Shangwe laibuka mazishi ya bibi mwenye miaka 132 Moshi

Shangwe laibuka mazishi ya bibi mwenye miaka 132 Moshi

Mpaka sasa sijaona mtu akihakikisha kwa kumbukumbu za kanisa.

Hakuna mtu akiyehakikisha kwa watoto.

Hakuna aliyehakiki kwa natukio aliyoyaona muhusika ambayo nayo yana shida ya uhakiki.

Hakuna hata mtu aliyesema mtoto wake wa kwanza alizaliwa mwaka huu, na tunahakiki hivi kwamba ni mtoto wake wa kwanza.
Nafikiri ni kwa ajili hakuna aliyetakiwa atoe uhakiki. Kama ingetakiwa nahisi wahusika wangetoa
 
Machen bb apumzike kwa aman acheni kujadili ujinga usiowasaidia fan kurudi manyoya...we hata 70 kufika kizungu mkutii unashindana na mwamba aliena uhakika wa 100 kafika acha hio 32 baking nayooo basi
 
Bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Anna amefariki dunia Septemba 3, 2024 akiwa na miaka 132 ambapo mamia ya watu wamekusanyika kumuaga katika Kijiji cha Huruma eneo la Uru Kaskazini – Moshi mkoani Kilimanjaro.

Bibi Anna ameweka rekodi ya kuishi umri mrefu zaidi katika kijiji hicho na vijiji jirani, Kufuatia kuishi katika umri huo, mamia ya waombolezaji hawakuwa na sababu ya kulia na kuhuzunika badala yake ilikuwa ni furaha, shangwe ya kucheza matarumbeta na vigelegele kama vyote huku wakimsifu na kumshukuru Mungu kwa kumpa bibi yao umri huo mrefu zaidi wa kuishi.

Bibi Anna alizaliwa Septemba 4, 1892 na kufariki dunia Septemba 3, 2024 akiwa na umri huo wa miaka 132, ibada ya kumuaka Bibi Anna imefanyika katika Kanisa Katoliki Jimbo la Huru Kaskazini Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Bibi Anna alijaliwa watoto tisa; nane wakiwa ni wanawake na mmoja wa kiume ambaye ameshatangulia mbele za haki, Bibi Anna alijaliwa wajukuu 45, vitukuu 132, virembwe 68 na virembwekize 8.
Huyo kawaida sana kwa kanda ya kaskazini..
 
Jamii yetu haithamini uhakiki na inapenda "hadithi hadithi, hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea."
Ila hiki kibwagizo uki kifikiria sana unaweza kubaki unacheka mwenyewe kama mwehu eti hadithi njoo uongo njoo utamu kolea 😆
 
Mfano mwane ana miaka 90 aya yey mama atakuwa na ngap sema alimzaa akiwa na miaka 20 probably 110
 
Madogo wa sahv sidhani kama wanaweza kuimba hiki kibwagizo bila kuuliza ina maana hadithi ni ya uongo alafu tunasikiliza 😆
Aah, wao wenyewe mbona wanaangalia movies za Hollywood na TV shows za ma dragon yanayopaa angani kwa mbawa?

Mimi niliangalia "Game of Thrones" nilipofika kwenye ma dragon tu nikashindwa kuendelea.

Sitaki ujinga mpaka kwenye movies na TV shows.
 
Aah, wao wenyewe mbona wanaangalia movies za Hollywood na TV shows za ma dragon yanayopaa angani kwa mbawa?

Mimi niliangakia "Game of Thrones" nilipofika kwenye ma dragon tu nikashindwa kuendelea.

Sitaki ujinga mpaka kwenye movies na TV shows.
Kweli wewe ni Kiranga umetisha 👐
 
Mkuu,

Si lazima vyeti.

Marehemu Alex Haley, muandishi maarufu wa Marekani (mweusi) aliyeandika kitabu cha maisha ya Malcolm X, aliandika kitabu cha "Roots" chenye historia ya kuunganisha familia yake ya Marekani na ile iliyokuwa Gambia, akawaunganisha ndugu waliopotezana kwa mamia ya miaka, kwa kufuatikia "oral tradition".

