Qwy

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
4,471
2,000
Mkuu,

Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?

Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.

Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?

Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Sasa hapo swali gumu ni lipi, very childish.
Kwa mfano, haufahamu kama pingu ni adjustable? Yaani hilo nalo ni swali.
 
Kong Chi

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
386
500
Sio siri watu wengi walikuwa wakiishi kwa hofu, viongozi wengine waligeuka miungu mtu walivamia ofisi za watu na nyumba za watu kwa silaha na askari mchana kweupe bila woga, nchi ilikuwa police state na usalama wa Taifa iligeuka chombo cha mauaji na utekaji sio ulinzi wa nchi tena, wapinzani walikuwa wanafunguliwa kesi hewa, kufungwa na wengine kuuwawa waziwazi,uchaguzi ulikuwa ni wa wizi mkubwa ambao haujawahi kutokea katika historia ya nchi...yana mwisho lakini na mwisho wake ni aibu tupu
 
Godo

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
353
500
Shahidi anaposema alipigwa nusu kufa maana alifikishwa hospitali je ni hospitali gani alipokelewa na kupatiwa matibabu na wahudumu wa hiyo hospital walimtibu majeruhi bila kuwa na PF3 na hiyo PF3 ilitolewa kituo gani na huyo askali alimuona majeruhi na uongozi husika walipata taarifa kuwa kuna majeruhi katika hospitali fulani kajeruhiwa na muhusika tajwa, kuna maswali mengi sana hapo matukio hayo yote yaliwahi kulipotiwa kituo chochote cha polisi.
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,464
2,000
Nianze kwa kusema, mimi sio mwanasheria ila naijua sheria na nashukuru Mungu amenijalia IQ kubwa sana.

Leo kwenye tovuti ya mwananchi, nimesoma muendelezo wa ushahidi dhidi ya Sabaya, na leo shahidi wa 6, diwani wa CCM alikuwa anatoa ushahidi wake.

Nimeshituka sana baada ya kujua kuwa aliyekuwa anatoa ushahidi ni diwani wa Arusha. Nilijua watu wa Arusha wajanja, mbona wanaongozwa na diwani mjinga kiasi hiki, kwanza hajui hata kupangilia uongo.

Kati ya mambo aliyoyaweka bayana ni :-

1. Kwanza alipigwa nusu ya kufa, mpaka akapoteza fahamu, na kuzinduka baadae...

2. Muda huo huo, alipigwa vibao viwili vya mfululizo, mpaka vikamuathili usikivu wake. Akawa hasikii vizuri.

2. Akachukuliwa na hadi kwa mfanyabiashara aliyekuwa anatafutwa na Sabaya...

Akasikia Sabaya anawaambia walinzi wa ile nyumba, yeye ni DC wa Hai...ametumwa na Magufuli kuwashughulikia waujumu uchumi. (Kumbuka jamaa, muda mfupi alipigwa nusu ya kufa, na vibao vikaziba masikio)

Baada ya kumkosa mfanyabiashara, Sabaya alitoka, Simu yake ikapigiwa, lilikuja jina la DC wa Arusha, Kenan Kihongosi,... ( Huyu aliyepigwa nusu kifo, alionaje Jina la DC Arusha?)

Baadae, Msangi anasema, baada ya mawasiliano yale, Sabaya alisema, Kenan ni maskini, anatumia Altezza.

Hoja nyingine, Msangi anasema, alimsikia Sabaya anasema yeye anamsikiliza Magufuli tu, vikalagosi wengine hawampi shida kabisaa.
Masalia ya Sabaya..
Nenda court Arusha ukamtetee..
Meko katuachia wehu wengi sana wa mfano wako.
 
othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
2,887
2,000
Mkuu,

Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?

Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.

Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?

Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Zipo pingu za plastic zile wanazofungiwa magaidi kule Afghanistan, kiazi ww
 
othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
2,887
2,000
Usisahau na team upinzani inazidi kukiona cha moto. Wameanza na kaka lao Mbowe kapigwa kesi ya ugaidi, halafu atafungwa miaka ambayo idadi yake haijulikani. Akija kutoka huko ashakuwa zezeta tayari.

Hii nchi hii!!!!
Hakuna kesi ya kumfunga mbowe pale
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,899
2,000
Usisahau na team upinzani inazidi kukiona cha moto. Wameanza na kaka lao Mbowe kapigwa kesi ya ugaidi, halafu atafungwa miaka ambayo idadi yake haijulikani. Akija kutoka huko ashakuwa zezeta tayari.

