Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,777
- 42,921
Bibi Anna ameweka rekodi ya kuishi umri mrefu zaidi katika kijiji hicho na vijiji jirani, Kufuatia kuishi katika umri huo, mamia ya waombolezaji hawakuwa na sababu ya kulia na kuhuzunika badala yake ilikuwa ni furaha, shangwe ya kucheza matarumbeta na vigelegele kama vyote huku wakimsifu na kumshukuru Mungu kwa kumpa bibi yao umri huo mrefu zaidi wa kuishi.
Bibi Anna alizaliwa Septemba 4, 1892 na kufariki dunia Septemba 3, 2024 akiwa na umri huo wa miaka 132, ibada ya kumuaka Bibi Anna imefanyika katika Kanisa Katoliki Jimbo la Huru Kaskazini Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Bibi Anna alijaliwa watoto tisa; nane wakiwa ni wanawake na mmoja wa kiume ambaye ameshatangulia mbele za haki, Bibi Anna alijaliwa wajukuu 45, vitukuu 132, virembwe 68 na virembwekize 8.