Kampuni ya Minjingu na Bashe nani wa kulaumiwa suala la mifuko 776 ya mchanga ikiuzwa kama mbolea kwa fedha za ruzuku ya Serikali?

juma30

Senior Member
Jun 25, 2022
149
421
Uongozi wa Kampuni ya uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mbolea ya Minjingu Mines and Fertiliser Limited (MMFL) umefafanua kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwa Kampuni hiyo kuhusu upatikanaji wa mifuko 776 ya mchanga kwenye ghala lake lililopo mjini Njombe na kusema Kampuni hiyo haijawahi kufanya hujuma yoyote kwa Wakulima au Wadau wa kilimo katika miaka yake 22 ya kazi.

“Tunautaarifu umma kwamba hatujawahi kuhujumu Wakulima au Wadau wa kilimo kwa kuzalisha na au kufungasha mchanga/udongo katika mifuko yake kama mbadala wa mbolea na kwa kipindi chote Kampuni yeti imeendelea kuwa na ushirikiano wa karibu na Serikali katika kuhakikisha Wakulima wanapata mbolea ya ruzuku kwa wakati na kwa bei nafuu”

“Afisa Mauzo wa MMFL kituo cha Njombe Gervas John Mtitu alipatikana na upotevu wa mbolea jambo ambalo alilikiri na baada ya upotevu huo aliendelea kutoonyesha ushirikiano licha ya jitihada mbalimbali za kumtafuta ambapo baada ya kutoendelea kupata ushirikiano tarehe 28/1/2023 Kampuni ilitoa taarifa Kituo cha Polisi Njombe mjini kuhusiana na upotevu wa mbolea na kutoonekana kazini ambapo tulipatiwa RB No. NJ/RB/390/2023”

“Tarehe 20/2/2023 Polisi walifika kwenye ghala na kumweleza Afisa Masoko wa MMFL kwamba walifika kufanya ukaguzi baada ya kupata taarifa kwamba kulikuwa na baadhi ya mifuko ambayo haikuwa na mbolea bali bidhaa nyingine na kwamba katika ukaguzi huo walibaini kwamba kwenye ile mifuko ya zamani (ambayo iliachwa na Gervas John Mtitu) kulikuwa na mifuko yenye mchanga”

“TFRA waliiandikia MMFL barua tarehe 24/2/2023 ambapo maudhui ya barua ilikuwa ni kukutwa na bidhaa ambayo siyo mbolea na Kampuni ilipigwa faini ya shilingi milioni 30 na ikailipa faini hiyo tarehe 25/2/2023, hata hivyo MMFL imesikitishwa na suala hilo (ambalo Mamlaka inayohusika Kisheria ilishalitolea maamuzi) kuletwa tena tarehe 5 Machi 2023 kwenye jamii na kuleta sintofahamu kwa jamii” imeeleza taarifa ya Kampuni hiyo. #MillardAyoUPDATES
 
Kama kampuni ilipigwa faini na ikalipa, sasa kwanini kampuni hiyo inaogopa ama inabadili kwamba jambo hili lisifike kwenye jamii (kwakua tu walisha malizana..??).

Anyway.......
Kampuni ya mbole haipaswi ijitoe kwenye hujuma hii kwasababu ni wao ndio walimuajiri mtu(afisa masoko) ambae amehusika kwenye hujuma hii.
 
Ukisoma maelezo yao ni kama wanamlaumu Bashe kwamba ishu hiyo anaifahamu na hatua zilishachukuliwa za kisheria wanachomlaumu kwanini jambo hilo ameliibua upya tena kwenye mkutano wa Rais? na ndio maana kama ulimzikiliza Rais naye hakusema chochote kuhusu suala hilo siku hiyo.
 
Kimsingi Hussein anajipalilia kisiasa na anataka boss wake aone kwamba anawajibika, lakini kampuni haikupaswa kumlaumu mtu yeyote kwakua tayari walisha wajibika.
 
Ni kama kuna kitu kimejicha baina ya Kampuni na Bashe ila uzuri nchi haina siri itajulikana tu mbivu na mbichi
 
Back
Top Bottom