Sharti gani gumu uliwahi pewa na mwenye nyumba kwenye nyumba za kupanga?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Sijakosea. Nafahamu fika kuwa members wote wa JamiiForums tuna majengo makubwa sana hasa maeneo ya Sinza na Oestabey, lakini yote kwa yote, wengi wetu tumewahi panga vyumba kabla ya kujenga

Ni sharti lipi gumu uliwahi pewa na mwenye nyumba ndani ya nyumba yake ulipopanga kwake?
GB9AMnLWsAIgs98.jpeg
 
Nakumbuka Xmas nilitembelewa na ndugu, tukapika zetu, tukala fresh, baadae tukasema tukae nje watu wa enjoy. Aisee alipotokea mwenye nyumba sikujua, matusi na maneno makali sio poa. Nikamwambia kama hukutaka niwe na wageni ungeandika kwenye sehemu ya masharti ya mkataba. I didn't renew my contract nikahama.
 
Sijakosea. Nafahamu fika kuwa members wote wa JamiiForums tuna majengo makubwa sana hasa maeneo ya Sinza na Oestabey, lakini yote kwa yote, wengi wetu tumewahi panga vyumba kabla ya kujenga

Ni sharti lipi gumu uliwahi pewa na mwenye nyumba ndani ya nyumba yake ulipopanga kwake?
View attachment 2850245
Eti nisilete mademu gheto...Anyway mpaka sasa sijajenga nimepanga kwenye nyumba ya mstaafu flani hivi ajuza huyu ana kamtindo ka kuamka alfajiri (utadhani anaendaga kazini) anaamka na kuanza kuzunguka uwanja wa nyumba akifoka foka bila sababu za msingi ilimradi muamke
 
Kuna mbibi mtu wa Iringa yule mama alikua ana gubu sio la kawaida. Kiguu na njia kuja dar kila leo japo wamestaafu na mume wake wake wanakaa Iringa. Kuna mwembe upo ndani ya uzio wa nyumba ule mwembe ni tasa ila unapupukutisha majani. Anataka kila yakidondoka pafagiliwe muda huohuo hata kama asubuhi palifagiliwa. Akiambiwa aukate au ku prune hataki.
 
Inakuwaje mwenye nyumba anakuzoea kiasi cha kukuleta dharau na kero?.

Niliwahi kupanga mitaa ya makumbusho wenyenyumba walikuwa ni jamaa mmoja na dada zake nyumba ya urithi.

Yule jamaa alitaka kuleta mazoea sikutaka hata kumlea nkamwambia wazi pigo zake sizielewi. Akaenda waambia dada zake huyo mchuga sio.

Mpaka naondoka pale hawakuwahi niletea mazoea au kero za kiswazi, nilikua naona malalamiko ya wapangaji wengine tu.

Vile unajiweka inachangia sana dharau na kero. Nikupe hale yangu alafu ulete dharau hautaamini nitavyokuvuruga.

Kila mtu afanye wajibu wake tu.
 
Back
Top Bottom