Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Akizungumza na Walimu katika Mkutano Mkuu wa tisa wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) katika Ukumbi wa Taasisi ya Utalii Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa amesema kumfundisha mtoto ndani ya chumba hakumpi nafasi Mwanafunzi kujifunza kwani Watoto wanahitaji eneo la kutosha ili kujifunza.
Lela amesema haya yanafanyika kutokana na baadhi ya wazazi kuendelea kuwapeleka watoto wao katika maeneo hayo ambayo hayakidhi vigezo vya kuwafundisha Watoto hasa ngazi ya awali.
Pia soma:
~ Matukio ya Ukatili wa Kijinsia yaripotiwa kuongezeka Visiwani Zanzibar
~ Uhalifu 2023: Zanzibar yaongoza ubakaji, Arusha yaongoza ulawiti
~ Kuepusha ulawiti, walimu wa madrassa wawe wanawake tu!