Elections 2010 SFO yakanusha Taarifa ya PCCB! Suala la Chenge bado halijaisha!

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,107
2,000
PressRelease-BHC.jpg


Wakati PCCB wamemshafisha Chenge kwenye kadhia ya Radar kuwa suala hilo limekwisha na Chenge hahusiki, SFO wenyewe wamekanusha kuisha kwa suala hilo na kueleza litatinga mahakama kuu ya Uingereza mwishoni mwa mwezi huu na huko ndiko suala litaamuliwa kama limekwisha au laa.

Taarifa kutoka ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari, umeweka wazi kila kitu kuwa kadhia hiyo bado haijakwisha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kitu ambacho kimekubaliwa kuwa kimekwisha, ni uchunguzi dhidi ya kadhia hiyo ndio umemalizika baada ya BAE kukubali wamegawa rushwa, ila badala ya kuwataja waliowagawia, wamekubali kulipa faini ambayo serikali ya Tanzania, itarudishiwa lile fungu lililokamuliwa ili wakubwa wale.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ubalozini, Mahakama ya Uingereza, inaweza kuamua kuwa hawakubali faini hiyo kulipwa, bali wakalazimisha lazima majina ya walarushwa yatajwe badala na kuzibwa midomo kwa faini na fidia, na kama itakuwa ndio hivyo, tuhuma za Chenge kwenye kadhia hiyo zinabaki kuwa bado ziko pale pale?.

Kama taarifa hii ya ubalozi wa Uingereza ni ya kweli, crdedibility ya PCCB yetu kwenye kuwasafisha mafisadi iko wapi?
 

MILKYWAY GALAXY

JF-Expert Member
Dec 12, 2008
205
195
Kama taarifa hii ya ubalozi wa Uingereza ni ya kweli, crdedibility ya PCCB yetu kwenye kuwasafisha mafisadi iko wapi?.

Ina maana hii taarifa si ya kweli?

Ndugu naomba ufafanuzi tafadhali
 

MONTESQUIEU

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
847
0
Wakati pccb wamemshafisha chenge kwenye kadhia ya radar kuwa suala hilo limekwisha na chenge hahusiki, sfo wenyewe wamekanusha kuisha kwa suala hilo na kueleza litatinga mahakama kuu ya uingereza mwishoni mwa mwezi huu na huko ndiko suala litaamuliwa kama limekwisha au laa.

Taarifa kutoka ubalozi wa uingereza kwa vyombo vya habari, umeweka wazi kila kitu kuwa kadhia hiyo bado haijakwisha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kitu ambacho kimekubaliwa kuwa kimekwisha, ni uchunguzi dhidi ya kadhia hiyo ndio umemalizika baada ya bae kukubali wamegawa rushwa, ila badala ya kuwataja waliowagawia, wamekubali kulipa faini ambayo serikali ya tanzania, itarudishiwa lile fungu lililokamuliwa ili wakubwa wale.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ubalozini, mahakama ya uingereza, inaweza kuamua kuwa hawakubali faini hiyo kulipwa, bali wakalazimisha lazima majina ya walarushwa yatajwe badala na kuzibwa midomo kwa faini na fidia, na kama itakuwa ndio hivyo, tuhuma za chenge kwenye kadhia hiyo zinabaki kuwa bado ziko pale pale?.

Kama taarifa hii ya ubalozi wa uingereza ni ya kweli, crdedibility ya pccb yetu kwenye kuwasafisha mafisadi iko wapi?.

chenge vidole vya nini?
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,212
2,000
The British Government is aware of a statement made by the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) on 8 November 2010. At this stage the case relating to BAe and its dealings in Tanzania is yet to go to court in the UK. It is therefore not possible to draw conclusions either way relating to those who were interviewed in connection with the case.
Sasa hawa Mafisadi wa TAKUKUNGURU wamepata wapi kuwa SFO wameona kuwa madai dhidi ya Chenge hayana uthibitisho?....
Pccb yetu wamekalia tu zile nafasi, lakini hawana wajuacho zaidi ya kufuatilia rushwa za buku 5 za uchaguzi!
Shame on them!
 

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,468
2,000
Ni lini PCCB ilikuwa credible, Richmond ilitosha kuonyesha kwamba they are not credible, not serious and absolutely reckless!
 

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
1,250
Hata kama uingereza wakikubali faini tha fact kwamba wanakubali walitoa rushwa na ndg chenge amekutwa na mabikioni hayo pamoja na dr rashid ambazo ni sehemu ya mkopo kwa tanzania mabao bado tunahangaika watanzania wote kuulipa ; hilo kwetu haliwezi kuisha.
 

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
1,195
Tangu niliposoma ile statement ya PCCB nilishangaa sana kwa sababu najua ile kesi haijapelekwa kwa judge kule UK kwa ajili ya kuamua kuhusu makubaliano ya SFO na BAE Systems. What if akikataa? kwa hiyo PCCB hawakuwa na sababu ya kumsafisha Chenge wakati huu kwani ngoma bado ni mbichi. Huu ni ufisadi kwa upande wa PCCB. Tunasubiri statement yao tena.
 

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,697
1,250
Chenge hata kama atakuwa cleared bado anatakiwa awaambie Watanzania:

1. $ 1.5 M alizitoa wapi?
2. Consultancy Fees na Personal saving anf Family Heritage anazodai ndo zimempatia hizo pesa ni zipi?
3. Kwa nini alitumia madaraka yake vibaya kuwaweka watanzania katika risk kwa manufaa yake tofauti na matarajio
4. Ameongea nini na PCCB wamemsafisha wakati Mdumange ndo kwanza unaaanza?
 

nginda

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
744
0
pccb walifanya uchunguzi wao ******. Hosea nae mtuhumiwa kisha anamlinda mtuhumiwa. Hii yote ni kesi ya nyani na ngedere.
 

GY

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,280
1,170
''''Taarifa kutoka ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari, umeweka wazi kila kitu kuwa kadhia hiyo bado haijakwisha.''''

Noted with thanks, tusubiri blablaa nyingine

Thisi kantry bwana!
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
2,000
The British Government is aware of a statement made by the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) on 8 November 2010. At this stage the case relating to BAe and its dealings in Tanzania is yet to go to court in the UK. It is therefore not possible to draw conclusions either way relating to those who were interviewed in connection with the case.

On 5 February 2010, the Serious Fraud Office (SFO) announced that it had reached a settlement with BAe following an investigation into a defence contract with the Government of Tanzania.

Regarding Tanzania, BAe has admitted that it failed to keep reasonably accurate accounting records in relation to its activities here. BAe has said it will plead guilty to the aforementioned offence, and that it will pay a sum of £30 million by way of a penalty and also for reparation to Tanzania. A hearing in the crown court will determine the amount of the financial order (fine) with the balance to be made available as an ex-gratia payment to the people of Tanzania.

Hapo ndipo kwenye goli la kisigino la Chenge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom