Serikali yamtorosha mwanafunzi kwenda Marekani (USA); mzazi aomba Rais Samia amsaidie

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,861
18,280
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Ukiisikiliza hii stori kwa umakini bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, utagundua kuwa serikali ndiyo imehusika katika kutoroka kwa mwanafunzi huyu 100%.


Kwa maana nyingine naweza kusema serikali ndiyo imemtorosha baada ya kupuuzia kilio cha wadau wa elimu kuhusu kupunguza idadi ya masomo ya kipuuzi, hivyo kupelekea kuwarundikia wanafunzi masomo mengi yasiyokuwa na maana na kuwafanya wachukie masomo na kisha kuchukua maamuzi magumu yanayowaacha wazazi na jamii vinywa wazi.

Kama serikali ingesikiliza kilio cha wadau wa elimu na kupunguza idadi ya masomo, nina uhakika huyu mwanafunzi asingechora ramani na kutengeneza mpangokazi wa kutoroka shuleni. Serikali inapaswa kulaumiwa moja kwa moja kwa tukio hili la kusikitisha na kuhudhunisha.
 
Back
Top Bottom