Serikali: Mtambo wa Megawati 20 mfano wa Injini ya Boeing 747 umewasili kutatua changamoto ya umeme Mtwara na Lindi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Serikali imesema imeendelea kutekeleza ahadi ya kupeleka umeme wa uhakika katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ameongoza mapokezi ya mtambo wa Megawati 20 utakaozalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia, mchakato ambao umefanyika Februari 9, 2024.

Amesema mtambo huo aina ya TM16 wenye mfano wa injini ya ndege ya Boeing 747 utafungwa katika Kijiji cha Hiari, Wilaya ya Mtwara Vijijini ikiwa ni maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa changamoto ya upatikanaji umeme kwenye mikoa hiyo inatatuliwa.
WhatsApp Image 2024-02-09 at 18.20.12_603dedad.jpg

WhatsApp Image 2024-02-09 at 18.20.16_3bb24e88.jpg

WhatsApp Image 2024-02-09 at 18.20.09_2ea56b4c.jpg
Akipokea mtambo huo kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema kuwa mtambo huo utaondoa changamoto ya upatikanaji wa umeme kwenye Mkoa wa Lindi na Mtwara.

“Mhe. Rais alitoa maelekezo kwa Wizara ya Nishati, kufanya kila jitihada ili changamoto ya umeme kwenye mikoa hiyo itatuliwe kwa haraka, tunashukuru leo tumeweza kutimiza ahadi hiyo kwani mtambo huu ni miongoni mwa mitambo ya kisasa kabisa ya umeme iliyowahi kuletwa nchini ambayo inatoa uhakika wa kuzalisha umeme kwa kipindi kirefu,” amesema Mramba.
WhatsApp Image 2024-02-09 at 18.20.11_20d3c0a6.jpg

WhatsApp Image 2024-02-09 at 18.20.23_90bcc2d1.jpg
Aidha, Mhandisi Mramba ameongeza kuwa, maelekezo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kuhusu kupeleka umeme wa gridi kwenye mikoa hiyo yameshaanza kutekelezwa ambapo kabla ya mwezi wa sita mwakani umeme wa Gridi ya Taifa utakuwa umefika kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara.

Kuhusu maelekezo aliyoyatoa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ya kuhakikisha wananchi wa mikoa hiyo inayozalisha gesi kwa wingi wananufaika na uwepo wa nishati hiyo, amesema tayari wameanza kuboreshewa huduma mbalimbali ikiwemo kuwajengea kituo cha Polisi, ununuzi wa boti ya kisasa kwa ajili ya usafiri wa wananchi eneo la Songosongo mkoani Lindi na ujenzi wa kituo cha afya eneo la Madimba mkoani Mtwara..

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed alisema kuwa, wananchi wa Mtwara wamepokea kwa furaha mtambo huo ambao utafungua fursa za uwekezaji kwa kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika kwani takriban asilimia 80 ya matumizi ya umeme mkoani humo yanatumika kwenye sekta ya biashara.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt. Samia kwa kutimiza ahadi yake na na mapenzi ya dhati aliyoyaonyesha kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara na kufanya mikoa hii kupata umeme wa uhakika ambao utainua sekta ya uchumi kwa ujumla.” Amesema Kanali Ahmed.

Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Kilumbe Ng’enda ameishukuru Serikali kupitia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko kwa kusikiliza kilio cha wabunge wa mikoa juu ya changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuipongeza Wizara ya Nishati kwa hatua kubwa inazochukua kuhakikisha sekta ya umeme inaimarika.
 
Hebu katika picha hiyo zungushia na useme huu ndio mfano wa injini ya boeing 747!

Sisi wengine hatuijui injini ya hoeing 747 inafanaje! Au hilo limtambo lote lililo juu ya tera la lori ndio linafanana na injini ya boeing 747?

Au unamaanisha nini unaposema mtambo unafanana na injini ya boeing 747?
 
Mtambo wa megawati 20 kuzalisha umeme Mtwara ma Lindi

[https://habarileo]

MIKOA ya Mtwara na Lindi imepokea mtambo mkubwa na kuzalisha umeme wa megawati 20 unaotarajiwa kuanza kazi kufanya kazi Machi 31, 2024.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema mtambo huo unaenda kumaliza tatizo la umeme kwenye mikoa hiyo miwili.

