Source ya habari please!
Hivi tuna rais kweli? Kwa nini alikubali aibu hii kujitokeza? Nionavyo mimi huyu 'rais' wetu hana mamlaka yoyote, mamlaka yako kwa wengine, nasikia wahindi kama wanne hivi na 'mzalendo' mmoja -- ndiyo wanamsukuma saa zote, na ndiyo waligharamia kampeni za mabango ya kufuru, wakijua mtu wao hauziki safari hii!
Eee Mungu, polepole unaanza kusikia kilio cha wapenda haki, usitutupe!
Source ya habari please!
hahaha nyoka amewekewa yai la kuchemsha na ameshalimeza
huo mpasuko wake ni mtafutano
Like PCCB like TFF...................Sasa PCCB watoe kauli nyingine kujifafanua kuwa "walimaanisha" nini...
Wakati PCCB wamemshafisha Chenge kwenye kadhia ya Radar kuwa suala hilo limekwisha na Chenge hahusiki, SFO wenyewe wamekanusha kuisha kwa suala hilo na kueleza litatinga mahakama kuu ya Uingereza mwishoni mwa mwezi huu na huko ndiko suala litaamuliwa kama limekwisha au laa.
Taarifa kutoka ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari, umeweka wazi kila kitu kuwa kadhia hiyo bado haijakwisha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kitu ambacho kimekubaliwa kuwa kimekwisha, ni uchunguzi dhidi ya kadhia hiyo ndio umemalizika baada ya BAE kukubali wamegawa rushwa, ila badala ya kuwataja waliowagawia, wamekubali kulipa faini ambayo serikali ya Tanzania, itarudishiwa lile fungu lililokamuliwa ili wakubwa wale.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ubalozini, Mahakama ya Uingereza, inaweza kuamua kuwa hawakubali faini hiyo kulipwa, bali wakalazimisha lazima majina ya walarushwa yatajwe badala na kuzibwa midomo kwa faini na fidia, na kama itakuwa ndio hivyo, tuhuma za Chenge kwenye kadhia hiyo zinabaki kuwa bado ziko pale pale?.
Kama taarifa hii ya ubalozi wa Uingereza ni ya kweli, crdedibility ya PCCB yetu kwenye kuwasafisha mafisadi iko wapi?.