.Lakini maaskofu nchi hii utadhani wana ubia na serikali ( labda upo) asiguswe askofu, serikali isifanye Kitu lazima waongee.katukanwa pengo au nani lazima serikali ihangaike. Tuna mashekhe kutoka Zanzibar wamefungwa mpaka leo hii wapo ndani hakuna kesi kinachoendelea hakijulikani.kwanini tusiseme waislam tunakandamizwa.?
Tafakari Mkuu
 
Uvuvi wa kufikiri ni tatizo sana hivi huo udini huwa unakuja pale tu wanapowekwa wakrsto?mbona kipindi kile wamejazana wao walikuwa hawasemi? Kutoka moyoni I hate this behaviour.
Wamekaa tu hawafanyi kazi kazi majungu tu.
,we huoni hata hiyo takwimu inaonyesha,sio unakulupuka tu soma kwanza uelewe kisha changia,
 
wenzenu wanajenga shule nyinyi mnajenga madrasa na kufundishana ngumi km vile tuko somalia! pia tambueni kuwahao wakristo wazungu ndio walizitawala nchi za kiarabu na uislamu kwa ujumla hivyo wakristo kutawala wameanza enzi na enzi na hakutakuja kuwa na usawa hapa duniani.
Dah.. mambo ya zamani sana unaleta

Ondoa ujuha kichwani mwako, hakuna sekta hapa Tz utamkosa muislam, kama kigezo ni elimu
 
Hiv ww unadhan mtoto kakua anajua mambo ya madrasa na quran atakuw na uwezo gn wa kufanya vyema drsan ilihali wazaz wak wamemwekea kaswida na quran ndo kipaumbele chake? Waislam wako nyuma kielim kubali ukatae jibu ni hlo,kikwete arijaribu kuwabebabeba lakin hawabebeki wanapwaya coz hamn kitu kichwan zero,fanya reseach kwanza ndo utokwe na hiyo mipovu yko mkuu
Na hiyo ndo kete mlobaki nayo kuwa waislam hawajasoma.lakini Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki.Ipo siku tutaheshimiana tu.
 
Kama hixi takwimu ni kweli basi kunahitajika " Affirmative Action"
 
Huyu shekhe anahitaji kupewa ushauri nasaha kwa upole. Lakini, niseme tu kwamba, manung'uniko yake ni kama ya kina Hellen Kijo Bisimba kuhusu ubaguzi wa kijinsia katika teuzi za JPM. Kina Hellen wanataka nafasi za uteuzi zigawiwe pasu kwa pasu kati ya wanawake na wanaume. Sasa shekhe anataka nafasi zigawiwe kwa kuzingatia uwiano fulani kati ya makundi mbalimbali ya kidini na kikanda. Naona auanongelea Ukristo dhidi ya Uislam, Umashariki dhidi ya Umagharibi. Amesahau kuongelea ujana dhidi ya uzee, Ukulima dhidi ya Ufanyabiashara, Usomi dhidi ya Kutosoma, na migawanyiko kama hiyo.

Yeye pamoja na kina Bisimba ni watu wa kuelimishwa hivi: Vyeo havigawiwi kwa kuangalia vigezo vinavyohusiana na migawanyiko ambayo haina tija katika ofisi. Kwa mfano, mwalimu wa hesanu anaweza kuwa mwanamke au mwanamume, mkristo au muislamu, mmashariki au mmagharibu, kijana au mzee. Lakini hawezi kuwa mkulima wala mfanya biashara kama ambavyo hawezi kuwa asiye na kisomo. Vigezo vya ujuzi, ustadi, uzoefu na utayari vinahusika. Hivi hoja hii ni ngumu?

Kuna performance indicators in good governance wanatuletea hawa development partners kama vile gender equity, denominational equity, geographical equity, inter generational equity, n.k. Haya mambo tuyakatae kwa hoja kwa kuwa hayana tija. Tukikubali kila kitu tutakuwa kama madodoki.
Umenena kwa hoja mkuu,that's true
 
Kwa bahati mbaya/nzuri uchaguzi mkuu hufanyika siku ya Juma pili. Wakristo wengi walikuwa wanapinga hii siku kutumika hivyo. Walienda mbali hadi kutengeneza Tsheti zenye kauli mbiu ya kukataa uchaguzi kufanyika Juma pili. Wengine hoja yao kwanini isiwe Ijumaa, then huu ni uonevu kwao. Hivi Kuna ubinafsi mkubwa kuliko huo? Kuna ulalamishi mkubwa kuliko huo? Siku moja ndani ya miaka mitano wakati Ijumaa zote ndani ya miaka mitano waisilamu wanakuwa kazini, hivi hapo ni kina nani wanalalamika bila hoja za msingi?

