SGS na ALS wamekuja kusema wa makinikia

SGS na ALS wamekuja kusema wa makinikia

Inaelekea kazi itakuwa rahisi as far as Acacia wanajitahidi kuji-expose kuleta taarifa hata kabla ya kuambiwa kuleta ushahidi.

Hebu angalia data hizi hapa chini;

i. Kwa mujibu wa kauli ya Acacia na maofisa watendaji wa TMAA waliotimuliwa kazi kwa tuhuma za kuhongwa na maofisa wa Acacia, kiwango cha dhahabu kwenye tani moja ya mchanga ni gram 200.


ii. Kwa mujibu wa Kamati ya Prof. Mruma, (iliyotolewa Mei 2017), kiwango cha dhahabu kwenye tani moja ya mchanga ni kati ya gram 671 na 2375.


iii. Kwa mujibu wa taarifa ya vipimo vya kampuni (maabara) ya ASL Metallurgy Ltd (iliyotolewa Juni 12/2017, Austraia) ikiwa ni matokeo ya kazi iliyopelekwa na Acacia, kiwango cha dhahabu kwenye tani moja ya mchanga ni gram 329


iv. Kwa mujibu wa barua ya kampuni ya SGS (June 15/2017, Geneva, Switzerland) ikithibitisha vipimo vya sampuli kwenye makontena 44 tu, yenye urefu wa futi 20, kutoka Acacia, kati ya Mei 2016 na Februari 2017, kiwango cha dhahabu kwenye tani moja ya mchanga ni gram 164

Twende tu, ukweli utapatikana si muda mrefu. Ila timing, tarehe za kuwasilisha matokeo hayo, na disclaimer statement kuwa uchambuzi huo wa kimaabara haukusudiwi kutumika kutanzua mgogo wa kibiashara mahakamani, ni maeneo interesting tukifanya uchambuzi wa kina.
 
Sawa na upo sahihi kwamba Sampuli huwa zinatunzwa. Issue ni wamechukua kutoka kwenye containers ambazo zimezuiliwa? Kama ni kutoka sehemu nyingine hazitakidhi kwenye utatuzi wa suala hili kwamba takwimu za Prof Mruma ni sahihi au za ACACIA. Hapa kumetokea kutokuaminiana hivyo kifanyike uchunguzi wa pamoja
SGS wanahusika na hizo container zilizozuiliwa na wana sample ya conatina zote.
 
Tatizo ni namna mruma alivyo mdanganya rais, repoti ya mruma ina mapungufu mengi sana kitalaam na hasa kwenye swala zima la 'grade & metal content estimation' leo hii ukimuuliza mruma ulizipataje zile data anaweza kujikojolea na kama si kujinyea kabisa. Hata kwenye mazungumzo jamaa waki propose swala la kuchukua sample upya ukweli ni kuwa rais na nchi kwa ujumla tutaumbuka vibaya, tunacho takiwa kukifanya kwa sasa ni 'kupoteza ushaidi' fasta, hayo makinikia tukayamwage au tuwagawie wachimbaji wadogo wadogo otherwise tutakuja kudondokea puz kwa maamuzi ya kukurupuka
Kati yako wewe na Prof Mruma nan alifanya utafiti? Mbona bongo tunajafanya wajuaji sana wakt hata kutatua matatizo kwenye maisha yetu hatuwezi?
 
Unapigana vita usiyo ijua. Hapa mwizi ni serikali ya CCM
Una kichaa cha fikra! Mimi cjaongelea vyama kwa sababu najua walolifikisha taifa hili hapa, wamekimbia CCM na kuja huko mnakojifanya walokole kumbe ni kichaka cha maovu.
Kwa sababu hata tukinyoosheana vidole haisaidii chochote! hapa swala ni kuangalia tunaokoa vipi mali zetu baada ya kumpata mtu thabiti aliyejitoa muhanga kuanzishwa vita hivi vya ukombozi wa kiuchumi.
Wewe unaewaona wazungu Mali endelea kuwakumbatia, kwa kuwa unapatapara makombo kidogo ili usogeze siku mbele. Pole!.
 
Kuhusu hicho kiwango cha madini kilichopo kwenye Makinikia ( copper concentrate) kinachosemwa na Kamati ya Prof Mruma kwa uhalisia huwa hakipo. Kwa hiyo kama kimeonekana ina maana kulikuwa na kitu kinafanyika. Hivyo vipimo vya pamoja kwa kutumia Sampuli kutoka kwenye hayo makontena ufanyike ili uongo wa Prof Mruma ufahamike. Tatizo lipo wapi?
Hayaa!
 
Angalia kuna element zingine zimefanyiwa analysis, kwenye hizo docs.
Mie nilikuwa nawaongelea SGS na jinsi wanavyofanyia kazi, kama wangetakiwa kupima uranium, calcium, nitrate n.k wangefanya hivyo lakini wao wanapima gold, silver na copper pekee na ndivyo ripoti zao zinaonyesha hapo.
 
