runtown
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 820
- 1,089
Mkuu toa explaination kidogo ya mtu mmoja kumaliza miaka miwili tofautiNaona kuna watu wanataka wanachoamini wao ndio wanataka wengine waamini hivyo hivyo, ukitofautiana nao basi unaambulia matusi. this is not fair.
1. Kwanza makosa ya kibinadamu yapo. Kwa hiyo kilichotokea kinaweza kuwa kwa kukusudia au kimakosa
2. Hili la jina kutokea mara mbili au tatu huwa lipo. Na tatizo hili huwa linatokea lakini mfumo wa kiajira hulifuta. Kwa mfano mtu amepangiwa vituo viwili, anapofika kituo ambacho ameamua kwenda basi hufanyiwa uhakiki upya na kama kuna makosa haajiriwi na taarifa hutolewa kunako husika. Katika kituo kingine atakuwa hakuripoti hivyo hutolewa.
3. Ni vigumu mishahara kupigwa kwani hata mhusika akifanya mbinu za kuripoti sehemu mbili waajiri wana utaratibu wa kuhakiki payroll kwa wale watoro kwa hiyo mtu wa hivyo hataonekana kazini upande mmoja kwa zaidi ya siku tatu na atatolewa ripoti ya utoro.
4. Kwa utawala uliopo mtu atakayefanya hila za kuchakachua mishahara atakuwa ameamua kujitoa mhanga kitakachomtokea sisemi. Hivi mtu anaweza kuhatarisha ajira yake kwa mishahara ya watu watatu?
5. Mwisho kichwa cha habari kinaweza kuwa sahihi kwa idadi ya waliopita lakini watakao ripoti, hata kama idadi iliyotolewa iko sahihi bila makosa watakao ripoti sio wote, kuna wengine kwa kipindi cha tangu watume maombi watakuwa wamepata shughuli nyingine, au ajira nyingine au hata kufariki. Hapo kwa idadi pungufu (imeitwa hewa) haitakosekana.
NASUBIRI MATUSI KWA WASIOKUBALI MAWAZO TOFAUTI NA YAO - TUMEWAZOEA.