Serikali yaagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,902
141,842
1644311477256.png


Waziri wa viwanda na biashara Dr Kijaji amezitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za Soda, Cement, Nondo na bidhaa nyingine kinyume cha utaratibu.

Dr Kijaji amesema uchunguzi umeonyesha kuwa wakati bidhaa hizo zinapandishiwa bei gharama za uzalishaji zilikuwa chini na hakukuwa na sababu yoyote ile ya kuongeza bei.

Source: ITV habari

========

Serikali imeziagiza mamlaka zote za udhibiti kuchukua hatua kali dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni ili kuhakikisha bidhaa zinafika sokoni kwa wakati na bei shindani.

Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu Februari 7, 2022 na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk Ashatu Kijaji wakati akitoa tathimini ya mwenendo wa uzalishaji, usambazaji na bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu nchini.

“Ninawaelekeza wazalishaji na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela na kuuza bidhaa bila kuzingatia gharama halisi za uzalishaji na usambazaji,” alisema.

Pia amewaagiza wazalishaji wa vifaa vya ujenzi kuweka mifumo mizuri ya usambazaji wa vifaa ili kuzuia kupanda kwa bei kunakoweza kuzuilika.

Dk Kijaji amewataka maofisa biashara wa mikoa kote nchini waendelee kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasilisha taarifa hizo mara kwa mara kwenye wizara hiyo kupitia ofisi za makatibu tawala mikoa ili itakapobidi hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.

Amesema tathimini iliyofanyika nchini imwegundua kuwa ongezejko holela la bei ya vifaa vya ujenzui hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu.

Pia amesema ongezeko hilo wamebaini limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

“Gharama halisi za uzalishaji wa saruji haiakisiwi katika bei ya saruji iliyopo sokoni ikilinganishwa na uwiano huo katika nchi jirani na kwingineko duniani,”amesema.

Aidha, amesema wamebaini kuwa ongezeko la bei ya saruji na nondo halina uwiano halisi na gharama za usafirishaji na usambazaji na bei ya saruji iliyopo sokoni haina uhusiano na mwenendo wa nguvu za utashi wa mlaji na ugavi.

Dk Kijaji amesema kuna ucheleweshaji wa makusudi kwa utoaji wa saruji kutoka viwandani kwenda kwa wasambazaji na wanunuzi wa ndani hususani wale wasambazaji na wanunuzi wadogo ambao tayari wanakuwa wamekwisha lipia saruji husika tofauti na wanunuzi wa nje ambao hupatiwa saruji kwa urahisi zaidi.

Amesema pamoja na mambo mengine hali hiyo imesababisha wasambazaji kupandisha bei za saruji ili kufidia gharama zilizotumika kuchukua mzigo.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa namna jambo hili lilivyo kaa inapaswa Rais atoe kauli, si jambo dogo hili!

Wananchi wameumizwa sana na uandaaji wa bei za didhaa mbalimbali nchini.

Hasa mafuta ya kula, sukari, na vifaa vya ujenzi
 
Bei zinapanda kiajabu ajabu sana.nondo hazigusiki.ukienda kwenye vioo ndio usiseme.itabidi tujenge majumba ya udongo sasa
Mkuu juzi tu nineenda kuuliza bati jeupe geji 30 ilikua 22500 leo naenda wananiambia 25 hizo nondo nazo ni hatari yaan maboma yetu naona tutayaacha yapigwe mvua tu
 
Back
Top Bottom