Serikali yasaini mikataba ya ujenzi wa barabara unganishi katika Daraja la Sibiti yenye urefu wa Kilometa 24.83

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Serikali kupitia TANROADS imesaini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara unganishi katika Daraja la Sibiti yenye urefu wa Kilometa 24.83 kwa kiwango cha lami (mradi unatekelezwa Wilaya ya Mkalama) na mkataba wa ujenzi wa barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa sehemu ya Noranga – Doroto yenye urefu wa kilometa 6 na Itigi – Mkiwa yenye urefu wa kilometa 25.569 kwa kiwango cha lami, Mradi ambao utatekelezwa katika Wilaya ya Itigi.
Snapinsta.app_346889800_627169625970300_6366266744903489538_n_1080.jpg

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa katika hafla ya utiaji saini mikataba ya miradi wa ujenzi wa barabara za maingilio ya Daraja la Sibiti (km25) na Noranga - Doroto (km6) pamoja na Itigi hadi Mkiwa (km 25) wilayani Itigi, Mkoani Singida.

Picha (2).jpg

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji Saini wa mikataba hiyo miwili leo Mei 14- 2023 Wilayani Itigi Mkoani Siginda, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof: Makame Mbarawa amesema:

“Lengo la miradi inayojengwa kwa kutumia fedha za ndani kwa 100% ni kuwaondolea wananchi kero ya usafiri wa barabarani na kuboresha mtandao wa barabara na madaraja ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji hivyo kukuza uchumi wa Nchi.”
Picha (3).jpg

Amesema Serikali imelenga kuendelea na kukamilisha mkakati wake wa kuunganisha mikoa kwa barabara za lami ambapo kwa miradi ambayo mikataba imesainiwa leo.

Amesema "Tunaelekea kuiunganisha Singida na Mbeya na kwa upande mwingine mikoa ya Singida na Simiyu na kwamba Ujenzi wa barabara unganishi katika Daraja la Sibiti utakapokamilika pia utasaidia kuondoa adha ya usafirishaji wa mizigo na abiria na kuongeza usalama kwa wote watakaotumia daraja hilo pamoja na kukuza biashara mbalimbali."
Picha (1).jpg

"Barabara unganishi katika daraja hili zitasaidia pia kuunganisha na kuboresha hali ya usafiri wa wananchi wetu na usafirishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na mazao ya misitu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Singida pamoja na mikoa jirani ya Manyara, Simiyu, Shinyanga, Arusha, Dodoma na Tabora kwenda maeneo mbalimbali ya nchi yetu," ameongeza Waziri Prof: Mbarawa.

Ameongeza Serikali imekamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara kutoka Mbeya hadi Makongolosi (km 111), hivyo ujenzi wa Barabara ya Itigi hadi Mkiwa ambayo ni sehemu ya barabara inayotoka Mbeya kupitia Makongolosi – Rungwa – Itigi hadi Mkiwa utapunguza muda na gharama za safari kwa Wananchi na bidhaa mbalimbali kutoka mikoa ya kanda ya ziwa kwenda katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Katavi na Rukwa pamoja na nchi jirani ya Zambia.

Snapinsta.app_346672513_151372137766790_2841004935696288454_n_1080.jpg

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila

Mativila: Barabara hizo za maingilio ni kiungo muhimu kati ya Wilaya ya Mkalama
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa barabara za Maingilio ya Daraja la Shibiti na barabara ya Noranga hadi Doroto pamoja na Itigi hadi Mkiwa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng: Rogatus Mativila amesema barabara hizo za maingilio ni kiungo muhimu kati ya wilaya ya Mkalama na wilaya zingine katika mkoa wa Singida, zinaungana na mtandao wa barabara muhimu za mkoa wa Singida ambazo zinaunganisha moja kwa moja mkoa huo na mikoa ya Simiyu, Manyara na hivyo kuunganisha na mikoa mingine jirani na Singida ya Shinyanga, Arusha, Tabora na Dodoma.

Amesema kuwa TANROADS ilisaini mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd. (CHICO) kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa, Sehemu ya kutoka Noranga hadi Itigi (Mlongoji) yenye urefu wa Km 25 kwa kiwango cha lami kwa Gharama ya Shilingi bilioni 29.77, kwa sasa Mkandarasi yupo katika eneo la kazi na Ujenzi wa mradi huo unaendelea vizuri, Ujenzi umefikia 29%.

Eng: Mativila ameongeza kuwa Ujenzi wa barabara sehemu ya Noranga hadi Doroto (Km 6) na Itigi hadi Mkiwa (km 25.569) kwa kiwango cha lami unaohusisha jumla ya KM 31.569, unajengwa pia na Mkandarasi China Henan International Cooperation Group Co. Ltd. (CHICO) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 39.988 kwa kipindi cha miezi 19, ambapo barabara hizo za maingilio zitakapokamilika zitaondoa adha ya usafiri katika eneo korofi karibu na Daraja la Sibiti na hivyo kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa bidhaa pamoja na uwezeshaji wa shughuli za kijamii kwa ujumla.
 
Awamu ya 6 itajenga barabara na miundombinu mingi ya kugusa wengi kuliko awamu ya zimwi
 
Sawa Sawa
Mzilankende Aliacha Daraja Tayari
Meatu, Maswa, Mkalama Jiandaeni
Kutoka Mara Sasa Itakuwa Saa Tano Asubuhi Tupo Singida
 
Mzingatie na ubora.maana barabara nyingi kwa sasa mnajenga chini ya kiwango.wananchi hatutaki kodi zetu mzitumie kwa vitu ambavyo ni chini ya kiwango
 
Ya Makongolosi - Rungwa bado hawajaanza.
Barabara hiyo imekuwa ikiimbwa mara Kwa Mara (na viongozi Wakubwa kama vile Kasimu Majaliwa) kwamba "tuko mbioni kuanza Ujenzi", lakini muda unazidi kwenda hakuna chochote kinachofanyika.
 
