Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,115
- 35,121
Mficha maradhi kifo kitamuumbua, yawahi hayawi sasa yamekuwa, ukweli halisi umeanza kujionyesha huko Kenya, hali ya maisha ni mbaya mnoo, vijijini ukame unawaua, mijijini maisha yanawanyonga na sasa Serikali imeshindwa kulipa hadi mishahara watumishi wake. Kenya kumechoka na kuchakaa balaa.
Rais wa Kenya (William Ruto) amekiri wazi wazi kuwa hali ya kiuchumi kwa wakenya na serikali yao ni tete mnoo, huku akisema serikali yake imezidiwa na madeni yaliyotokana na kukopa kiholela ili kugharamia miradi iliyojaa ufisadi mkubwa kiasi cha kushindwa kuwa na pesa za kulipa mishahara.
Sio hayo tu, zipo sehemu kadhaa (kaunti nyingi) katika Kenya ambapo mbali na kutokuweza kupokea pesa za kulipa mishahara kwa miezi kadhaa pia zimeshindwa kupokea pesa kwa ajili ya kugharamia utoaji wa huduma za Afya na elimu kutoka serikalini. Kwa lugha rahisi na fupi sana, Kenya kwa sasa ni taifa rasmi la kimaskini zaidi katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.
Kwa hali ilivyo sasa ni dhihaka kubwa sana kutaka kuilinganisha Kenya na Tanzania, kwa kuwa Tanzania mbali na kuwa kihistoria ni nchi yenye mizizi ya kimaskini (ujamaa!) na tangu kumfukuza mkoloni imekuwa chini ya CCM (chama kinachoukumbatia umaskini) bado haijaweza kupitia vipindi vya umaskini na kufirisika kwa serikali kiasi cha kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wake. Kwa sasa kimaskini Kenya imepitiliza.
Kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu kidogo kuna kila dalili kuwa huenda Kenya ikaweka rehani bandari ya Mombasa, viwanja vya ndege na mtandao wa reli ya SGR ili kulipa madeni au kuendelea kukopesheka.