Serikali yaagiza eneo la Shishi Food livunjwe ndani ya siku 3 kutoka leo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mchana wa leo Januari 18, 2023, msanii na Mfanyabiashara Shilole amelazimika kulivunja eneo lake la Biashara la Shishi Food iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam baada ya kupokea Barua ya Maelekezo kutoka Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni iliyomuelekeza kuondoa biashara hiyo kwenye eneo iliyopo ndani ya siku tatu.

Taarifa inaeleza kuwa eneo hilo linatakiwa kutumika katika kupanua eneo la kituo cha Afya na hivyo Shilole kulazimika kutafutiwa eneo jingine la kufanyia biashara yake.

Shilole amesema “Ni tamko la leo rasmi, Shishi Food hatutakuwa na huduma ya chakula ili kupisha ujenzi wa kituo cha Afya, nikiwa kama mpenda maendeleo na mwanajamii ninayeunga jitihada za Serikali nimelipokea.

“Namshukuru Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kwa kuniwezesha kupata eneo lingine mbadala, nawashukuru wote ambao mmeshiriki kunitafutia eneo lingine kwa kuwa ni lazima tubomoe kila kitu ili tuendelee kutoa ajira kwa vijana.”
 
Vipi kuhusu gharama za kuvunja na kujenga eneo lingine,ni nani atakayegharamia hiyo gharama?

Nauliza tu ili nijue.
 
Huyo kada wa ccm, wanajua wanavomalizana wenyewe, ila angekuwa upande mwingine angejua hajui.
 
Bora huyo atatafutiwa.😁
Hii nchi hii! Ningekuwa mie ningekuja kuweka 'Shishi food' yangu sebuleni.
 
Back
Top Bottom