Taarifa ya balozi wa Tanzania nchini Japan na fursa katika zao la kahawa kutoka Tanzania

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
"Jina langu ni Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Japan, nikiwa na dhamana ya kuiwakilisha pia nchi yetu katika nchi za Australia, New Zealand na Papua New Guinea.

Leo tumekusanyika hapa katika mojawapo ya makampuni makubwa nchini Japan yanayojishughulisha na biashara ya chakula Japan na barani Asia, kwa ujumla. Kusanyiko hili ni mahsusi kwa ajili ya kushuhudia kwa furaha na bashasha kubwa hafla ya uonjaji wa kahawa ya Tanzania, chapa ya GDM inayozalishwa huko Mbozi mkoani Mbeya, Tanzania. Nitumie nafasi hii kuipongeza kwa dhati Kampuni ya GDM ambayo ni kampuni ya kitanzania kwa mafanikio haya makubwa.

Kahawa hii imezinduliwa rasmi jusi tarehe 7 Juni 2023katika migahawa mikubwa na maarufu ya Japan ambayo inapatikana katika viunga vyote vya Japan.

Kuzinduliwa kwa kahawa ya GDM hapa Japan kunapandisha zaidi uhakika wa soko la kahawa ya Tanzania nchini Japan ambayo imejizoelea umaarufu mkubwa kwa ubora na ladha ya aina yake na kupewa jina la kibiashara la Tanzania Kilimanjaro Coffee.

Kahawa ya Tanzania inayouzwa nchini Japan ni kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha,Manyara, Kagera, Mara, Tanga, Morogoro, Njombe, Iringa,Katavi, Rukwa, Ruvuma, Kigoma, Songwe na Mbeya.

Hivyo, napenda kuchukua nafasi hii, kutoa rai kwa watanzania wote hususan, wakulima wa zao la kahawa,watayarishaji, wasafirishaji na wafanyabiashara wa zao hili kuchangamkia fursa ya soko hili la Japan ambalo linakua siku hadi siku.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Bodi ya Kahawa Tanzania Japan ni nchi ya kwanza inayonunua kahawa ya Tanzania kwa wingi ambapo, kwa mwaka Tanzania inauza kahawa nchini Japan, wastani wa asilimia 33 ya kahawa inayolimwa nchini, Kiwango hicho ni sawa na wastani wa tani 15,000 yakahawa ya Tanzania inayouzwa Japan, ikilinganishwa na matumizi na uhitaji wa Japan wa wastani wa tani laki nne na elfu hamsini na tatu za kahawa kwa mwaka (tani 453,000. Hivyo, ni dhahiri kuwa soko la kahawa hapa nchini Japan,bado ni kubwa na hiyo ni fursa adhimu kwa watanzania wenzangu.

Napenda kutoa wito kwa watanzania wenzangu kuzingatia ubora wa viwango kwa mazao tunayolima nchini kwani nchi nyingi tunakouza bidhaa zetu hususan, hapa Japan wanazingatia sana viwango. Hivyo, ili kulikamata soko hili la Japan ipasavyo, inatupasa kwenda sambamba na mahitajiya kidunia, ikiwemo, uzalishaji kwa viwango bora.

Katika shughuli hii ya leo, tumepokea mrejesho mzuri wa kahawa ya Tanzania na maoni ya namna ya kuongeza zaidisoko la kahawa, ambalo kwa namna moja ama nyingine linawagusa wakulima wa Tanzania moja kwa moja katika kuongeza uchumi wao na pato la Taifa kwa ujumla.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwa kuwekeza katik amiradi ya muda mrefu na mifupi pamoja na maeneo yamsingi ya kutatua changamoto za kilimo kuanzia shambani hadi sokoni ili kujihakikishia uhakika wa chakula, kulisha wengine kibiashara duniani, lakini pia wakulima kujipatia kipato cha kutosha ili kupunguza umaskini.

Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita kwa kasi kubwa imewekeza kwenye rasilimali fedha na watu pamoja na uhamasishaji wa sekta binafsi kuwekeza na kukifanya kilimo kuanza kutoa ajira zenye staha hususan, kwa vijanana wanawake, ikiwa ni pamoja na hatua ya kuongeza bajetiya Wizara ya Kilimo na kujenga msingi imara wa utekelezajiwa mipango ya kilimo yenye kutazama Tanzania ifikapomwaka 2050.

Nasi Ubalozi tuna jukumu kubwa la kuendelea kutafutamasoko ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ikiwemo, mazao ya kilimo kama kahawa, kwa kutangaza bidhaa hizo na kutafuta wawekezaji katika kuendeleza sektambalimbali kama vile sekta ya kilimo hususan, kilimo cha biashara kwa mazao ya kimkakati. Hivyo, nirejee wito wangu kwa watanzania kuzingatia ubora wa viwangokatika bidhaa tunazozalisha ili kujihakikishia soko la uhakika kwa wakati wote.

Nihitimishe kwa kuwahamasisha wazalishaji, wanunuzi nawasafirishaji wa kahawa ya Tanzania na wadau wenginewote wa mnyororo wa thamani wa zao hili kuja kushirikikwa wingi katika Maonesho Makubwa ya Kimataifa yaKahawa ya Mwaka 2023 (World Speciality Coffee 2023) yatakayofanyika jijini Tokyo tarehe 27 -29 Septemba 202. Bodi ya Kahawa Tanzania inaratibu ushiriki wa Tanzania kama ilivyokuwa mwaka jana. Maonesho haya hutoa fursa muhimu sana kwa wadau wa kahawa duniani kukutana na kubadilishana taarifa muhimu, uzoefu na maarifa kuhusu kahawa."
 
Back
Top Bottom