Ndugu, you are missing the whole point. Tukianza kufikiria kwa misingi ya vikundi hatutafika popote. The issue ni kuwa public fund ifanye kazi ya kunufaisha kila mtu kwenye jamii - regardless who or what he happens to be. Assuming wewe ni Muislamu, uliamua kuwa hivyo au ni "social accident"? Hata kama uliamua, wote walio waislamu waliamua kuwa waislamu au walijikuta wakiwa waislamu (kwa kuzaliwa katika familia ya waislamu)?
Wazo lako in zuri japo nadhani kwa mazingira ya sasa ya nchi yetu si practical. Kuna ngumi kila kukicha kwenye vikundi vya kijamii (makanisa, misikiti, klabu za michezo n.k) kugombea rasilimali kidogo zilizopo. Tukianza kuwapa fungu toka serikalini unadhani itakuwaje? Kanisa gani lipewe hiyo ruzuku, Wakatoliki? Walutheri, Waanglikana, Wapentekoste n.k. watakaa kimya?
Hiyo ruzuku wapewe BAKWATA au jumuiya gani ya Kiislamu? Taasisi za kidini hupewa misaada na serikali tangu zamani (Chuo cha TANESCO Morogoro kwa mfano), hakujawahi kuwa na malalamiko. Ila hili la ku-formalize matumizi ya kodi kwa ajili ya kundi moja kwenye jamii litatupeleka pabaya.
Nadhani umeelewa hoja yangu.