Serikali ya Wanafunzi-UDSM yatoa saa 72 kwa HESLB kutimiziwa maagizo yao vinginevyo kukusanyika nje ya ofisi ya HESLB

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imetoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo (HESLB) kutekeleza maagizo 4 likiwamo kuwaingizia fedha wanafunzi ambao hawajapewa tangu chuo hicho kifunguliwe, yasema isipotekeleza watakusanyika nje za ofisi ya HESLB.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Daruso, Judith Mariki ilisema wamefikia uamuzi huo baada ya changamoto ya kukosekana kwa mikopo kwa wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza tangu chuo kifunguliwe huku baadhi ya wanafunzi wanaoendelea wakikatwa fedha zao.

DARUSO wamesema kuwa baada ya muda huo wanafunzi wote ambao hawajilipwa mikopo , wamekatwa mikopo yao, wamepewa mikopo kwa waliokata rufaa na kubadili Ofisa mikopo wa chuo hicho wataandamana nje ya ofisi za bodi hiyo

“Wanafunzi wamevumilia vya kutosha na mazungumzio yamefanyika vya kutosha, ahadi za uongo tumepewa za kutosha, hivyo endapo saa 72 zitaisha bila mambo hayo yote kutekelezwa kwa pamoja, Daruso tukutane nje ya ofisi ya ofisa mikopo ili kwa umoja wetu tuelekee HESLB.” imenukuliwa Taarifa hiyo

Zaidi, soma:

1.jpg
 
Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) imetoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa, vinginevyo wanafunzi watakutana nje ya ofisi za bodi hiyo zilizopo Mwenge Dar es Salaam Desemba 19, 2019.

Taarifa iliyotolewa jana Jumapili Desemba 15, 2019 na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Daruso, Judith Mariki ilisema wamefikia uamuzi huo baada ya changamoto ya kukosekana kwa mikopo kwa wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza tangu chuo kifunguliwe huku baadhi ya wanafunzi wanaoendelea wakikatwa fedha zao.

Mariki alisema baada ya juhudi kubwa ya kufuatilia na mazungumzo kugonga mwamba, serikali imefanya mazungumzo ya ndani kwa ndani iliyojumuisha mihimili mitatu ya serikali hiyo.
 
Hivi sheria ipo vipi kuhusiana mikopo:!?

Ni jambo la lazima kukopeshwa au ni misaada tu???

Unaomba kupewa pesa bado unakuwa mkali... Imekaaje hii wajuvi wa daruso?

Sent using Jamii Forums mobile app
kwenye kukata kwenye kupandisha makato mpakaasilimia ngapi huko sijui walijadiliana hata kidogo na wanaokatwa? Mmekubaliana nitakukopesha na mkataba mmefunga kwann usibipe changu
 
Tumeshinda kwa kishindo serikali za mitaa, hivyo msitusumbue. Alisikika mtu mmoja kutoka lumumba fc akisema hivyo. Poleni sana mliopatwa na hiyo kadhia.
 
Yaani nikukumbuka kile kipigo cha Wale mashetani wanaovaa vikofia vyekundu. Sitaki kabisa hiyo habari yenu mpaka Leo began langu halijakaaga sawa yaani nilitandikwa rugu. Kama nawaona vile wanaudsm na wanavyopenda chips vidole laini kama wote wanawake watakavyozamishwa Kwenye mitaro na kipigo cha mbwa koko. Eti mihimili yote aaaaaahaaaa kichuo eti kila dola umesahau dola lazima iwe na jeshi. Wale jamaa wamefanya sana mazoezi halafu hawajapata hata vurugu moja wala maandamano tokea aingie jpm. Sasa wewe chuma janga ule na nduguzo usisahau kufukuzwa chuo na kwenda jela vyote vitakuhusu. Kama nakuona vile utakapokuwa unaelekea segerea na umevaa date zilizoandikwa maboresho magereza, utakapokutana wafungwa ambao hawajaona wake zao tokea mwaka. 1980 .Kama wewe unafikiri kukopeshwa ni lazima nenda kaandamane.

Punguza uoga mzee
 
Back
Top Bottom