Serikali yadai uhaba wa Chuma umesababisha kupanda bei ya Misumari na Nondo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
images (13).jpeg

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesema kupanda kwa bei ya nondo na misumari kumetokana na uhaba wa chuma ghafi na chakavu ambavyo ndio malighafi inayotumika kutengenezea bidhaa hizo.

Kigahe alibainisha hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi aliyehoji sababu za kupanda kwa bei ya bidhaa hizo.

Naibu Waziri huyo alisema kupanda kwa bei kunategemeana na soko la chuma duniani, akiwa na ufafanuzi kwamba viwanda vingi kwa sasa vinategemea chuma ghafi toka nje ya nchi.

"Bei hizi ni za kimataifa, ndio maana unaona bei inaongezeka, ndio maana tumeruhusu hata chuma chakavu kutoka nje kuuzwa hapa (nchini) ili kusaidia (kukabili) huo upungufu.

"Tunajitahidi kutoa taarifa sahihi kwa wakati kwamba kuna changamoto hizo na mpango wa serikali ni upi katika kuhakikisha bei inashuka.
 
Kuna jamaa mmoja alisema tujenge reli tayari tukishachimba chuma yetu naa tuitumie Mana gharama ya ujenzi ungepunguaje pia
 
..na badoo hatujaseeema...mpaka tuseeme!
Just imagine tuna uhaba wa chuma ghafi na huku chuma tunacho hapahapa, ni kweli uwekezaji wa kukichimba ni mkubwa , sio kwamba hatuwezi, sera na mipango ni tofauti na vipaumbele.
 
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesema kupanda kwa bei ya nondo na misumari kumetokana na uhaba wa chuma ghafi na chakavu ambavyo ndio malighafi inayotumika kutengenezea bidhaa hizo.

Kigahe alibainisha hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi aliyehoji sababu za kupanda kwa bei ya bidhaa hizo.

Naibu Waziri huyo alisema kupanda kwa bei kunategemeana na soko la chuma duniani, akiwa na ufafanuzi kwamba viwanda vingi kwa sasa vinategemea chuma ghafi toka nje ya nchi.

"Bei hizi ni za kimataifa, ndio maana unaona bei inaongezeka, ndio maana tumeruhusu hata chuma chakavu kutoka nje kuuzwa hapa (nchini) ili kusaidia (kukabili) huo upungufu.

"Tunajitahidi kutoa taarifa sahihi kwa wakati kwamba kuna changamoto hizo na mpango wa serikali ni upi katika kuhakikisha bei inashuka.
Serikali inashindwa kabisa kuwekeza kwenye uchimbaji wa chuma badala yake viwanda karibu vyote vya vyuma vinatumia chuma chakavu kutengeneza bidhaa za vyuma
 
Back
Top Bottom