Hii nchi hii!!!!
Ni wapuuzi wachache kama wewe wanaoweza kuamini kama pale kuna kesi! uhuni wa hawa jamaa umeshapuuzwa na ndio maana hata majirani zetu wanatucheka kumwita Mbowe GAIDI.
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,634
2,000
Shahidi wa sita katika kesi ya Unyang'anyi wa Kutumia Silaha na uporaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkaoni Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya(34) na wenzake wawili,Bakari Rahibu Msangi ameieleza Mahakama kuwa kipigo alichokipata ni sawa na nusu kifo kwani alipoteza fahamu kwa muda huku akiwa amefungwa pingu mguuni na mikononi na walinzi wa Sabaya walimwambia kosa ni kuingilia dili ya Mkuu wao na sijui kama anaweza kubaki salama.

Sabaya na wenzake Silyvester Nyengu(26) na Daniel Mbura(38) wanatuhumiwa Kutumia Silaha kupora kiasi hicho cha pesa na Mali katika tukio lililotokea Februari 9 mwaka huu katika duka la Shahiid Store lililopo mtaa wa Bondeni Jijini Arusha duka linalomilikiwa na Mfanyabiashara Mohamed Saad Hajirini (45).

Msangi Alisema mungu ndio anajua kipigo alichokipata kutoka kwa walinzi wa Sabaya walivyompigia kwa amri ya Mkuu huyo na kusema tu hadi Sasa hawezi kusikia vizuri kufuatia masikio yake kutosikika vizuri kufuatia makofi mawili ya nguvu ya mfululizo aliyokuwa akipigwa kichwani,masikioni na mwili mzima na hajui kilichomfanya kuzinduka na kuwa hai hadi Sasa.

Alisema mlinzi wa Sabaya alimwambia Msangi kuwa tatizo lake ni kuingilia dili la Mkuu General Lengai Ole Sabaya na kuwa kiherehere kufuatilia mambo yake na salama yake ni yeye kumwonyesha Mohamed Saad Hajirini au Ally Saad Hajirini alipo vinginevyo hatabaki salama kwani anaweza kuuawa.

Shahidi Alisema hayo wakati akiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali,Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Mwandamizi,Odira Amworo na kusema kuwa wafanyabiashara hao wa kiaarabu walitafutwa na Sabaya usiku kucha hadi majumbani mwao lakini hawakuweza kufanikiwa kuwapata usiku huu hadi walipoamua kukataa tamaa.

Alisema wakati anazungushwa mjini maeneo mbalimbali kuwasaka akina Hajirini,Sabaya aliendelea kumtisha kwa Bastola akiwa ndani ya gari na aliomba kutouawawa kwa kuwa ana Mke na watoto ambao wote ni wagonjwa na hana shida yoyote na Sabaya lakini alisisitizwa kuhakikisha anawaonyesha Waarabu ili aweze kusalimika.

Msangi ambaye alikuwa akitoa ushahidi huku akilia kwa uchungu aliendelea kusema kuwa alimsikia Sabaya akisema kuwa shughuli zote anazifanya Arusha za kuwasaka Waarabu ni maelekezo kutoka ngazi ya juu hivyo hakuna kiongozi wa Arusha wala Polisi anayeweza kumuuliza chochote pindi anavyofanya shughuli Arusha.

Alisema na kumsikia Sabaya akitaka Derava amweleza Msangi kuwa mie napata maelekezo kutoka kwa mtu mmoja tu wa nchi hii ya Tanzania( alimtaja Marehemu Dk John Magufuli) na sio mtu mwingine yoyote hivyo usiwe na kiherehere cha kufuata katika mambo yake na akimwona akae mbali kabisa.

Shahidi Alisema Sabaya akimtafuta Mohamed Saad Hajirini hadi nyumbani na kwenye gari alibaki yeye na dereva na baada ya muda alisikia ukunga ukitoka katika nyumba ya Hajirini iliyopo katika majengo ya NHC yaliyopo eneo la Makao Mapya Jiiini Arusha.

Alisema ghafla aliona Sabaya na walinzi wake wakirudi katika magari lakini hawakuweza kumpata Hajirini na waliendelea kulalamika kukosekana kwa Mfanyabiashara huyo ila waliapa kumtia nguvuni na wakimpata cha moto atakiona màana anafanya biashara haramu na kuihujumu Nchi.

Msangi aliendelea kuieleza Mahakama kuwa mmoja wa walinzi wake anaitwa Andwer na dereva walioneiana kumsaidia na kumpa mbinu za kuwasiliana na Ndugu au rafiki na alifanya hivyo kwa kupewa simu na alimpigia Mke wake na alikwenda eneo walipo ndani ya muda wa nusu saa na alipofika alimwomba Sabaya kumsamehe mume wake lakini aliishia kutaka kupigwa Risasi ya kichwa.

Alisema bàadhi ya walinzi wa Sabaya walionyesha nia ya kumsaidia lakini walikuwa wakifanya kwa usiri mkubwa kwani miongoni mwao alikuwa anawajua na walimwaahidi kumsaidia Ila awe mtulivu kwa kuwa Mkuu wao alikuwa amelewa hivyo asiwe na papara.

