Serikali za miji zingekataza kufuga maeneo ya miji na majiji.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,239
12,756
Nimeona mdau mmoja analalamika kero ya jirani yake anayefuga ng'ombe. Kwa nini serikali za miji hazikatazi kufuga maeneo ya mjini, badala yake wanakataza kulima mahindi na alizeti, vitu visivyo na madhara yoyote kwa mji? Huwa tunawaza kinyume nyume sana. Binadamu alianza kusumbuliwa sana na magonjwa baada ya kuanza kufuga, magonjwa yetu mengi yanatoka kwa wanyama. Mfano mzuri ni mafua ambayo kiasili ni magonjwa ya ndege. Kufuga wanyama kwenye maeneo ya makazi ni kero kubwa, ukiacha magonjwa bado kuna kero ya harufu na uchafuzi mwingine wa mazingira.

Mtu akitaka kufuga akanunue eneo nje ya mji/jiji. Si sawa wala ustaarabu kufuga kwenye makazi ya watu.
 
Lakini mkuu kuna ile hali hutokea; nimenunua eneo mfano mapinga kwa ajili ya kufanya shughuli za ufugaji baadae mji unakua mpaka najikuta nipo katikati ya makazi ya watu. Hapo nini kifanyike?
Kama upo kijijini sheria zinakuruhusu, waliokufuata ndiyo wenye matatizo. Wakuvumilie. Lakini sehemu ikishapanda hadhi kutoka kijiji kuwa mtaa maana yake na mambo mengi na shughuli zake za uchumi zinabadilika. Ndiyo maana raia tunatakiwa kuwa makini sana kwenye mabadiliko ya hadhi ya maeneo.
 
Kuna kanga pia, wanaweza kupiga kelele za hatari usiku.
Mila na desturi za kiswahili zimevuka mipaka! Baada ya kuibuka kizazi ambacho hakitambikii mizimu! Mizimu imejiongeza na kutaka kukaa ndani ya kizazi kupitia mifugo! Hii mifugo hasahasa kuku ambao watu wanaishi nao ni nyumba za mizimu na ndo chanzo cha umasikini na migogoro ya ndoa, umasiki, kukwama kimaisha! Kama unataka kufuga, fuga kibiashara sio kufuga unaishi na wanyama kazi kuchafua mazingira kwa vinyesi na kelele na kukuingizia gharama za kujengea banda kumbe unajenga "nyaruju". Ua! Fukuzia mbali hao wanyama! Eti ni kwasababu za kitoweo! Faida za kitoweo ni ndogo kuliko hasara za kuwatunza! Akili kumkichwa!
 
Kama upo kijijini sheria zinakuruhusu, waliokufuata ndiyo wenye matatizo. Wakuvumilie. Lakini sehemu ikishapanda hadhi kutoka kijiji kuwa mtaa maana yake na mambo mengi na shughuli zake za uchumi zinabadilika. Ndiyo maana raia tunatakiwa kuwa makini sana kwenye mabadiliko ya hadhi ya maeneo.
Binafsi naona tutawalaumu hao wanao fuga lakini sheria zikisimamia kucha mwanzo mwisho wengi wetu tutashindwa kuishi.

Sera ya makazi hakuna njia itatimia kama kipato cha mtu mmoja mmoja hakitaimarika
 
Lakini mkuu kuna ile hali hutokea; nimenunua eneo mfano mapinga kwa ajili ya kufanya shughuli za ufugaji baadae mji unakua mpaka najikuta nipo katikati ya makazi ya watu. Hapo nini kifanyike?
Unafanya kama jamaa zangu wazaramo, unauza na kusogea mbali ambako utapata eneo kubwa zaidi.
 
Nimeona mdau mmoja analalamika kero ya jirani yake anayefuga ng'ombe. Kwa nini serikali za miji hazikatazi kufuga maeneo ya mjini, badala yake wanakataza kulima mahindi na alizeti, vitu visivyo na madhara yoyote kwa mji? Huwa tunawaza kinyume nyume sana. Binadamu alianza kusumbuliwa sana na magonjwa baada ya kuanza kufuga, magonjwa yetu mengi yanatoka kwa wanyama. Mfano mzuri ni mafua ambayo kiasili ni magonjwa ya ndege. Kufuga wanyama kwenye maeneo ya makazi ni kero kubwa, ukiacha magonjwa bado kuna kero ya harufu na uchafuzi mwingine wa mazingira.

Mtu akitaka kufuga akanunue eneo nje ya mji/jiji. Si sawa wala ustaarabu kufuga kwenye makazi ya watu.
Wafugaji wameufuata mji au ni mji unawasengeasengea wafugaji ??
 
Binafsi naona tutawalaumu hao wanao fuga lakini sheria zikisimamia kucha mwanzo mwisho wengi wetu tutashindwa kuishi.

Sera ya makazi hakuna njia itatimia kama kipato cha mtu mmoja mmoja hakitaimarika
Ni kweli, maana maskini makazi yake ndiyo kazini kwake. Lakini kuna vitu tunaweza kuvikataa, kama ufugaji.
 
Back
Top Bottom