Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,705
- 36,157
Habari,
Watu wanaishia kulaumu majani na matawi huku wakisahau shinda na mizizi yake kuwa ndiyo chanzo cha mti kutokutoa matunda .
Serikali ya Tanzania imeweka kodi za kuumiza kila kona.
Ngoja nikupe mfano mmoja kutoka taasisi za mikopo midogo Mtandaoni.
Hizi Taasisi au microfinance hazina kiwango kikubwa cha riba kama watu wanavyopayuka ila serikali imeweka VAT kubwa , badala ya VAT kuchukua kwenye sehemu ya faida serikali inachukua VAT kwenye mkopo wenyewe.
Hii inawatesa wakopaji, pili hii inafanya watu wafilisike kwa kukosa wateja au kwa wateja kushindwa kulipa mikopo kandamizi.
Anayewakandamiza ni serikali.
Mikopo hii wangeitumia wajasiriamali wadogo kujikwamua katika biashara zao.
Riba ya mikopo hii inahint 35% ambayo mkopaji analazimika kuilipa ndani ya siku 5-6 tu ingawa wanatangaza kuwa mkopo ni wa siku 7.
Angalia hizi picha chini halafu nitakufafanulia. Huo mkopo wa kwanza ni mtu kakopa sh. 380000 ambapo riba ya mkopo wote ni 135000 ndani ya siku 5 . Serikali ikachukua VAT ya sh.78000 huku mwenye kampuni anayelipia Kodi ya pango , anayelipa watumishi anabaki na sh. 50000.
Huo mkopo wa pili ni sh. 510000 riba yake ni 180k ndani ya siku 5.
Nasema siku tano ni kwamba ukichukua leo tarehe 15 kwenye app yao inaonyesha marejesho ni tarehe 21 (six days) lakini tarehe 20 ya mwezi huu mapema saa tatu utapokea simu kuambiwa ni siku ya rejesho.
Kama hujalipa unaaibishwa, kwakuwa uli submit calls na sms za simu zako watawafahamisha watu wote uliowahi kuwasiliana nao kwa sms au calls. Ni zaidi ya aibu.
Hii mikopo ni ya hovyo, serikali iache ukatili kwa raia wake.
Baadaye BOT wanatoka hadharani kusema wakopaji wasiaibishwe mara talalila nyingi huku wao ndio wenye mamlaka ya kuzifungia hizi microfinance na wamekaa kimya kwakuwa wanazoa kodi nyingi haramu kutoka kwa hizi microfinance
Hao hao ndani ya app yao mkopo namba mbili ndio kuna maajabu zaidi ambayo huwezi kuyakuta nchi yoyote duniani.
Ukichukua 31 ndani ya siku 5 unapaswa kurejesha sh. 51.
Serikali ya Tanzania inayowataka vijana wawe wazalendo ndio waliopitisha huu ushetani.