Hayo yamesemwa wakati wa zoezi la ukaguzi wa mtambo huo wa kuzalisha umeme lililofanyika leo Februari 9, 2024 katika kijiji cha Hiari halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Amesema anafahamu namna ambavyo nishati hiyo ilivyokuwa kero kwa wananchi wa mikoa hiyo.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyofanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara alitoa maelekezo mahususi kwa mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko kuhusu hali ya umeme katika mikoa hii”

“Na kusema ukweli kwa maelekezo yale aliyoyatoa haikuwezekana tupate usingizi”amesema Mramba

“Mtambo huu mnaouona hapa umeletwa kwa maelekezo ya mheshimiwa Rais aliyoyatoa kwa Naibu Waziri Mkuu na yeye baada ya kupokea maelekezo hayo aliyasimamia”

Mkuu wa Mkoa Mtwara Kanali Amhed Abbas amesema upatikanaji wa mitambo hiyo inaenda kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo na ile dhana ya kuifungua mikoa hiyo inaenda kutimia.

Aidha sasa mikoa hiyo inaenda kuwa na umeme unaojitosheleza na mwingine wa ziada kwenye uwekezaji wa shughuli zingine mbalimbali za kimaendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba mkoani Mtwara, Abdallah Chikota amesema mikoa hiyo bila uwepo wa nishati ya uhakika haiwezi kufunguka.
 
Hongera kwa serikal ya awamu ya (vi)hongera mama samia hongera naibu waziri mkuu na waziri wa nishati kwa kujali wanachi wenu 2025 kura bwererere kutoka kusin, yaan mbaazi ufuta halaf kura tumpe mpinga maendeleo
 
Mtambo wa megawati 20 kuzalisha umeme Mtwara ma Lindi

[https://habarileo]

MIKOA ya Mtwara na Lindi imepokea mtambo mkubwa na kuzalisha umeme wa megawati 20 unaotarajiwa kuanza kazi kufanya kazi Machi 31, 2024.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema mtambo huo unaenda kumaliza tatizo la umeme kwenye mikoa hiyo miwili.

Hayo yamesemwa wakati wa zoezi la ukaguzi wa mtambo huo wa kuzalisha umeme lililofanyika leo Februari 9, 2024 katika kijiji cha Hiari halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Amesema anafahamu namna ambavyo nishati hiyo ilivyokuwa kero kwa wananchi wa mikoa hiyo.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyofanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara alitoa maelekezo mahususi kwa mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko kuhusu hali ya umeme katika mikoa hii”

“Na kusema ukweli kwa maelekezo yale aliyoyatoa haikuwezekana tupate usingizi”amesema Mramba

“Mtambo huu mnaouona hapa umeletwa kwa maelekezo ya mheshimiwa Rais aliyoyatoa kwa Naibu Waziri Mkuu na yeye baada ya kupokea maelekezo hayo aliyasimamia”

Mkuu wa Mkoa Mtwara Kanali Amhed Abbas amesema upatikanaji wa mitambo hiyo inaenda kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo na ile dhana ya kuifungua mikoa hiyo inaenda kutimia.

Aidha sasa mikoa hiyo inaenda kuwa na umeme unaojitosheleza na mwingine wa ziada kwenye uwekezaji wa shughuli zingine mbalimbali za kimaendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba mkoani Mtwara, Abdallah Chikota amesema mikoa hiyo bila uwepo wa nishati ya uhakika haiwezi kufunguka.
Mmekodi kama ule wa Richmond au tumenunua?
 
Serikali imesema imeendelea kutekeleza ahadi ya kupeleka umeme wa uhakika katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ameongoza mapokezi ya mtambo wa Megawati 20 utakaozalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia, mchakato ambao umefanyika Februari 9, 2024.

Amesema mtambo huo aina ya TM16 wenye mfano wa injini ya ndege ya Boeing 747 utafungwa katika Kijiji cha Hiari, Wilaya ya Mtwara Vijijini ikiwa ni maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa changamoto ya upatikanaji umeme kwenye mikoa hiyo inatatuliwa.
Akipokea mtambo huo kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema kuwa mtambo huo utaondoa changamoto ya upatikanaji wa umeme kwenye Mkoa wa Lindi na Mtwara.

“Mhe. Rais alitoa maelekezo kwa Wizara ya Nishati, kufanya kila jitihada ili changamoto ya umeme kwenye mikoa hiyo itatuliwe kwa haraka, tunashukuru leo tumeweza kutimiza ahadi hiyo kwani mtambo huu ni miongoni mwa mitambo ya kisasa kabisa ya umeme iliyowahi kuletwa nchini ambayo inatoa uhakika wa kuzalisha umeme kwa kipindi kirefu,” amesema Mramba.
Aidha, Mhandisi Mramba ameongeza kuwa, maelekezo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kuhusu kupeleka umeme wa gridi kwenye mikoa hiyo yameshaanza kutekelezwa ambapo kabla ya mwezi wa sita mwakani umeme wa Gridi ya Taifa utakuwa umefika kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara.