Serikali kupitia TANROADS imesaini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara unganishi katika Daraja la Sibiti yenye urefu wa Kilometa 24.83 kwa kiwango cha lami (mradi unatekelezwa Wilaya ya Mkalama) na mkataba wa ujenzi wa barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa sehemu ya Noranga – Doroto yenye urefu wa kilometa 6 na Itigi – Mkiwa yenye urefu wa kilometa 25.569 kwa kiwango cha lami, Mradi ambao utatekelezwa katika Wilaya ya Itigi.
View attachment 2622083
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa katika hafla ya utiaji saini mikataba ya miradi wa ujenzi wa barabara za maingilio ya Daraja la Sibiti (km25) na Noranga - Doroto (km6) pamoja na Itigi hadi Mkiwa (km 25) wilayani Itigi, Mkoani Singida.

View attachment 2622079
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji Saini wa mikataba hiyo miwili leo Mei 14- 2023 Wilayani Itigi Mkoani Siginda, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof: Makame Mbarawa amesema:

“Lengo la miradi inayojengwa kwa kutumia fedha za ndani kwa 100% ni kuwaondolea wananchi kero ya usafiri wa barabarani na kuboresha mtandao wa barabara na madaraja ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji hivyo kukuza uchumi wa Nchi.”
View attachment 2622080
Amesema Serikali imelenga kuendelea na kukamilisha mkakati wake wa kuunganisha mikoa kwa barabara za lami ambapo kwa miradi ambayo mikataba imesainiwa leo.

Amesema "Tunaelekea kuiunganisha Singida na Mbeya na kwa upande mwingine mikoa ya Singida na Simiyu na kwamba Ujenzi wa barabara unganishi katika Daraja la Sibiti utakapokamilika pia utasaidia kuondoa adha ya usafirishaji wa mizigo na abiria na kuongeza usalama kwa wote watakaotumia daraja hilo pamoja na kukuza biashara mbalimbali."
View attachment 2622081
"Barabara unganishi katika daraja hili zitasaidia pia kuunganisha na kuboresha hali ya usafiri wa wananchi wetu na usafirishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na mazao ya misitu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Singida pamoja na mikoa jirani ya Manyara, Simiyu, Shinyanga, Arusha, Dodoma na Tabora kwenda maeneo mbalimbali ya nchi yetu," ameongeza Waziri Prof: Mbarawa.

Ameongeza Serikali imekamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara kutoka Mbeya hadi Makongolosi (km 111), hivyo ujenzi wa Barabara ya Itigi hadi Mkiwa ambayo ni sehemu ya barabara inayotoka Mbeya kupitia Makongolosi – Rungwa – Itigi hadi Mkiwa utapunguza muda na gharama za safari kwa Wananchi na bidhaa mbalimbali kutoka mikoa ya kanda ya ziwa kwenda katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Katavi na Rukwa pamoja na nchi jirani ya Zambia.

View attachment 2622085
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila

Mativila: Barabara hizo za maingilio ni kiungo muhimu kati ya Wilaya ya Mkalama
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa barabara za Maingilio ya Daraja la Shibiti na barabara ya Noranga hadi Doroto pamoja na Itigi hadi Mkiwa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng: Rogatus Mativila amesema barabara hizo za maingilio ni kiungo muhimu kati ya wilaya ya Mkalama na wilaya zingine katika mkoa wa Singida, zinaungana na mtandao wa barabara muhimu za mkoa wa Singida ambazo zinaunganisha moja kwa moja mkoa huo na mikoa ya Simiyu, Manyara na hivyo kuunganisha na mikoa mingine jirani na Singida ya Shinyanga, Arusha, Tabora na Dodoma.

Amesema kuwa TANROADS ilisaini mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd. (CHICO) kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa, Sehemu ya kutoka Noranga hadi Itigi (Mlongoji) yenye urefu wa Km 25 kwa kiwango cha lami kwa Gharama ya Shilingi bilioni 29.77, kwa sasa Mkandarasi yupo katika eneo la kazi na Ujenzi wa mradi huo unaendelea vizuri, Ujenzi umefikia 29%.

Eng: Mativila ameongeza kuwa Ujenzi wa barabara sehemu ya Noranga hadi Doroto (Km 6) na Itigi hadi Mkiwa (km 25.569) kwa kiwango cha lami unaohusisha jumla ya KM 31.569, unajengwa pia na Mkandarasi China Henan International Cooperation Group Co. Ltd. (CHICO) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 39.988 kwa kipindi cha miezi 19, ambapo barabara hizo za maingilio zitakapokamilika zitaondoa adha ya usafiri katika eneo korofi karibu na Daraja la Sibiti na hivyo kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa bidhaa pamoja na uwezeshaji wa shughuli za kijamii kwa ujumla.
sasa kwanini i liishie wilaya ya mkalama tu, huo ni ubaguzi hiyo bara bara inatakiwa iende hadi wilaya ya bariadi na maswa yaanii iunge mkoa wa simiyu na singida
 
Hii bajeti ya 2023/24 ndo itajumuisha hiyo barabara ya Sibiti-Mwanhuzi (Meatu)-Lalago-Binza (Maswa) na Ile ya Kolandoto-Lalago-Mwanhuzi zipo kwenye bajeti hizo tuwe na subra tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom