Serikali yaridhishwa na utekelezaji mradi mkubwa wa maji Arusha

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1574762053913.png


SERIKALI imeonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji uliogharimu shilingi bilioni 520 unaotekelezwa katika halmashauri ya jiji la Arusha kwa lengo la kuhudumia wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Maji, Nadhifa Kemikimba baada ya kukagua miundombinu ya mradi huo huku akibainisha nia ya serikali ni kuona ifikapo mwaka 2010 upatikanaji wa huduma za maji mijini inafika asilimia 95 huku wananchi wa vijijini wanapata maji kwa asilimia 85.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa AUWASA, Mhandisi Justine Mwangijomba amesema mradi huo umefikia hatua ya kusafisha mtandao wa mabomba yanayopeleka maji kwenye matanki na kuweka dawa kwenye maji tayari kwa ajili ya matumizi ya wananchi. "Kama tulivyoona tumepita katika matanki yetu ya maji natumeona tanki moja la lita milioni kumi tumeanza kuweka maji kwani ujenzi wa tanki hilo umekamilika hivyo muda sio mrefu wananchi watapata ongezeko la maji na tutaanza kuwapa wale wenye shida ya maji kama muriet na olasiti" amesema Mwangijomba.

Akiongelea mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema kuwa kuna ujenzi wa makao makuu ya mamlaka ya Maji safi na Maji taka ambao ulikuwa unasuasua lakini baada ya ofisi yake kwa kushirikiana na msimamizi wa mkandarasi kufatilia kwa makini ujenzi huo umeanza kwenda vizuri

1574762102606.png
 
Back
Top Bottom