#COVID19 Serikali yakusudia kuchanja asilimia 60 ya Watanzania Chanjo ya Coronavirus

Dar es Salaam. Baada ya chanjo ya Covid-19 kuwasili nchini Serikali imejiweka lengo la kuwachanja asilimia 60 ya Watanzania wote.
Waziri wa Afya, Dk Doroth Gwajima amesema awamu ya kwanza ya chanzo hiyo itatolewa kwa makundi ya mstari wa mbele ambayo yatawekwa wazi siku ya kesho.

Amesema kwa kuanzia watachanjwa watu walio kwenye mstari wa mbele lakini lengo ni kuwafikia watanzania wote watakaohitaji.

“Serikali ya awamu ya sita imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania kwa hiari yake bila malipo atapata chanjo.

“Kuhusu makundi yatakayoanza tutaweka wazi kesho ni akina nani na utaratibu upi utatumika, zitapatikana wapi haya yote tutayaeleza,” amesema Dk Gwajima.

Mwananchi
I bet haina uwezo huo wa kuchanja asilimia 40 katu katu i bet

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Huiogopi Corona unaiogopa chanjo?! haya maajabu yako Tz pekee.
Tanzania peke yake ?

Mpaka leo July 23, 2021, nchini Marekani 56% ya Wananchi wamepokea chanjo...

Nusu iliyobaki wamekataa!

Hata sisi tunaweza kuigomea!
 
Habari za jion wana JF poleni na mihangaiko ya kila siku na mapambano haya ya gonjwa hili hatari la COVID19 chini ya third wave
.
.
.
Napenda kuchukua fursa hii kuipongeza serikali kwa kukubali msaada wa chanjo kutoka taiifa kubwa na linaloogopeka kwa nguvu za kijeshi duniani kuisaidia nchi masikini kama yetu ni jambo la kushukuru Tajiri anapomkumbuka maskini ni mara chache sana kutokea
.
.
.
Kwakua chanjo iliyotolewa ni chache na hawajasema kama wataongeza na idadi ya watanzania ni zaidi ya million sitini na kitu ningependa kwanza kusikia kauli ya raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh samia suluhu hassani juu ya ubora na ufanisi wa hii chanjo na pia atuondolee hofu na mashaka kwakua matamko yamekua mengi ya kupinga hii chanjo na kwakuzingatia hilo ningeomba awe wa kwanza kuchomwa hadharani ili kujenga uaminifu na kujiamini kwa mwanachi wa kawaida.
.
.
Jambo lingine ambalo ndio msingi wa andiko langu ningependa hii chanjo waanze kupewa ndugu zetu wa dini ya kiislamu wanaokwenda kuhiji ili wawe na vigezo vya kuingia mji mtakatifu wa macca (kama sijakosea) na viongozi wa serikali ambao wanasafiri sana nje ya nchi ili tuepuke kila kiongozi aende kuchanjwa nje kila anaposafiri


Jambo la mwisho naomba nitoe angalizo kwa manaounga mkono chanjo na wanaopinga kuona haja kuja na suluhisho kila mmoja na huja mujarabu na sio matusi na kebehi kwa kila upande sisi ni watanzania na tunaijenga Tanzania moja tofauti zetu za kimtazamo zisifanye kuharibu umoja wetu wa kitaifa nadhani hii ni njia sahihi
.
.HITIMISHI:
SIJAWAHI CHANJWA IWE PEPOPUNDA POLIO WALA NINI HII ITAKUA CHANJO YANGU YA KWANZA NA NNA MIAKA ZAIDI YA 25 HOSPITALI SIIJUI NA KINGINE TOKA UMEINGIA HUU UGONJWA SIJAWAHI ONA WALA KUSIKIA KWA MTU JIRANI ANAUMWA HUU UGONJWA NAUSIKIA TUU REDIONI NA KWENYE RUNINGA NA KUSOMA KWENYE MAGAZETI NAWAPA POLE WALIOTANGIA MBELE ZA HAKI KWA HUU UGONJWA NA WANAOUMWA HUU UGONJWA NA KINACHONITIA HOFU WANAOKUFA NA HUU UGONJWA NI WATU WENYE PESA ZAO NAWASIWASI NIKIUPATA MIMI MASKINI SIJUI ITAKUAJE MUNGU NISAIDIE
.
.
 
Back
Top Bottom