REPOA: Utafiti wetu umebaini Watanzania wengi wana imani na Serikali ya Rais Samia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,045
49,728
Kwa mujibu wa Utafiti wa Repoa Watanzania Katika ngazi zote Wana Imani na Rais Samia na Serikali yake.

DAR: Utafiti uliofanywa na Taasisi inayojishughulisha na Utafiti, masuala ya Uchumi, Umaskini na Maendeleo ya Nchi ( Repoa), umeonesha Watanzania wana imani na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi wa Utafiti Repoa, Dk Lucas Katera amesema hayo alipokuwa akiwasilisha repoti ya Mpango wa Tisa wa Afro Barometer.

Amesema katika masuala ya uchumi, Watanzania wanahofia kuhusu kupanda kwa bei za vitu na ajira kwa vijana, lakini wana matumaini na muelekeo kama nchi kutokana na utendaji kazi wa serikali na kwenye baadhi ya mambo.

Amesema katika eneo la utawala na sheria, utafiti unaonesha kuwa asilimia 82 wa Watanzania wametoa maoni yao kuwa Rais anaheshimu Mahakama na Sheria, huku asilimia 81 maoni yaliyokusanywa yanaonesha Rais anaheshimu Mahakama.

Kwa upande wa imani katika taasisi za umma, Dk Katera amesema utafiti umebaini kuwa asilimia 82 raia wana imani na Rais, huku asilimia 78 wakionyesha imani yao kwa Bunge lakini pia asilimia 79 wana imani na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Habari Leo

 
Ndio tunayoyaweza haya.

Ukiwasikiliza wasanii wa bongo movie jinsi wanavyosifia movie na tamthilia zao huwezi kudhania kama ndio movie ambazo jambazi anavua viatu ili kuingia ndani akamuuwe mtu au jini anaangalia kwanza magari avuke barabara. Na ndio uongozi wa nchi yetu ulivyo, sifa nyingi kuliko hata kinachofanyika.

Mambo haya yanatufanya kuzidi kuchelewa kimaendeleo, hizo imani sijui zimejengwa kwa yapi?
 
Back
Top Bottom