SGS wanahusika na hizo container zilizozuiliwa na wana sample ya conatina zote.
Upo sahihi. Kwa vile kumetokea kutokubaliana kuhusu zipi ni takwimu sahihi na makontena yapo pale bandarini basi kifanyike uchunguzi wa pamoja kuondoa huo mkanganyiko.
 
Profesa Mruma akae tayari sasa ni mpambano na the leading laboratory in the mining industry .
Hapa patam " Muda ndiyo Msema kweli"
Jamani, kama tangu 2007 tulisema kwamba " TUNAIBIWA KWELI KWELI" na takwimu za Prof. Mruma kuunga mkono kauli hiyo. Sasa huo woga mumeutoa wapi? Kama laboratories za Pro. Mduma ni hafifu hazioni mbali, basi kwa maelezo yako kwa nini tusitegemee kiwango kikubwa zaidi ya cha Mduma kutoka kwa hizo leading laboratories zako? Au ndio yaleyale ya Lowassa baada ya kutoa kitu kidogo tukabadili gea angani? Yote tuliyoyahubiri kwa takwibani miaka 20 kuwa Lowassa ni fisadi papa tukayakana ghafla bin vuu tukaambiwa kuwa Lowassa ni mtu safi tatizo ni CCM. Katika hili saga la makinikia naanza kuyaona yale yale ya gea kubadiliswa angani. Sasa tumeanza kuambiwa hakuna wizi kwenye makinikia, Acacia ni safi tatizo ni mikataba yetu.( pamoja na kuambiwa kuwa Acacia ni dubious co.) hakika rushwa ni zaidi ya hatari.
 
Profesa Mruma akae tayari sasa ni mpambano na the leading laboratory in the mining industry .
Hapa patam " Muda ndiyo Msema kweli"
Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu tukae tayari. Hii si ya prof Mruma pekee. Tunakusubiri wewe na hao Acacia wenzako, karibuni sana
 
Hii ishu ya makanikia itakuja ishia chinichini kama barafu inayoyeyuka. Hakuna atakaekuja kujua ni nini kinaendelea. Kwa sasa pigeni kelele ila time will tell.

Nikiangalia Yale magari yaliyokuwa yanapita mtaani kuhimiza bar zifunguliwe saa mbili asubuhi ili tuiangalie ripoti, sichelewi kuamini kuwa ilikuwa ni promo ya kisiasa.

Quote my words
 
Kati yako wewe na Prof Mruma nan alifanya utafiti? Mbona bongo tunajafanya wajuaji sana wakt hata kutatua matatizo kwenye maisha yetu hatuwezi?
Ieleweke kuwa baadhi ya vipimo vya viwango vya madini yaliyomo kwenye Makinikia hufanywa na Watanzania ambao walifundishwa na Prof Mruma. Hivyo kumuona Prof Mruma amejitungia huko ni kumdhalilisha Mtanzania mwenzetu na kuwatukuza watu weupe.
ACACIA ni wafanyabiasha na kila mfanya biashara siku zote ni kujinufaisha. Kama hayo Makinikia hayafaida kwa vipi waseme wanapata hasara biliion 2-3 fedha za Kitanzania kwa siku? Vipi waseme watafunga Mgodi ? Kwani biashara kuu ya Mgodi ni Dhahabu au Makinikia? Iwaje sasa mabaki( by products) ndiyo yaonekane yanathamani kubwa na ndiyo yanayoendesha Mgodi? Kwa mantiki hiyo Mgodi wa Bulyanhulu una Dhahabu kidogo inayoweza kuchenjuliwa kuliko iliyomo kwenye Makinikia? Hivyo basi kuondoa mkanganyiko huo uchunguzi wa pamoja hufanyike ili kila upande uridhike
 
Makontaina yako bandarini kibaraka wewe makontaina waliyosafirisha ni mengi kuliko waliyodeclare. Wewe tulia acha wazalendo tupiganie chetu wewe na tundu lisu nendeni mkale makombo Ya vyakula vinavyoangushwa chini na waxungu wa accacia

Huo uzalendo umeanza baada ya kuti.Wa dole?
 
Kumbuka lengo ilikuwa kutaka kujua nini siri ya Kusafirisha Mchanga Nje, so we wanted to know the truth..... and We have knew the truth. Whether ipo kwa contract on not what we wanted is no tell Tanzania and the whole world kuwa kinachopelekwa Nje siyo Mchanga as we used to be told. Pia siyo kweli kuwa ratio za payable meneral zinazosemwa kwenye huo mchanga kuwa ni ndogo kama wanavyoadvocate. Pia siyo kweli other mineral are of the threshhold kiasi kwamba haya thamani as we used to be told as well.

