Serikali Yashindwa Kulipa Mishahara ya December

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
0
Huwezi kuamini wafanyakazi wa serikali hadi leo tarehe 2 hawajalipwa mishahara. Nimeombwa na rafiki zangu wawili kuwakopesha kwa vile mishahara haijatoka nikazungumza na jamaa yangu wa hazina anasema mishahara bado waliolipwa ni wajeshi na taasisi baadhi zimelipa kupitia OC. Huu ndio ukweli , kama serikali inashindwa kulipa mishahara kwa wakati tunarudi kama wakati wa Mwinyi mishahara tarehe 7. Kaserikali dhaifu! Vyama vya wafanyakazi vipo wapi au kazi yao kukusanya ada tu?

Watu wanaingia tarehe 6 kesho bila mishahara sijui serikali ina tatizo gani? Effect yake ni kuuwa sekta ya umma maana kama mtu huwezi kupata mshahara kwa wakati ulee familia yako utaijali kazi? je rushwa itaisha wakati hulipi mishahara?
 
Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,489
1,250
Hoja ni dhaifu sana kwani haina utafiti wa kutosha !!!!
 
masatujr1985

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,984
2,000
Mbugi unataka ushahidi gani? Mie sijalipwa na nianafanya Shirika la Umma na Leo Ni trh 2
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,875
2,000
Mkuu nimi ni mmoja wa wahanga wa kutolipwa mshahara.

Nilipost hii habari hapa jukwaani kuna watu wakaniona mimi mzushi.Bora na wewe umesema.

Jamani waandishi wa habari mtusaidie katika hili!
 
ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
0
Hoja ni dhaifu sana kwani haina utafiti wa kutosha !!!!
Una maanisha nini? Nitajie ni wafanyakazi gani wa serikali wamelipwa mishahara hadi leo tarehe 2. Tuanze na vyuo vya elimu ya juu, ukiondoa IFM ambayo imelipa kutoka OC nitajie chuo kingine kilicholipa mishahara. Tuje walimu wa msingi na sekondari, wafanyakazi wa mawizara, nitajie ni akina nani wamelipwa mishahara
 
ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
0
Hoja ni dhaifu sana kwani haina utafiti wa kutosha !!!!
Wewe ndie ungepaswa kuthibitisha kuwa wafanyakazi wa serikali wamelipwa maana wafanyakazi wenyewe wanasema hawajalipwa wewe unasemaje ni hoja dhaifu?
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,875
2,000
Hoja ni dhaifu sana kwani haina utafiti wa kutosha !!!!

Watu kama nyie mnakera sana.Huu ni ukweli kuwa mpaka leo tarehe 02/012014 hatujalipwa mshahara wa mwezi December na serikali iko kimya kabisa.

Mpaka habari hizi ziende kwenye media ndio serikali itashituka na kuona aibu.
 
suleym

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,923
2,000
Watu kama nyie mnakera sana.Huu ni ukweli kuwa mpaka leo tarehe 02/012014 hatujalipwa mshahara wa mwezi December na serikali iko kimya kabisa.

Mpaka habari hizi ziende kwenye media ndio serikali itashituka na kuona aibu.

pole mkuu achana nae huyo yupo hapa kuspin mada, kiukweli serikali iko taabani dhoofu hali!
 
Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
2,000
Huwezi kuamini wafanyakazi wa serikali hadi leo tarehe 2 hawajalipwa mishahara. Nimeombwa na rafiki zangu wawili kuwakopesha kwa vile mishahara haijatoka nikazungumza na jamaa yangu wa hazina anasema mishahara bado waliolipwa ni wajeshi na taasisi baadhi zimelipa kupitia OC. Huu ndio ukweli , kama serikali inashindwa kulipa mishahara kwa wakati tunarudi kama wakati wa Mwinyi mishahara tarehe 7. Kaserikali dhaifu! Vyama vya wafanyakazi vipo wapi au kazi yao kukusanya ada tu?

Wanaostaili kulipwa kwa wakati ni Walimu, Polisi na Manesi maana hao hawana semina na vikao feki vya posho. The rest hata mkikosa sawa
 
1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,041
1,250
Hela na mafweza yoote yameishia kwenye safari za ki-Vasco da Gama. Anapoenda kutafuta vitunguu saumu vya kupikia pilau. Kwani hujamskia tarehe 31 Desemba 2013? Kasema safari zake zimefanikiwa mno maana tumepata "mdalasini, vitunguu maji, iliki, nyanya chungu, nk." kwa wingi kabisa kutokana na safari hizo utafikiri hatuna hivyo viungo hadi tugeuke matonya wa dunia nzima. Tume kuwa kama mwanamke mbea kila uchao ni kiguu na njia kwenye majumba ya watu.,
 
kasinge

JF-Expert Member
May 22, 2011
1,259
1,500
Mgimwa kafa kwa stress. Wewe kama waziri wa fedha ambaye uko dedicated, lazima utakufa kwa stress kwa kaserikali dhaifu kama haka. Dah, RIP.
 
Bob G

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
2,352
1,500
Utasikia makusanyo ya kodi mwezi huu tumevuka malengo, huku watu wanalia hawajalipwa mshahara, usanii huu uwe na mwisho. Lkn na ninyi wafanyakazi mlimpa kura za nini na yeye alisema hataki kura zenu! wezi wakubwa ninyi mnaikumbatia ccm kwa kuruhusu muwaibie WADANGANYIKA.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom