Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,965
Wabunge wa Ufaransa wamepitisha mswada ambao utawapiga marufuku vijana wa chini ya umri wa miaka 15 nchini humo kuwa katika mitandao ya kijamii.
Mswada huo uliopitishwa katika Bunge la kitaifa sasa utapelekwa kwa Baraza la Seneti ili kupitishwa kuwa sheria. Rais Emmanuel Macron ameitaja kuwa hatua muhimu kuelekea kuwalinda watoto wa Ufaransa. Maafisa wa Serikali wanatumai kuwa mswada huo utaidhinishwa haraka kuwa sheria ili ianze kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka mpya wa masomo nchini humo unaoanza mwezi Septemba.
Sheria hiyo ikipitishwa,itapiga pia marufuku wanafunzi kwenda shuleni na simu za mkononi.