Mwisho

View attachment 1871789

Mmmh, aiseee...!!

Hii ni hatari sana. Yaani yote haya ni ili tu eti "kiongozi wa umma aitwaye Lengai Ole Sabaya DC wa Hai" by then kutaka pesa na utajiri wa haraka haraka kwa njia haramu kwa kutumia jasho la watu wengine na kwa ku - abuse mamlaka yake...!!

Hata kama sheria za nchi (law of land) zitakuwa manipulated ili kumuepusha na adhabu anayostahili, lakini kamwe hataikwepa KARMA huyu....!!
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,822
2,000
Kweli tulikuwa hatuna utawala...yaani a simple mkuu wa wilaya anafanya haya yote...mkuu wa wilaya...

Tuna tatizo kubwa sana Tanzania, nawaunga mkono wanaosema katiba hii iangaliwe upya.
 
G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
763
1,000
Ni wapuuzi wachache kama wewe wanaoweza kuamini kama pale kuna kesi! uhuni wa hawa jamaa umeshapuuzwa na ndio maana hata majirani zetu wanatucheka kumwita Mbowe GAIDI.
Ni kweli hakuna kesi. Lkn kufungwa atafugwa. Nadhani unakumbuka mashekhe wamekaa miaka 9 gerezani pamoja na kwamba hawakuwa na kesi.

Nchi ngumu sana
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,598
2,000
Duh hii nchi tulishafika pabaya.

Sana tu na sina imani kama hata sasa tumetoka katika mfumo huu mbaya , halafu Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Arusha pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Arusha hawakuwa na taarifa za mwanaCCM mwenzao toka wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro akifanya mambo haya .
Sheria Na. 24 ya mwaka 1966 ya Ulinzi na Usalama wa Taifa, Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU), Katibu Tawala wa Mkoa atasimamia Maagizo ya KUU
1.2 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya

  • Madaraka yake yanatiririka kutoka kwa Rais kupitia kwa Mkuu wa Mkoa
  • Madaraka kwa mujibu wa sheria Na 19 ya 1997 (kumweka mtu kuzuizini masaa 48 mfulilizo)

Au Hizi kamati ni kwa ajili ya kufuatiliwa wapinzani na siyo za ulinzi na usalama wa waTanzania.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
55,246
2,000
Nianze kwa kusema, mimi sio mwanasheria ila naijua sheria na nashukuru Mungu amenijalia IQ kubwa sana.

Leo kwenye tovuti ya mwananchi, nimesoma muendelezo wa ushahidi dhidi ya Sabaya, na leo shahidi wa 6, diwani wa CCM alikuwa anatoa ushahidi wake.

Nimeshituka sana baada ya kujua kuwa aliyekuwa anatoa ushahidi ni diwani wa Arusha. Nilijua watu wa Arusha wajanja, mbona wanaongozwa na diwani mjinga kiasi hiki, kwanza hajui hata kupangilia uongo.

Kati ya mambo aliyoyaweka bayana ni :-

1. Kwanza alipigwa nusu ya kufa, mpaka akapoteza fahamu, na kuzinduka baadae...

2. Muda huo huo, alipigwa vibao viwili vya mfululizo, mpaka vikamuathili usikivu wake. Akawa hasikii vizuri.

2. Akachukuliwa na hadi kwa mfanyabiashara aliyekuwa anatafutwa na Sabaya...

Akasikia Sabaya anawaambia walinzi wa ile nyumba, yeye ni DC wa Hai...ametumwa na Magufuli kuwashughulikia waujumu uchumi. (Kumbuka jamaa, muda mfupi alipigwa nusu ya kufa, na vibao vikaziba masikio)

Baada ya kumkosa mfanyabiashara, Sabaya alitoka, Simu yake ikapigiwa, lilikuja jina la DC wa Arusha, Kenan Kihongosi,... ( Huyu aliyepigwa nusu kifo, alionaje Jina la DC Arusha?)

Baadae, Msangi anasema, baada ya mawasiliano yale, Sabaya alisema, Kenan ni maskini, anatumia Altezza.

Hoja nyingine, Msangi anasema, alimsikia Sabaya anasema yeye anamsikiliza Magufuli tu, vikalagosi wengine hawampi shida kabisaa.
hahaha huu ugoro ulioandika hapa ndiyo unatokana na hiyo IQ yako kubwa uliyokua nayo???
 
Kitimoto

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
749
225
Huyu kijana usalama wake ni kubaki jela maisha yote.
Kuna mlevi mmoja wa maji jana nilimsikia akisema huyu ni mtu wa system kesi itaisha ataachiwa na atapewa Ubalozi wa nchi mojawapo ataenda kuishi uko.

Tuvute subira tuone mwisho wa kesi.
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
8,957
2,000
Mkuu,

Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?

Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.

Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?

Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Kuzimia ni nusu ya kufa jomba
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom