Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,730
2,000
sabaya angekuwa nchi zenye watu wenye hasira kali, alikuwa wa kufa nae na bomu la kujitoa mhanga!
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,481
2,000
huyo ni miongoni mwa wanufaika wa bia za bure
Ana manyuzi ya kutosha kumtetea huyo jamaa..!!!! Wakati mtu katoka nje ya wilaya na mkoa kwenda kutumia bunduki kwenye maduka ya watu huku akitaka apewe vitu mbalimba..!!! Yaani hata kama ni kesi ya uhujumu uchumi, kwani Arusha haina mkuu wa wilaya kama yeye?
 

E oxygen

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
326
250
Toto tundu kama kunakitu anajuajua namwona hana shaka kabisa du!!ni kama mission inakwenda kama ilivyopangwa.
 

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,357
2,000
Nianze kwa kusema, mimi sio mwanasheria ila naijua sheria na nashukuru Mungu amenijalia IQ kubwa sana.

Leo kwenye tovuti ya mwananchi, nimesoma muendelezo wa ushahidi dhidi ya Sabaya, na leo shahidi wa 6, diwani wa CCM alikuwa anatoa ushahidi wake.

Nimeshituka sana baada ya kujua kuwa aliyekuwa anatoa ushahidi ni diwani wa Arusha. Nilijua watu wa Arusha wajanja, mbona wanaongozwa na diwani mjinga kiasi hiki, kwanza hajui hata kupangilia uongo.


Kati ya mambo aliyoyaweka bayana ni :-

1. Kwanza alipigwa nusu ya kufa, mpaka akapoteza fahamu, na kuzinduka baadae...

2. Muda huo huo, alipigwa vibao viwili vya mfululizo, mpaka vikamuathili usikivu wake. Akawa hasikii vizuri.

2. Akachukuliwa na hadi kwa mfanyabiashara aliyekuwa anatafutwa na Sabaya...

Akasikia Sabaya anawaambia walinzi wa ile nyumba, yeye ni DC wa Hai...ametumwa na Magufuli kuwashughulikia waujumu uchumi. (Kumbuka jamaa, muda mfupi alipigwa nusu ya kufa, na vibao vikaziba masikio)

Baada ya kumkosa mfanyabiashara, Sabaya alitoka, Simu yake ikapigiwa, lilikuja jina la DC wa Arusha, Kenan Kihongosi,... ( Huyu aliyepigwa nusu kifo, alionaje Jina la DC Arusha?)

Baadae, Msangi anasema, baada ya mawasiliano yale, Sabaya alisema, Kenan ni maskini, anatumia Altezza.

Hoja nyingine, Msangi anasema, alimsikia Sabaya anasema yeye anamsikiliza Magufuli tu, vikalagosi wengine hawampi shida kabisaa.
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,297
2,000
Mbona jamaa hana kesi hata moja,mimi nawamaambiwa wale kwerea kwerea waliokuwa wanalipuka kwa shangwe kwamba sukumagang wameanza kuona moto.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,481
2,000
Mbona jamaa hana kesi hata moja,mimi nawamaambiwa wale kwerea kwerea waliokuwa wanalipuka kwa shangwe kwamba sukumagang wameanza kuona moto.
Itunze hii... Usisahau mashahidi wapo wengi.. Kama katika wote umemuona huyo mmoja kwamba kachemka, basi utachemka wewe.. By the way, shahidi kaweka maelezo kwa mtiririko wa matukio.

Tukio zima linaweza likawa limechukua masaa manne, lakini ukalisimulia kwa dakika 20 tu.. Unapopataka ni kuwa alizimia na kusikia kwa wakati mmoja..!! kumbe ni usimuliaji ila kiuhalisia kulikuwa na nterval
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,437
2,000
Mkuu,

Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?

Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.

Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?

Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Maswali gani ya kijinga hivi?au huna akili
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,297
2,000
Itunze hii... Usisahau mashahidi wapo wengi.. Kama katika wote umemuona huyo mmoja kwamba kachemka, basi utachemka wewe.. By the way, shahidi kaweka maelezo kwa mtiririko wa matukio.. Tukio zima linaweza likawa limechukua masaa manne, lakini ukalisimulia kwa dakika 20 tu.. Unapopataka ni kuwa alizimia na kusikia kwa wakati mmoja..!! kumbe ni usimuliaji ila kiuhalisia kulikuwa na nterval
Ishu sio ushahidi wa mtu mmoja,ni patern nzima ya tuhuma zinazomkabili sabaya,zimejaaa chuya kibao.

Sabaya analalamikiwa kubaka wanawake zaidi 40,japo kesi hii haijajumuishwa,sabaya analalamikiwa kupora 30 elfu kwa kutumi silaha.
Msichojua wengi sabaya anaanguka shutumani kwa chuki za baadhi ya watu aliokutana nao akitimiza majukumu yake.
Hifadhi tarehe utakuja kunambia.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,481
2,000
Ishu sio ushahidi wa mtu mmoja,ni patern nzima ya tuhuma zinazomkabili sabaya,zimejaaa chuya kibao.

Sabaya analalamikiwa kubaka wanawake zaidi 40,japo kesi hii haijajumuishwa,sabaya analalamikiwa kupora 30 elfu kwa kutumi silaha...
Unaamini katoka hayo yote, YOTE ANAONEWA? Na anaonewa na kila mtu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom