Shirika la Reli: Treni ya SGR haitumii umeme mwingi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa, amesema umeme utakaotumika kwenye uendeshaji wa Treni ya Umeme ya SGR una KV 220 lakini kuna transfoma itakayokuwa inapunguza umeme mpaka KV 25.

Aidha amesema treni ikifika mikoa ya Kigoma na Mwanza matumizi ya uhitaji yatakapoongezeka ndipo umeme mwingi utahitajika na tayari upo kwani wameunganishwa na gridi ya Taifa.

Kwa upande mwengine Mkurugenzi Miondombinu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa amesema “Hatua ya leo kwetu ni muhimu kwamba tunafanya majaribio na inatuhakikishia kuanza safari mwaka huu na kama tulivyoelekezwa na Mh. Rais kwamba kufikia July safari ziwe zimeanza na naamini hadi July safari zitaanza Dar hadi Dodoma, hii ni hatua kubwa sana”

“Kwa namna ilivyosanifiwa itakapofika kiwango cha juu cha uendeshaji cha KM 160 kwa saa tutakuwa tunatumia chini ya dakika 90, haya ni majaribio na majaribio ni hatua lakini safari itachukua dakika 90”

20240226_131235.jpg

20240226_131241.jpg

20240226_131249.jpg
 
Mzee umeandika andika tu ,izo KV ni kitu Gani, hatuna kitu kama hicho katika umeme, wala SI unit inayoitwa KV
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom