Serikali yaagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu

Waziri wa viwanda na biashara Dr Kijaji amezitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za Soda, Cement, Nondo na bidhaa nyingine kinyume cha utaratibu.

Dr Kijaji amesema uchunguzi umeonyesha kuwa wakati bidhaa hizo zinapandishiwa bei gharama za uzalishaji zilikuwa chini na hakukuwa na sababu yoyote ile ya kuongeza bei.

Source: ITV habari
Ni mwendawazimu pekee ndie atakayeamini serikali haina mkono kwenye hizi bei.
 
Waziri wa viwanda na biashara Dr Kijaji amezitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za Soda, Cement, Nondo na bidhaa nyingine kinyume cha utaratibu.

Dr Kijaji amesema uchunguzi umeonyesha kuwa wakati bidhaa hizo zinapandishiwa bei gharama za uzalishaji zilikuwa chini na hakukuwa na sababu yoyote ile ya kuongeza bei.

Source: ITV habari
Mambo ya hivi ndio huua uchumi,soko Lita adjust lenyewe
 
Si kuna mjinga na mpumbavu mmoja humu jf anasemaga ata marekani nayo vitu ni vimepanda bei na apost makala za huko ulaya ili kuonesha kuwa ni swala la kidunia .
 
Jamani mnalalamika nini na nchi ilishatangazwa ipo ktk uchumi wa kati?,hii inamaanisha watz wapo vizuri na ndio maana hawalalamiki
 
Waziri wa viwanda na biashara Dr Kijaji amezitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za Soda, Cement, Nondo na bidhaa nyingine kinyume cha utaratibu.

Dr Kijaji amesema uchunguzi umeonyesha kuwa wakati bidhaa hizo zinapandishiwa bei gharama za uzalishaji zilikuwa chini na hakukuwa na sababu yoyote ile ya kuongeza bei.

Source: ITV habari
Wafanyabiashara wenyewe ni wawili tuu nchi hii na wanafahamika. Wenye coca na pepsi. Sijui wanajizungusha nini kuwaita na kuwahoji.
Wakikana, waje dukani kwangu waanzie hapa, niwapeleke niliponunua ghali, napo watawapeleka waliponunua, hivyo hivyo hadi watapata muhusika
 
Ni wazi sasa wafanyabiashara wanashirikiana kupanga bei badala ya kuachia nguvu ya soko ili iamue.
 
Bei zinapanda kiajabu ajabu sana.nondo hazigusiki.ukienda kwenye vioo ndio usiseme.itabidi tujenge majumba ya udongo sasa
Mkihamia kwenye udongo na wenyewe tutapandisha bei ya mahitaji yote yanayohusika katika kukamilisha ujenzi 🐒
 
Serikali imeziagiza mamlaka zote za udhibiti kuchukua hatua kali dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni ili kuhakikisha bidhaa zinafika sokoni kwa wakati na bei shindani.

Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu Februari 7, 2022 na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk Ashatu Kijaji wakati akitoa tathimini ya mwenendo wa uzalishaji, usambazaji na bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu nchini.

“Ninawaelekeza wazalishaji na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela na kuuza bidhaa bila kuzingatia gharama halisi za uzalishaji na usambazaji,” alisema.

Pia amewaagiza wazalishaji wa vifaa vya ujenzi kuweka mifumo mizuri ya usambazaji wa vifaa ili kuzuia kupanda kwa bei kunakoweza kuzuilika.

Dk Kijaji amewataka maofisa biashara wa mikoa kote nchini waendelee kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasilisha taarifa hizo mara kwa mara kwenye wizara hiyo kupitia ofisi za makatibu tawala mikoa ili itakapobidi hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.

Amesema tathimini iliyofanyika nchini imwegundua kuwa ongezejko holela la bei ya vifaa vya ujenzui hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu.

Pia amesema ongezeko hilo wamebaini limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

“Gharama halisi za uzalishaji wa saruji haiakisiwi katika bei ya saruji iliyopo sokoni ikilinganishwa na uwiano huo katika nchi jirani na kwingineko duniani,”amesema.

Aidha, amesema wamebaini kuwa ongezeko la bei ya saruji na nondo halina uwiano halisi na gharama za usafirishaji na usambazaji na bei ya saruji iliyopo sokoni haina uhusiano na mwenendo wa nguvu za utashi wa mlaji na ugavi.

Dk Kijaji amesema kuna ucheleweshaji wa makusudi kwa utoaji wa saruji kutoka viwandani kwenda kwa wasambazaji na wanunuzi wa ndani hususani wale wasambazaji na wanunuzi wadogo ambao tayari wanakuwa wamekwisha lipia saruji husika tofauti na wanunuzi wa nje ambao hupatiwa saruji kwa urahisi zaidi.

Amesema pamoja na mambo mengine hali hiyo imesababisha wasambazaji kupandisha bei za saruji ili kufidia gharama zilizotumika kuchukua mzigo.

Chanzo: Mwananchi
 
Ndio mmegundua leo? Toka Mwaka Jana July bei za vifaa vya ujenzi iko juu
 
Dodoma. Serikali imeziagiza mamlaka zote za udhibiti kuchukua hatua kali dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni ili kuhakikisha bidhaa zinafika sokoni kwa wakati na bei shindani.

Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu Februari 7, 2022 na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk Ashatu Kijaji wakati akitoa tathimini ya mwenendo wa uzalishaji, usambazaji na bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu nchini.

“Ninawaelekeza wazalishaji na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela na kuuza bidhaa bila kuzingatia gharama halisi za uzalishaji na usambazaji,” alisema.

Pia amewaagiza wazalishaji wa vifaa vya ujenzi kuweka mifumo mizuri ya usambazaji wa vifaa ili kuzuia kupanda kwa bei kunakoweza kuzuilika.

Dk Kijaji amewataka maofisa biashara wa mikoa kote nchini waendelee kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasilisha taarifa hizo mara kwa mara kwenye wizara hiyo kupitia ofisi za makatibu tawala mikoa ili itakapobidi hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.

Amesema tathimini iliyofanyika nchini imwegundua kuwa ongezejko holela la bei ya vifaa vya ujenzui hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu.

Pia amesema ongezeko hilo wamebaini limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

“Gharama halisi za uzalishaji wa saruji haiakisiwi katika bei ya saruji iliyopo sokoni ikilinganishwa na uwiano huo katika nchi jirani na kwingineko duniani,”amesema.

Aidha, amesema wamebaini kuwa ongezeko la bei ya saruji na nondo halina uwiano halisi na gharama za usafirishaji na usambazaji na bei ya saruji iliyopo sokoni haina uhusiano na mwenendo wa nguvu za utashi wa mlaji na ugavi.

Dk Kijaji amesema kuna ucheleweshaji wa makusudi kwa utoaji wa saruji kutoka viwandani kwenda kwa wasambazaji na wanunuzi wa ndani hususani wale wasambazaji na wanunuzi wadogo ambao tayari wanakuwa wamekwisha lipia saruji husika tofauti na wanunuzi wa nje ambao hupatiwa saruji kwa urahisi zaidi.

Amesema pamoja na mambo mengine hali hiyo imesababisha wasambazaji kupandisha bei za saruji ili kufidia gharama zilizotumika kuchukua mzigo.
 
Tunapenda sana kutoa taarifa za wafanyabiashara wahuni wanaopandisha bei kiholela lakini hatuna mwongozo wa bei elekezi.

Kwa mfano bei elekezi ya kilo moja ya nyama au maharagwe.

Vinginevyo tutakuwa tunapiga siasa tu!

Maendeleo hayana vyama.
 
Back
Top Bottom