Wakristo wanaongoza kutoa mahubiri kwenye maeneo ya umma na waisilam wala hawaangaiki nao,Lakin wakisikia tu Adhana tena msikitini hao wanalalamika. Sasa najiuliza hivi hapa nani wavumilivu? Siku hizi kwenye mabasi,daladala, vituo vya daladala (kama ubungo) nk wao wa natoa mahubiri na waisilam wala hawalalamiki. Hadi kwenye mwendo kasi wapo na mahubiri wanatoa ila hakuna mwisilam anayewakataza. Lakini ikitokea akaoa mawaidha muisilam kweye gari itakuwa balaa.

Taasisi za umma wakristo wanaongoza kuendesha vitu kidini dini tu. Utakuta Kuna kikao watu ngoja tuombe na wa naomba kwa imani yao kana kwamba wote pale ni dini ile. Ukifika maofisini utakuta kwaya zinapigwa humo. Viongozi wakitoa mifano nk hutumia biblia kana kwamba kila mtu aniamini na kuifuata. Haya yote wala waisilamu hawashulishwi nayo. Ila ikitokea tu mkristo kapanda hata daladala a kakuta dereva kaka mawaidha basi atalalamika sana. Hivi hapo nani walalamishi?

Huduma saa za ibada. Mkristo akienda hata dukani tu akakuta jamaa kafunga kaenda msikitini kuswali ila anarudi ataanza kulalamika. Lakini anasahau kuwa Jumapili yeye kutwa kafunga na watu wanakosa huduma. Cha ajabu ni kuwa yule anayesubiri muisilam atoke msikitini aje aampe huduma analalamika wakati yule ambaye hapati huduma ile kwa siku nzima ya Jumapili amenyamaza. Hivi hapo anayependa kulalamika nani?
 
nimeenda page kwa page,post kwa post kutafuta comment yoyote ya Faiza Foxy,mpaka sasa sijaona hata moja.

hapana si kawaida....kuna kitu hakiko sawa.
 
Watu wakitoa madai yao msiwabeze wajibuni kwa weledi wataelewa kuliko kudhihaki......hii mambo noma sana.

Political violance feels your city yeah.....dont involve rasta in your say say......
 
Kwa kweli mbali ya kua muislam, kuna haja ya waislam kuwasomesha watoto wao madrasa na pia shuleni wakasome elimu ya kawaida. La sivyo tutaishia kulalama na kuibua hoja zczo na mantiki. Unakuta watto wanaenda kusoma Qur'an kila siku badili ya kutenga mda wao pia kusoma elimu dunia. Sasa ukimuliza huyo sheikh mtto wake kasoma mpk wapi atakwambia kahifadhi juzuu.

zuu
Ww muislam wmenye kujitambua na unatambua dunia unavyoenda,bora ulivowachana live
 
Teuzi za mhisimiwa zina ukakasi! Mtaani kuna minong'ono kuwa zina chembe ya udini!
 
hata mimi sikubaliani na suala kuwa utawala wa JPM unawapendelea wakiristo sababu kuna maswala matatu mazuri rais aliwafanyia waislamu, ambaye wakiristu haja wafanyia:
1) kwanza kashiriki Baraza la IID, na kuwaahidi mali zote za waislam zilizo porwa, watarejeshewa.
2 )waislam waliahidiwa kuwa BAKWATA, wajengewe OFISI mpya.
3) rais aliwaobea kwa Mfalme wa Morocco awajegee MSIKITI MKUUUBWA..
sasa wakiristu hakuna hata jambo moja walio fanyiwa
Dah.. Kazi ya ualimu ni ngumu sana

Yaani mada ni nyadhifa Serikalini wewe unazungumzia misaada na sherehe..!?
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.

Hiyo si kweli kwamba kuna ubaguzi wa kikanda na kidini. Rais alipotangaza kuwa Mfalme wa Morroco amekubali kuwajengea waislamu Msikiti mkubwa sana Dar. Si waislamu walifurahi sana? Na wakristo walishangazwa sana na wakanyamza?
Na kama ingekuwa ni wakristo wanajengewa Kanisa KUBWA si kelele ingekuwa kibao?

Sasa basi ni lazima tujue TAKWIMU za DINI hizi mbili zilivyo nchini mwetu:
WAKRISTO ni 61.4%
WAISLAMU 35.2%
Kati ya hawa WAISLAMU 35.2% Wengi walienda Madrassa zaidi kuliko masomo ya elimu ya kawaida kabla ya serikali kuhimiza umuhimu wa elimu!