Hicho ndicho we wanted to know na Dunia kwa Ujumla kujua. Sasa tumemshika Mchawi wasiwasi wetu nini are not still believing to this still???

..hakuna haja ya kubishana nani mkweli na nani muongo.

..solution ni serikali ya Tz kuuza mchanga wa dhahabu.

..Kitakachopatikana tuwakatie acacia vile walivyo-under declare. Sisi Tz tuendelee na faida tutakayoipata.
 
yani wewe unafikiria international business zinaoperate kama vile kkoo ilo ndo tatizo lako
na sijui unajua nini kuhusu international business operations
na sijui una exposure yoyote kuhusu mineral industry duniani linaweza kua sio tatizo lako labda ni umizuka, ujuaji, maarifa nusu na udumavu, naomba usinichukulie kama nakutukana lakini ndio ukweli wenyewe.
kwanini makampuni yanakua na independent laboratory kwenye kazi zao, lengo ni kupata exactly data ya kitu kinachotakiwa, ndani ya makampuni kuna maabara zao akini aziwi validy hadi maabara zinginge independent laboratory ku verify content na hapo ni kujiridhisha kama kiwango husika cha mzigo hakizidi wala akipungui hii ni kutokana na standards za mteja wake ambae anaweza kua kampuni x basically inajikita kwa kuchenjua makanikia
kama umewahi kufanya kazi japo agency yyt ya kimataifa au kampuni za bishara za imataifa au supermarket utaelewa kwa nini watu wana dought ratio ya samples na result zilizotolewa na ma prof wetu
kila mzigo/packaged una kua proved kila mahala hadi kupata kiwango knachotakiwa, yan maabara za uku zina prove kiwango kilichopo na taarifa zinatumwa, maabara za uko nje nazo zinaverify ili kuepuka kupata loss ama fraud katika kazi zao.
kampuni ndogo ya kuuza mazbibu ya africa kusini inaoperate kiasi kwamba huwezi kuba hata zabibu moja sembuse dhahabu na makanikia
siasa katika professional ndo mazara yake haya
mtu anatoa findings kila mtu anambishia sabu hata kwa wasio na elimu wanajua huo ni uongo
mnachotaka kutuaminisha ni kwamba mzungu alivunjavunja dhahabu ili asilipe kodi na ii akifika ulaya akapate dhahabu nyingi, na faida kubwa. yani mtu ambae 95 percent ni yake bado aibe kwenye 4% tena 0.4 % ya makanikia
cant make sense
ni wajinga tuu ndo watakubali upuuzi huu

Heshima kwako Ndugu.
 
Kwa hiyo ile tume ya mh. Rais unaiona hawajui walichokifanya mambumbumbu woote wakosee ww ndio unaejua ? Wakati mchanga wenyewe hata hujauwona unapinga pinga tu gologoso kweli ww na lazima waturudishie ela zetu wametuibia sana
 
Ndugu Lissu anawazidi akili sana, ni vyema mkamshirikisha, kinacho hangaikiwa sasa hivi Lissu alikiona miaka 20 iliyo pita, wakati huo mkidai kuwa "tunapata tunacho stahili", mambo yanaenda vizuri,...............bla bla nyingi. Hivi kipindi chote hicho mlikuwa mnakula makombo??????.…lisu hakuwazuia kufanya makosa yenu kama ambavyo hatowazuia kusahihisha. Wapuuzi sana nyie
Ni Lissu huyo huyo kwa miaka 20 alituambia Lowassa ni fisadi papa. Umesahau kuwa Lissu ndie aliyeandaa list of shame. Lissu hana sifa ya kuaminika, Lissu si wa kumtilia maanani, Lissu ni kigeugeu, Lissu kama Njonjo wanawadharau wataalam wazawa, lakini hii sishangai kwani hata yeye hajithamini. Rejea maelezo yake ya kutetea kukiuza chama chetu cha CHADEMA kwa Lowassa, kwa mbwembwe kubwa Lissu alitueleza ushauri walioupata kutoka kwa consultant kutoka nje kuwa hoja ya ufisadi haina nguvu. Hii ina maana akina Lissu ni mambumbumbu. Kama wangekuwa makini na wasomi kama wanavyojibainisha kwa nini wasilione hili kwa miaka yote 20? Akina Lissu ni watu wa matukio. No tukio no Lissu. Sisi hatuna shida na Lissu wala hatupi pressure, tunachofanya ni kuwazindua nyinyi ambao mko possessed na Lissu.
 
Hivi kwanini wasichukuliwe manyoka kutoka Arusha, Kahama au Chunya wapewe kontena moja pale waoshe tuone kinapatikana nini, Naona mchezo rahisi tunasumbuana tu hata bajeti inatupita hivi hivi motor vehicle tunaanza kulipa mara mbili nyambafu sana.
 
Back
Top Bottom