Mawasiliano ya Barabara Katika Daraja la Somanga Yarejea

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MAWASILIANO YA BARABARA KATIKA DARAJA LA SOMANGA YAREJEA

Mawasiliano ya barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara yarejea katika eneo la Somangafungu Mkoani Lindi kutokana na daraja la Somanga linalounganisha barabara hiyo kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa kwa saa kadhaa.

Akitoa taarifa, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, Eng. Emil Nzengo amesema tayari magari ya abiria na mizigo na vyombo vingine vya usafiri vimeruhusiwa na kuaza kupita upande mmoja katika Daraja hilo ambalo lilikuwa halipitiki tangu usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua zinaoendelea kunyesha Mkoani humo.

“Tumekamilisha kazi awamu ya kwanza, wananchi na magari wameruhusiwa kuanza kupita. Tunawashukuru Wananchi kwa uvumilivu na tunaomba waendelee kuiamini Serikali ipo kazini kwa ajlili yao”, amesema Eng. Nzengo.

Awali, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alieleza kuwa jitihada kubwa zinaendelea za kurudisha mawasiliano ya barabara eneo la Somangafungu na kuagiza timu ya Wataalam kutoka TANROADS kuhakikisha hadi kufikia mchana leo March 25, 2024 mawasiliano yawe yamerejeshwa na magari yaanze kupita katika daraja hilo
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-03-25 at 13.11.44.mp4
    7.8 MB
Back
Top Bottom