Wazazi wa watoto wa Kiislamu waliojua UMUHIMU wa ELIMU waliwapeleka watoto wao shule za dini ya Kikristo wakasomehuko nao hawakuwa wengi walikuwa ni WACHACHE.
Hivyo basi kati ya WAKRISTO 61.4% wengi waliosoma ni wale waliotoka mahali WAMISIONARY WALIKUBALIKA na kuanza kujenga shule.Hivyo wengi WAKABAHATIKA kusoma zaidi.

Na Sehemu zilizokuwa hazikufikiwa na wamisionari zilibaki nyuma kimasomo bila KUJALI DINI ama UKANDA. Hivyo wengi HAWAKUSOMA!
Hiyo ndio hali halisi iliyoleyeleza UWIANO kuwa hivyo MPAKA LEO!

SIDHANI kama rais Magufuli ANABAGUA.Ila anaangalia Qualifications na si UDINI! ama UKANDA.
Watanzania wote wanapewa haki sawa.
Kusema kanda ya ziwa inapendelewa si kweli Ukanda wa KUSINI una MAWAZIRI wengi zaidi. Hii ikiwa ni pamoja na WAZIRI wetu MKUU Kassimu Majaliwa ambaye ni MWISLAMU na mke wake Mary ambaye ni Mkristo.
Hizi kelele za Sheikh Khalifa HAZINA msingi wowote!
 
Aiseee yaani Mimi nikiona mtu akiona kitu mawazo yanamjia ya ukabila, ukanda na udini. Kwa mtazamo wng mtu wa aina hii atakuwa na akili fupi sana, tena ambazo zipo tumboni.
 
Dr Dau mkamchafua sana kwasababu tu za dini yake. Lakini Kuna taasisi nyingi na mashirika mengi tu ambayo utendaji kazi wake ni wa kwango cha chini sana lakini hayo hayakuonekana. Baadaye zikaletwa takwimu ambazo bado zilionesha kuwa sio tu kuwa idadi ya wakristo ilikuwa kubwa kuliko waisilam bali hata kwenye ngazi za juu Hali ilikuwa vivyo hivyo. Hata hivyo hamkuridhika mkawa bado mnalalamika na sijui kama mmeacha.

Mwisho:
Ndugu zangu wakristo waisilam wanaongoza kwa uvumilivu hapa tz. Ninyi mnangoza sio tu kwa kulalamika bali pia kujikweza. Yani akipewa nafasi mkristo ni kwasababu anaelimu hivyo anaweza,akipewa muisilam nafasi kapendelewa. Naomba mbadilike. Nadhani mlifika mahali mkadhani mnahati miliki ya hii nchi na ndio maana hata taasisi iwe na wakristo 99 akiwepo muisilam mmoja bado mnaona Kuna udini. Kwa ndugu zangu katika imani, vyeo ni dhamana. Na kwa hakika tutakujwa ulizwa juu ya dhamana hizo. Tuwaelimishe ndugu zetu hawa maana wengine ni ndugu wa damu kabisa na tujitahidi kupunguza hasira na jazba ili tuwaelimshe hawa ndugu zetu taratibu.Allah awaongoze vyema ndugu za katika imani na awape uwezo wa kuitambua haki ndugu zangu wakristo kabla hayajawafika mauti. Amin.
 
The book,
Siwezi nikaeleza yote hapa uwanja mdogo.

Lakini påta kitabu cha Abdul Sykes kila kitu kimo mle.
Mohammed Said, naomba kukujuza tu kuwa nimeshasoma vitabu vyako kadhaa tokea january ya mwaka 2014 nilipokuomba unielekeze ntavipata wapi.

Umejitahidi sana kuelezea matukio hasa yaliyotokea miaka michache kabla ya uhuru, wakati wa uhuru na baada ya hapo.

Pia nakiri kuwa upo exposed kwa sehemu kubwa na dunia hii.

Pia uliwataja wahusika walioisaidia Tanganyika kupata uhuru wake na wale wa kipindi cha muungano ambao majority of us tusingewafahamu.

LAKINI pia kuna namna flani umeonesha kuwa Waislam waliplay role kubwa sana kuliko wakristo halafu hawakuthaminiwa.

Umeonesha kuwa Nyerere hakuwathamini waislam pindi tu baada ya uhuru.

SASA, Kila nikijaribu kujiuliza kuwa J.K Nyerere alipaswa kufanya nini kwa waislam kwa wakati ule nashindwa kujua.

SWALI: Hebu naomba leo katika uzi huu uweke wazi kuwa Je Nyerere alipaswa kufanya nini kwa waasisi wa TANU na viongozi wa Waislam wa kipindi kile?

Karibu Mzee.
 
Kule kwetu kuna msemo unasema "Bora nguo zichakae utapeleka kwa fundi zipigwe kiraka, sio akili".
Watanzania wengi tumefika mbali sana, mawazo ya waliowengi yamejikita kwenye vitu visivyo na misingi yeyote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom