Kilimanjaro: Serikali yasema inasubiri Wananchi watenge eneo ili ujenzi wa Shule ya Kigulunde uanze

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
HUU NDIO MUONEKANO WA SHULE YA MSINGI KUGULUNDE (5).jpg
Baada ya JamiiForums.com kusambaza picha zinazoonesha muonekano wa Shule ya Msingi Kigulunde iliyopo Kitongoji cha Mahande, Kata ya Mtii, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kutokuwa katika mazingira mazuri kutokana na uchakavu wa majengo, ufafanuzi umetolewa.

Andiko la kwanza hiki hapa - Muonekano wa Shule ya Msingi Kugulunde, miundombinu yake ni hatari kwa Wanafunzi na Walimu

Akizungumzia Shule hiyo ya Serikali, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Same, Anastazia Tutuba Ruhamvya anasema:

“Shule hiyo ni moja ya majengo ambayo yalijengwa miaka ya zamani, hivyo miundombinu yake pia ni chakavu. Ipo kwenye mpango wa ujenzi lakini ratiba yake haijafika kutokana na sababu kadhaa nitakazozifafanua.

“Shule hiyo ipo katika kwenye mkondo wa maji kutokana na mazingira ya eneo husika, Mwaka 2011 ilikumbwa na mafuriko na majengo yake mengi yakaharibika, ikabidi ifungwe na Wanafunzi wakahamishiwa kwenye shule nyingine za jirani kulinga na machaguo yao.

“Mwaka 2016 Wazazi wakaomba Shule ifunguliwe kwa kuwa waliona kuna uhitaji huo, hilo likafanyika lakini namba ya Wanafunzi haikuwa kubwa na wakati wa mitihani ya darasa la saba walikuwa wakienda kufanyia kwenye vituo vingine.

"Mwaka jana (2022) tulizungumza na Wananchi na maombi yao ya kuboreshwa shule yakaingizwa kwenye Bajeti ya mwaka 2022/23, mpango uliopo ni kujenga shule mpya kabisa sehemu nyingine kwa jina hilohilo kwa kuwa ene ilipo shule si salama.

"Wananchi wameonesha mwitikio mzuri wameshanunua matofali na mawe lakini changamoto ambayo ilikwamisha ni kuwa eneo la kujenga bado halijapatikana.

"Fedha zilipofika kipaumbele chao cha kwanza ilikuwa Kituo cha Afya ikabidi hilo ndilo lifanyiwe kazi. Serikali ipo tayari kusaidia na mara nyingi tunaangalia kipaumbele cha Wananchi wenyewe.

"Mwaka huu Wakati wa mvua kuna shule yenye Wanafunzi zaidi ya 500 katika Kata hiiyohiyo ilipata majanga ya paa kuezuliwa, vyoo vikatitia kutokana na mvua kubwa, hivyo fedha zikaelekezwa kuboreshwa shule huyo kutokana na wingi wa Wanafunzi.

"Kwa mazingira yalivyo katika Shule ya Kigulunde gharama za ujenzi ni kubwa na Serikai ipo tayari kushirikiana na Wananchi kujenga darasa la kwanza hadi la saba katika eneo ambalo watalichagua wenyewe.

"Serikali inaona na inafahamu kuwa mazingira ya Shule ya Kigulunde si mazuri, na ndio maana hata idadi ya Wanafunzi waliopo hapo ni chini ya 100."
HUU NDIO MUONEKANO WA SHULE YA MSINGI KUGULUNDE (3).jpg
 
Hongera sana upngozi wahalmashaur ya same, ila jaribuni kupita shule ya msingi Lugulu ,kwasekinga nazo miundombinu yake imechoka sana, Pia tunaomba umeme kijiji cha lugulu na shulee ya sekondary lugulu ipelekewe umeme
 
Back
Top Bottom