USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
6,317
2,000
Inamaana wachaga wote mmejiunga kupambana na sabaya mtu mmoja

USSR
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,997
2,000
Shahidi wa sita katika kesi ya Unyang'anyi wa Kutumia Silaha na uporaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkaoni Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya(34) na wenzake wawili,Bakari Rahibu Msangi ameieleza Mahakama kuwa kipigo alichokipata ni sawa na nusu kifo kwani alipoteza fahamu kwa muda huku akiwa amefungwa pingu mguuni na mikononi na walinzi wa Sabaya walimwambia kosa ni kuingilia dili ya Mkuu wao na sijui kama anaweza kubaki salama.

Sabaya na wenzake Silyvester Nyengu(26) na Daniel Mbura(38) wanatuhumiwa Kutumia Silaha kupora kiasi hicho cha pesa na Mali katika tukio lililotokea Februari 9 mwaka huu katika duka la Shahiid Store lililopo mtaa wa Bondeni Jijini Arusha duka linalomilikiwa na Mfanyabiashara Mohamed Saad Hajirini (45).

Msangi Alisema mungu ndio anajua kipigo alichokipata kutoka kwa walinzi wa Sabaya walivyompigia kwa amri ya Mkuu huyo na kusema tu hadi Sasa hawezi kusikia vizuri kufuatia masikio yake kutosikika vizuri kufuatia makofi mawili ya nguvu ya mfululizo aliyokuwa akipigwa kichwani,masikioni na mwili mzima na hajui kilichomfanya kuzinduka na kuwa hai hadi Sasa.

Alisema mlinzi wa Sabaya alimwambia Msangi kuwa tatizo lake ni kuingilia dili la Mkuu General Lengai Ole Sabaya na kuwa kiherehere kufuatilia mambo yake na salama yake ni yeye kumwonyesha Mohamed Saad Hajirini au Ally Saad Hajirini alipo vinginevyo hatabaki salama kwani anaweza kuuawa.

Shahidi Alisema hayo wakati akiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali,Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Mwandamizi,Odira Amworo na kusema kuwa wafanyabiashara hao wa kiaarabu walitafutwa na Sabaya usiku kucha hadi majumbani mwao lakini hawakuweza kufanikiwa kuwapata usiku huu hadi walipoamua kukataa tamaa.

Alisema wakati anazungushwa mjini maeneo mbalimbali kuwasaka akina Hajirini,Sabaya aliendelea kumtisha kwa Bastola akiwa ndani ya gari na aliomba kutouawawa kwa kuwa ana Mke na watoto ambao wote ni wagonjwa na hana shida yoyote na Sabaya lakini alisisitizwa kuhakikisha anawaonyesha Waarabu ili aweze kusalimika.

Msangi ambaye alikuwa akitoa ushahidi huku akilia kwa uchungu aliendelea kusema kuwa alimsikia Sabaya akisema kuwa shughuli zote anazifanya Arusha za kuwasaka Waarabu ni maelekezo kutoka ngazi ya juu hivyo hakuna kiongozi wa Arusha wala Polisi anayeweza kumuuliza chochote pindi anavyofanya shughuli Arusha.

Alisema na kumsikia Sabaya akitaka Derava amweleza Msangi kuwa mie napata maelekezo kutoka kwa mtu mmoja tu wa nchi hii ya Tanzania( alimtaja Marehemu Dk John Magufuli) na sio mtu mwingine yoyote hivyo usiwe na kiherehere cha kufuata katika mambo yake na akimwona akae mbali kabisa.

Shahidi Alisema Sabaya akimtafuta Mohamed Saad Hajirini hadi nyumbani na kwenye gari alibaki yeye na dereva na baada ya muda alisikia ukunga ukitoka katika nyumba ya Hajirini iliyopo katika majengo ya NHC yaliyopo eneo la Makao Mapya Jiiini Arusha.

Alisema ghafla aliona Sabaya na walinzi wake wakirudi katika magari lakini hawakuweza kumpata Hajirini na waliendelea kulalamika kukosekana kwa Mfanyabiashara huyo ila waliapa kumtia nguvuni na wakimpata cha moto atakiona màana anafanya biashara haramu na kuihujumu Nchi.

Msangi aliendelea kuieleza Mahakama kuwa mmoja wa walinzi wake anaitwa Andwer na dereva walioneiana kumsaidia na kumpa mbinu za kuwasiliana na Ndugu au rafiki na alifanya hivyo kwa kupewa simu na alimpigia Mke wake na alikwenda eneo walipo ndani ya muda wa nusu saa na alipofika alimwomba Sabaya kumsamehe mume wake lakini aliishia kutaka kupigwa Risasi ya kichwa.

Alisema bàadhi ya walinzi wa Sabaya walionyesha nia ya kumsaidia lakini walikuwa wakifanya kwa usiri mkubwa kwani miongoni mwao alikuwa anawajua na walimwaahidi kumsaidia Ila awe mtulivu kwa kuwa Mkuu wao alikuwa amelewa hivyo asiwe na papara.

Mwisho

View attachment 1871789
ana kitambi bado na yuko fit, hyu halali gerezani asilani
 
kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,144

SIO SABAYQ MI CCM
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,376
2,000
ana kitambi bado na yuko fit, hyu halali gerezani asilani
Nafikiri ulikuwa na umri wa kutambua kinachoendelea Mramba na Yona walipokamatwa. Kabla ya kukamatwa kuna vyumba vya selo vilifanyiwa ukarabati wa nguvu.

Tulipiga sana kelele humu JF lakini ndio hivyo, Mramba na Yona gerezani walikuwa kama hoteli ya nyota 3. Walichopungukiwa ilikuwa uhuru wa uraiani.

Sabaya yupo Kisongo japo huduma anazopata zitakuwa tofauti na wengi wengine walio rumande. Nina hakika anaendelea kupata milo mitatu kwa siku.
 
Perfect, issue ya Mramba nilikuwa kwenye late40s????. Ilisemekana hivyo.. na inawezekana sana tena sana. Sabaya anawweza akawa ndani, lkn kwa move ya samia, lolote can be speculated
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
57,157
2,000
Maajabu ya mahakama,.pamoja na mlolongo mrefu hivyo wa mashtaka si ajabu Sabaya kaachiwa huru na hao wapambe wa Sabaya ndio wakala mvua
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,997
2,000
Perfect, issue ya Mramba nilikuwa kwenye late40s????. Ilisemekana hivyo.. na inawezekana sana tena sana. Sabaya anawweza akawa ndani, lkn kwa move ya samia, lolote can be speculated
Gagnija nimeona nitafute mawazo ya watu maana kunawili huku siyo kwa kawaida. Ukiangalia mzee Rugemalila unaona kuwa yuko gerezani/remand prison
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,818
2,000
unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini?
Kifo ni kinyume cha uhai.
Nusu yake
Nusu ya kifo ni kuwa katika mazingira hatarishi ya kuondoa uhai kama vile kupigwa na kukabwa shingoni au kuzimia.
Kufa ni kutokuwa hai,ama nini kinaendelea baada ya kufa hakuna anayejua.
Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Ni kwa sababu pingu inaongezeka uduara wake kadri ya ukubwa wa hiko kinachofungwa unavyokua.

Endelea kuuliza maswali wakili mwenye akili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom