Mkuu ni kweli ni issue ya ustaarabu tu, wala haina haja ya kulumbana. Kwanza tungeambiwa mahakama za kawaida zina upungufu gani mpaka zionekane kushindwa ku-accomodate mambo ya waislamu au kama zinashughulikia mambo ya wakristo na wapagani kwa haki na kupuuza ya waislamu, tuambiwe ni mahakama gani itakuwa na final say, ya kadhi au ya mahakama kuu. Na kama hiyo mahakama itashughulikia mambo ya ndoa na mmoja kati ya wanandoa ni wa dini nyingine issue hii itashughulikiwa vipi.
Na kama mahakama za sasa zina upungufu (hazitendi haki kwa watanzania-waislamu na wakristo) kwa nini tusiombe reform kwa mahakama ili kuwe na haki kwa watanzania wote na si waislamu tu?
Ni kwanini sehemu moja ya watanzania iwe subjected kwenye two legal systmes, wengine kwenye legal system moja?
Mkuu unaweza kuona kuwa kuna maswali mengi kuliko majibu kuhusu idea nzima ya mahakama ya "kadhi". Hata mipaka yake bado haijulikani, maana Tanzania hakuna watu wanaoandikishwa kuwa waislamu, na ndoa kati ya dini mbalimbali hapa kwetu ni kawaida, tofauti sana na nchi zenye udini na ukabila. Kama wewe mkristo itakuwa ajabu sana mtu unaambiwa mkeo au mumeo mwislamu anaenda kuhukumiwa kwenye mahakama ya kadhi.
Inaonekana kama kuna watu waliitumia kwa sababu za kisiasa, na sio kuboresha maisha ya waislamu. MImi kwa mamoni yangu Mahakama za sasa zina matatizo makubwa, si kwa waislamu tu. Hata wapagani na wakristo nao wana matatizo nazo, for the sake of umoja wetu na utanzania wetu ni bora wote tupambane na mahakma hizi kuliko kuleta za kadhi.