Kuhusu maelekezo aliyoyatoa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ya kuhakikisha wananchi wa mikoa hiyo inayozalisha gesi kwa wingi wananufaika na uwepo wa nishati hiyo, amesema tayari wameanza kuboreshewa huduma mbalimbali ikiwemo kuwajengea kituo cha Polisi, ununuzi wa boti ya kisasa kwa ajili ya usafiri wa wananchi eneo la Songosongo mkoani Lindi na ujenzi wa kituo cha afya eneo la Madimba mkoani Mtwara..

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed alisema kuwa, wananchi wa Mtwara wamepokea kwa furaha mtambo huo ambao utafungua fursa za uwekezaji kwa kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika kwani takriban asilimia 80 ya matumizi ya umeme mkoani humo yanatumika kwenye sekta ya biashara.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt. Samia kwa kutimiza ahadi yake na na mapenzi ya dhati aliyoyaonyesha kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara na kufanya mikoa hii kupata umeme wa uhakika ambao utainua sekta ya uchumi kwa ujumla.” Amesema Kanali Ahmed.

Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Kilumbe Ng’enda ameishukuru Serikali kupitia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko kwa kusikiliza kilio cha wabunge wa mikoa juu ya changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuipongeza Wizara ya Nishati kwa hatua kubwa inazochukua kuhakikisha sekta ya umeme inaimarika.
Wacheni uwongo hilo li mtambo wamelitoa Ubungo na limetumika pale muda mrefu.
 
Mtambo wa megawati 20 kuzalisha umeme Mtwara ma Lindi

[https://habarileo]

MIKOA ya Mtwara na Lindi imepokea mtambo mkubwa na kuzalisha umeme wa megawati 20 unaotarajiwa kuanza kazi kufanya kazi Machi 31, 2024.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema mtambo huo unaenda kumaliza tatizo la umeme kwenye mikoa hiyo miwili.

Hayo yamesemwa wakati wa zoezi la ukaguzi wa mtambo huo wa kuzalisha umeme lililofanyika leo Februari 9, 2024 katika kijiji cha Hiari halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Amesema anafahamu namna ambavyo nishati hiyo ilivyokuwa kero kwa wananchi wa mikoa hiyo.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyofanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara alitoa maelekezo mahususi kwa mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko kuhusu hali ya umeme katika mikoa hii”

“Na kusema ukweli kwa maelekezo yale aliyoyatoa haikuwezekana tupate usingizi”amesema Mramba

“Mtambo huu mnaouona hapa umeletwa kwa maelekezo ya mheshimiwa Rais aliyoyatoa kwa Naibu Waziri Mkuu na yeye baada ya kupokea maelekezo hayo aliyasimamia”

Mkuu wa Mkoa Mtwara Kanali Amhed Abbas amesema upatikanaji wa mitambo hiyo inaenda kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo na ile dhana ya kuifungua mikoa hiyo inaenda kutimia.

Aidha sasa mikoa hiyo inaenda kuwa na umeme unaojitosheleza na mwingine wa ziada kwenye uwekezaji wa shughuli zingine mbalimbali za kimaendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba mkoani Mtwara, Abdallah Chikota amesema mikoa hiyo bila uwepo wa nishati ya uhakika haiwezi kufunguka.
wenye gas yao wanapelekewa mtambo, basi sawa
kula kwa urefu wa kamba
 
Kwani tuna upungufu wa kiasi gani mpaka mseme 20MW itatatua tatizo?
  • Demand ya Mtwara yote ni kiasi gani?
  • Plant ya Tanesco waliyoiridhi kutoka kwa ALTMAS, ina megawatt ngapi kama installed capacity na ngapi ziko active?
  • Manunuzi ya 20MW turbine hiyo yalifanyika lini?

Bwawa la Nyerere, 2115MW ndio mwiba wa upungufu, lini linakamilika?
  • Installed capacity ya nchi zima ni 1660MW
  • Installed ya bwawa moja tu ni 2115MW

Kwanini hatu-push kukamilisha hilo? Hatuoni kuwa bwawa moja hilo, sio tu litaondoa upungufu, ila litachochea kufufua hiyo mitambo chakavu yenye jumla ya 1660MW?
  • Ambapo baada ya pengine mwaka mmoja wa Bwawa la Nyerere kutembea, tutakuwa tumefufua hizo 1660MW na hivyo kutufanya kuwa na 3700MW?
  • Lengo la miaka 5 ni kufikia 5000MW by 2025, tutafanikiwa?

Hopeless country.
 
Ni jambo jema sana japo sijaelewa
Huo ni mtambo wa kufua gesi yetu ya Asilia itoe umeme au ni Generator la kutumia mafuta?
Nimeuliza hivyo kwa sababu, tuliambiwa Stigler's na vyanzo vingine vya umeme vilivyopo tayari vitatoa umeme wa Kutosha Nchi nzima na kuwe na ziada
Sasa kama tumeamua kutumia mabilioni kununua Generator badala ya kukamilisha Stiglers mnazidi kunichanganya....
 
Back
Top Bottom