Shangwe laibuka mazishi ya bibi mwenye miaka 132 Moshi

Rekodi za Kanisa Katoliki la Mitume huonesha hivyo
Huonesha au zimeonesha? Hayo ni maneno mawili tofauti.

Huonesha maana yake ni kwamba habari kama hizi kwa kawaida huwa zinaoneshwa katika rekodi za kanisa. Hii ni general statement haihusiani moja kwa moja na kesi hii.

Zimeonesha maana yake kuna rekodi zinazoonesha kuwa huyu bibibkazaliwa 1892.

Now, which is which hapa?
 
Bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Anna amefariki dunia Septemba 3, 2024 akiwa na miaka 132 ambapo mamia ya watu wamekusanyika kumuaga katika Kijiji cha Huruma eneo la Uru Kaskazini – Moshi mkoani Kilimanjaro.

Bibi Anna ameweka rekodi ya kuishi umri mrefu zaidi katika kijiji hicho na vijiji jirani, Kufuatia kuishi katika umri huo, mamia ya waombolezaji hawakuwa na sababu ya kulia na kuhuzunika badala yake ilikuwa ni furaha, shangwe ya kucheza matarumbeta na vigelegele kama vyote huku wakimsifu na kumshukuru Mungu kwa kumpa bibi yao umri huo mrefu zaidi wa kuishi.

Bibi Anna alizaliwa Septemba 4, 1892 na kufariki dunia Septemba 3, 2024 akiwa na umri huo wa miaka 132, ibada ya kumuaka Bibi Anna imefanyika katika Kanisa Katoliki Jimbo la Huru Kaskazini Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Bibi Anna alijaliwa watoto tisa; nane wakiwa ni wanawake na mmoja wa kiume ambaye ameshatangulia mbele za haki, Bibi Anna alijaliwa wajukuu 45, vitukuu 132, virembwe 68 na virembwekize 8.
angekuaa ni mwanaume asingetobia 132 ila kwa bibi uyoo congratulations kwakee
 
RIP.

Wamehakikishaje kazaliwa 1892?
Hii mbona rahisi sana? First kama alibatizwa miaka ya kuzaliwa kanisa huwa wana kumbukumbu zote.
Pili unaweza kukadiria kwa kutumia watoto, mtoto wa kwanza au wa mwisho.
Tatu, kukadiria kupitia matukio aliyoona muhusika.
Aidha unaweza kutumia vizazi vilivyotokana na yeye
Nawasilisha
 
Habari za wajinga Global Tv msizilete humu habari hazina picha ya marehemu bali wajinga wakikatika na makelele tu.. Yule Bibi wa Ukoo wa Mbuya mwanae alistaafu usista Parokia ya Moshi last time i checked alikuwa na 135 mwaka 2007 sijui kama bado yupo
 
Bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Anna amefariki dunia Septemba 3, 2024 akiwa na miaka 132 ambapo mamia ya watu wamekusanyika kumuaga katika Kijiji cha Huruma eneo la Uru Kaskazini – Moshi mkoani Kilimanjaro.

Bibi Anna ameweka rekodi ya kuishi umri mrefu zaidi katika kijiji hicho na vijiji jirani, Kufuatia kuishi katika umri huo, mamia ya waombolezaji hawakuwa na sababu ya kulia na kuhuzunika badala yake ilikuwa ni furaha, shangwe ya kucheza matarumbeta na vigelegele kama vyote huku wakimsifu na kumshukuru Mungu kwa kumpa bibi yao umri huo mrefu zaidi wa kuishi.

Bibi Anna alizaliwa Septemba 4, 1892 na kufariki dunia Septemba 3, 2024 akiwa na umri huo wa miaka 132, ibada ya kumuaka Bibi Anna imefanyika katika Kanisa Katoliki Jimbo la Huru Kaskazini Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Bibi Anna alijaliwa watoto tisa; nane wakiwa ni wanawake na mmoja wa kiume ambaye ameshatangulia mbele za haki, Bibi Anna alijaliwa wajukuu 45, vitukuu 132, virembwe 68 na virembwekize 8.
2012 alifariki bibi yangu yeye alikua na mia na 3 , bibi huyo ndie alie nilea toka nikiwa na miezi miezi 3 , kwangu nilimuona ni kama mama yangu, wakati wa msiba watu walikua wanashangilia na kupiga vigelegele kuna muda nikitamani kuwapasua na chupa!
Ni moja kati ya kifo kilicho niuma sana.
 
Hii mbona rahisi sana? First kama alibatizwa miaka ya kuzaliwa kanisa huwa wana kumbukumbu zote.
Pili unaweza kukadiria kwa kutumia watoto, mtoto wa kwanza au wa mwisho.
Tatu, kukadiria kupitia matukio aliyoona muhusika.
Aidha unaweza kutumia vizazi vilivyotokana na yeye
Nawasilisha
Mpaka sasa sijaona mtu akihakikisha kwa kumbukumbu za kanisa.

Hakuna mtu akiyehakikisha kwa watoto.

Hakuna aliyehakiki kwa natukio aliyoyaona muhusika ambayo nayo yana shida ya uhakiki.

Hakuna hata mtu aliyesema mtoto wake wa kwanza alizaliwa mwaka huu, na tunahakiki hivi kwamba ni mtoto wake wa kwanza.
 
Back
Top Bottom