Babu wa babu wa babu wa babu yake wa vizazi vingi Kunta Kinte, alivyokuja Marekani, alikuwa kashikikia baadhi ya maneno ya kwao kama vike "Kambi Bolongo" (River Gambia) na "Juffure" kijijini kwao. Akawarithisha watoto wake historia ya kwao, wakarithishana miaka na miaka, mpaka Alex Haley akaja ku trace ike historia kwao Gambia, ambako alikutana na hostoria nyingine ya ma Griot wa Gambia iliyorekodi Kunta Kinte alivyotoweka Gambia.

Watu walijuwa na oral tradition iliyorekodi matukio, kwa hiyo hata kama vyeti havipo, kuna any documented oral tradition ikiyo credible?

Kuondokana na utata wa oral tradition kuweza kupotoshwa, pia, umri wa ntu unaweza kukadiriwa kwa vipimo vya kisayansi kama DNA tests, dental scan, wrist scan, clavicle ossification, incremental lines of dental root cementum.

Huyo bibi alihakikiwa kwa njia yoyote kati ya hizi?
Naona unataka kutumia "oral tradition" kuhakiki tarehe.

Unaweza patia tarehe ila chances za kukosea ni highest.

Kama unakumbuka Wamisionari ndio wa kwanza kutangulia na makanisa yao,yalifika zamani kabla ya German Political Administration kutia timu,hivyo kumbukumbu nyingi zilitunzwa parokiani mkuu.

Nasema hivi maana natoka hivyo vijiji anapotoka huyu bibi marehemu...Babu yangu alizaliwa 1911 kumbukumbu zipo mpaka wa leo....

Baba yake alikua anaitwa Mzee Kitali alizaliwa mwaka 1869 kumbukumbu zake zipo mpaka waleo Parish ya Kilema....

Kumbukumbu za 1869 zipo,iweje ya 1891 isiwepo ambapo ni juzi tu ukizi-compare?

Ila unachosema kwenye post yako ni sawa pia.
 
Huwa wanakadiria tu kipindi fulani , kwa tukio fulani.
Hapana, kanisa katoliki huwa wana kumbukumbu zote za kuzaliwa,ubatizo,kipaimara ,ndoa na kuzaliwa watoto kwa waumini wao,wana data zote, ukienda parokiani wanakuletea file lenye record zote
 
Mbona record za Nyerere kuzaliwa ambazo zipo kwenye parokia yake unazikubali ila za bibi hutaki kuamini kama zipo kwenye hilo kanisa lao.
Mkuu,mimi naamini zipo

On top of that natoka hivyo vijiji anapotoka huyu bibi maana baba wa babu yangu aliezaliwa 1869 kumbukumbu zake zipo Kilema Parish huyu bibi ni wa juzi tu 1892 ni lazima zipo

Nachojua hizi dates zipo disputed sana ila sidhani kama variation ni very high above 10%

Most definitely wapo within -10% to +10%
 
Hapana, kanisa katoliki huwa wana kumbukumbu zote za kuzaliwa,ubatizo,kipaimara ,ndoa na kuzaliwa watoto kwa waumini wao,wana data zote, ukienda parokiani wanakuletea file lenye record zote
Sawa
 
Naona unataka kutumia "oral tradition" kuhakiki tarehe.

Unaweza patia tarehe ila chances za kukosea ni highest.

Kama unakumbuka Wamisionari ndio wa kwanza kutangulia na makanisa yao,yalifika zamani kabla ya German Political Administration kutia timu,hivyo kumbukumbu nyingi zilitunzwa parokiani mkuu.

Nasema hivi maana natoka hivyo vijiji anapotoka huyu bibi marehemu...Babu yangu alizaliwa 1911 kumbukumbu zipo mpaka wa leo....

Baba yake alikua anaitwa Mzee Kitali alizaliwa mwaka 1869 kumbukumbu zake zipo mpaka waleo Parish ya Kilema....

Kumbukumbu za 1869 zipo,iweje ya 1891 isiwepo ambapo ni juzi tu ukizi-compare?

Ila unachosema kwenye post yako ni sawa pia.
Nimeeleza matatizo ya oral tradition na jinsi ya kuyakabili.

Mpaka sasa hakuna document za kuonesha huyu bibi kazaliwa 1892.
 
Nijalie umri zaidi ya huyo Bibi eee muumba wangu ,ndiyo maana mtoto wako nimeachana na pombe za kemikali ili walau niione dunia na vimbwanga vyake ,eeee muumba unisikie na unisaidie mwanao
Ukifikisha umri huo itakuwa wakati huo magari yanapanda watu na simu zinapiga watu.
 
Back
Top Bottom